Anime

Anime

Tatizo 3D kali zinatoka chache kwa mwaka na nyingi ni single so ukiangalia chap tu inaisha. Halafu ni nadra sana kukuta zina maudhui kama ya Anime kama demon hunting, violence, killings, Actions nk.
Ila Transformers One ilikuwa ni single ya 3D ya 2024 ile ilikuwa kali kinoma kwenye Action
Hizi za Disney (Pixar) na Universal (Illumination & DreamWorks) huwa zimebase kwenye comedy na zinalenga sana watoto
Mi ninachofanya naangalia zote za 3D na Anime ili nipate ladha zote mbili. Hakinipiti kitu 😅😅
3d Animation sijaangalia kitambo na kama niliangalia nadhan huwa naludia Rango tuu
 
Habari wana Jamii Forums!
Nimekuwa nikifuatilia sana mijadala hapa JF, na nimegundua kuna uhaba wa mada kuhusu Anime na Manga, hususan zile za Kijapani. Mimi ni mgeni kwenye ulimwengu huu, nimeanza kuangalia Anime mwaka 2024 na nimezipenda sana! Nilishangaa sana kuona hakuna mada rasmi kuhusu hili hapa JF hadi leo.
Kwa wale ambao hamjui, Anime ni filamu za katuni zinazotengenezwa nchini Japani. Zina mtindo wa kipekee wa michoro na hadithi mbalimbali, kuanzia vichekesho, kusisimua, mapenzi, hadi sayansi. Manga kwa upande mwingine, ni vitabu vya katuni au riwaya za picha za Kijapani ambazo mara nyingi huwa ndio chimbuko la hadithi za Anime.
Kwanini Anime Inavutia?
Kuna mambo mengi yanayofanya Anime ivutie:
* Hadithi Pekee: Zina hadithi za kusisimua na zenye undani, zinazokuvuta na kukuweka mtegoni.
* Wahusika Wenye Undani: Wahusika wake huwa na maisha halisi, matatizo, na ndoto, unajikuta unaelewana nao kirahisi.
* Ubunifu wa Michoro: Michoro ni ya kipekee na yenye ubunifu wa hali ya juu, inakupa picha halisi ya matukio.
* Maadili na Mafunzo: Mara nyingi zinafundisha maadili na masomo muhimu ya maisha.
Mifano ya Anime Maarufu Zilizoshinda Tuzo
Kuna Anime nyingi zilizofanya vizuri na kutambulika kimataifa. Baadhi ya hizo ni pamoja na:
* Spirited Away: Imeshinda tuzo ya Oscar kwa Filamu Bora ya Uhuishaji.
* Your Name. (Kimi no Na wa.): Imepokea tuzo nyingi na kuvunja rekodi za mapato duniani.
* Demon Slayer: Kimetsu no Yaiba: Imeshinda tuzo mbalimbali ikiwemo "Anime of the Year."
* Attack on Titan: Maarufu sana kwa hadithi yake tata na yenye kusisimua.
Nimeona inafaa kufungua mada hii ili tupate nafasi ya kujadili na kushiriki uzoefu wetu kuhusu Anime na Manga. Karibuni sana tushiriki mawazo, tuulizane maswali, na kupendekeza Anime/Manga nzuri!
Je, kuna wengine hapa mnaopenda Anime
? Tuanze mjadala!
View attachment 3411124View attachment 3411125View attachment 3411126View attachment 3411127View attachment 3411128
Shida ya hizi katuni hazina maadili
 
Browser na app vyote natumia
Nishakuambia hakinipiti kitu 😅😅
Kwel haupitwi na kitu me ni mtalaamu wa Browser

Kwenye browser nenda kwenye message hiyo ya Mwananchi B Quote baada ya hapo nenda kwenye message ya kwanza pale juu bonyeza sehemu ya kuedit watakuletea sehemu ya insert Quote utaweka

Ili mtu aeelewa kabla hujaauote andika baadhi ya recommendations zilizotolewa na wadau then una insert Quote yako hapo chini
 
cheko na kutembea kwake 🤣
One of my Favourite characters.

Hapa wanafuatia.

1. Boa Hancock - Mtoto mkali ana Pozi sana huyu ila ni Very Deadly - (Warlord of Sea).

2. Marshall .D. Teach - Huyu mwamba muda wote anacheka na very unpredictable, Mpaka Leo sijui mwamba anawaza nini. (Emperor of the Sea).

3. Big Mom - Kwanza Picha linaanza ana Watoto 85, Huyu cheko lake lile "Mama mama." Ujue umeondoka. ( Emperor of the Sea)
 
Ukishatoa One peace mwingine anayenitia uvivu ni Black Clover 😃😃ila hii ngoja nijikaze week ijayo niishushe nianze mdogo mdogo episode 100+ sio pow😃😃
Ha ha ha Mimi Black Clover nasubiria Muendelezo maana niliimaliza.

One Piece saizi inaendelea ila nasubiria zifike angalau 50 hivi ndio niendelee mdogo mdogo.
 
Ha ha ha Mimi Black Clover nasubiria Muendelezo maana niliimaliza.

One Piece saizi inaendelea ila nasubiria zifike angalau 50 hivi ndio niendelee mdogo mdogo.
Huwa una moyo wa kuzingojea zijae jae 😃😃me hicho kipaji sina😃😃Solo leveling baada ya S2Ep1 Nilitafuta manga ilipo nikasoma yote na bado ikawa ikitoka nipo nayo siku hiyo hiyo
 
Back
Top Bottom