Anguko sasa ni dhahiri

Ungekuwa hujakielewa ungeniuliza in the first place hukufanya hivyo....!mimi sijakuelewa ndio maana nikakuomba ufafanuzi...hivi vingine ulivyoandika havikusaidii hata wewe mwenyewe
Wakati mwingine unaweza kuwa unapambana na Jesca,hapo utegemee nini

Wengine ni viherehere tuu na vipayukaji

Achana navyo vijione vyenyewe vipumbavu
 
Watawala wengi wasiopenda kushauriwa na wananchi na viongozi wengine waandamizi katika serikali zao wameshindwa kuongoza mataifa yao ...

Uongo utakupa ushindi wa siku moja Ukweli utakupa ushindi moja kwa moja.

Haya ya juu imekaa kinadharia ikisukumwa na nguvu za hisia kuliko uhalisia. Japo ungetoa mfano kiongozi gani hapa nchini umemfananisha na hao viongozi uliowatolea mfano.

Utawala wa kidemokrasia una njia nyingi za kuzuia kiongozi kuhodhi madaraka kwani demokrasia tafsiri nyepesi ni utawala wa wengi.

Haya yako ya mwisho inatoa taswira ya uwewe.
 

sinauhakika na unakoishi huenda kweli umeme sio wa uhakika,but trust me tokea prof Muhongo apewe wizara,huku kwetu umeme unanguvu na haukatikiti katikik kama zamani.ndio akili ya waafrika wengi,hupata furaha pale mwenzao anaposhindwa na pengine kabisa waga wanatumia nguvu na akili nyingi iliashindwe then wanarudi kusema,ooo si tuliwaambia atashindwa? let us be objective.
 

Wanaostahili lawama, ni waliojifungia "chumbani" na vijikaratasi vyao mifukoni vyenye majina mtoto wa "shemeji" na "baba mdogo" , mwisho wa siku wakaamua wafanye sandakalawe ili hali wakijua kuna mamilioni ya watanzania wanaumia na wataumia kwa mchezo wao wa sandakalawe.
 
Sina milioni saba wala wadhamini wawili wenye noti, ngoja nigugumie tu ndani kwa ndani na kuchangia kimoyomoyo huku nikiweka like.
 
Kuna mtu alishawahi kukushikia akili yako, husiandike hayo uliyokua unayaona wewe?
Kwani umeelewa nini kwenye post au uzi wa mshana jr? Na Mwisho umejifunza nini?
 
Unafki nao ni sehemu ya maisha kwa watu wanafki. Mnafki hutumia jina la muumba kuhalalisha unafiki. Tatizo kubla wanafiki huwa wakifanya unafiki wanasahau kuwa walishafanya unafiki. Unafiki ni sehemu ya maisha ya mnafiki.
 
Tunatonesha vidonda kwa kuvitia chumvi na ndimu..tunahubiri chuki na visasi

Nilidhani siasa zimekwisha na sasa ni kazi tu, kumbe ndiyo kwanza vijembe vya mjengoni vimehamia kwenye majukwaa. Ingelikuwa busara kama JPM wakati wa ziara zake mikoani angejikita zaidi kwenye mipango kufanikisha dira yake ya TZ ya viwanda na kuondoa umaskini badala ya kuendeleza vijembe. Je vijembe na chuki za kisiasa ndivyo vitaleta viwanda?
 
Aisee mkuu, nashukuru kama ulifatilia taarifa husika, yani wakati wamekaa bungeni wanapitisha maamuzi yao sijui ni jotoridi gani lilikuwa limewakumba. Kafumu jana kapigwa butwaa kuikuta bandari ipo wazi vile. Alafu wanaambiwa bado wanaleta siasa na ubabe tu, ngoja tuendelee kuhesabu tu, muda utaamua.
 
Mungu akuepushe na vitu vyenye ncha kali , amina .
 
Dua la kuku. Mnatapa tapa kutafuta makosa ya Mh. rais Dkt JPM. Tunawashauri vunjeni kambi zenu muje tushirikiane kujenga nchi. Majungu na vijembe havisaidii, maana kila mtanzania anakubali kile kinachofanywa na JPM na serikali yake.
 
Natafakari kama nilichokisikia jana ni cha mtu mwenye dhamana ya kuwaongoza watanzania kwenye njia ya utu, ucha-Mungu, upendo, kusameheana, kuunganisha nguvu ktk kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano. Mungu atusaidie tufike salama siku ya kutafakari kwa upya kumchagua Mtanzania halisi mwenye kuielewa Tanzania imetoka wapi na inapaswa iweje, iongozweje na mwenye kujivunia watanzania wote. Sielewi vijana na watoto wetu wanao mwona akisema, akiamua na kufanya afanyayo wanajifunza nini? Ee, Mungu muumba wa mbingu na nchi, badilisha moyo wa Farao ulio wa Jiwe na kumpa moyo wa nyama wenye upendo na usio na nia ya kulipa kisasi kila uchao. Ondoa giza lililotanda Tanzania. Tusamehe kwa kukosea hata pale unapotupatia nafasi ya kuwachagua wa kutuongoza. Siku zote machaguo yetu yamekuwa yakituletea majuto tu. Ee Mungu tusamehe kwa kuwa ni sisi wenyewe tumekuwa chanzo cha mateso yetu na ni sisi wenyewe tumekuwa mstari wa mbele kukuomba utuepushe na mateso hayohayo tuliyoyasababisha sisi wenyewe. Hata makuhani wetu wa kiroho wameamua kuwa upande wa mtesi wetu. Loooooooooo! Tanzania yanguuuuuuuuuu! Inayoyoma kwenye kilindi cha gizaaaaaa! Nani wa kutusaidiaaaa?
 
Dua la kuku. Mnatapa tapa kutafuta makosa ya Mh. rais Dkt JPM. Tunawashauri vunjeni kambi zenu muje tushirikiane kujenga nchi. Majungu na vijembe havisaidii, maana kila mtanzania anakubali kile kinachofanywa na JPM na serikali yake.
umekuja full doze...naamini kwa dhati ya moyo uliimisi sana forum..nitafute private nikupe dawa ya kifungo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…