barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
UFAFANUZI: INJILI NDANI YA SIASA.
Hoja na ombi la mmoja wa wasomaji wa ukurasa wangu kuwa niache siasa niwaunge kuhubiri injili imetafsiriwa kuwa ni mimi ndio nataka kuacha siasa na kuingia kuhubiri.
Jibu langu kuwa kazi ya injili ni kazi njema lakini kwa sasa nitafanya injili ndani ya siasa lina maana ya kujikita zaidi katika siasa, si kuacha.
Ninaamini kuwa siasa za tanzania zinahitaji vionjo vingi kuleta ubora.
Ninafikiri wito wa kiinjili yaani habari njema ya kufungua maisha ya watu kupitia sera bora za maendeleo, kuwasemea wasio na sauti , kushauri, kuelekeza, kufundisha nk ndio maana yake na ndio maana ya kusema huu ni utume maalum, si wa kupuuza na si wa kuacha kirahisi.
Ninaamini ninaeleweka sasa.