Anguko la soko la dhahabu

GONZZ EPACLEM

JF-Expert Member
Dec 3, 2016
312
239
Habari wana jukwaa,

Ni mjadala huru kwa wafanya biashara wa dhahabu nchini, wakubwa kwa wadogo.

Ni kama swali hivi, kumekuwepo na kuporomoka kwa soko la dhahabu kwa kipindi cha takribani ya miezi miwili mfululizo na matumaini ya kupanda kwa dhahabu kwa mda mfupi ujao hayaonekani kiukweli, je nini chanzo cha kuporomoka namna hii kwa soko na kipi kifanyike kwa serikali kutusaidia wafanya biashara wa dhahabu kama ilivyo kwa wenzetu wa mazao ya kilimo?


Screenshot_20220917-111324_NetDania.jpg
Screenshot_20220917-111324_NetDania.jpg
 
Habari wana jukwaa,
Ni mjadala huru kwa wafanya biashara wa dhahabu nchini, wakubwa kwa wadogo.
Ni kama swali hivi, kumekuwepo na kuporomoka kwa soko la dhahabu kwa kipindi cha takribani ya miezi miwili mfululizo na matumaini ya kupanda kwa dhahabu kwa mda mfupi ujao hayaonekani kiukweli, je nini chanzo cha kuporomoka namna hii kwa soko na kipi kifanyike kwa serikali kutusaidia wafanya biashara wa dhahabu kama ilivyo kwa wenzetu wa mazao ya kilimo?View attachment 2359520View attachment 2359520
Una uelewa wowote kuhusiana na market dynamic forces & price flactuation factors ?
 
Habari wana jukwaa,
Ni mjadala huru kwa wafanya biashara wa dhahabu nchini, wakubwa kwa wadogo...
Ungetupa somo kidogo ili nasi wa hapa Parakwiyo tupate kuelewa: imeshuka kutoka wapi hadi wapi et cetera
 
Familia ya De beers ndio inamiliki biashara yote ya madini duniani wao ndio upanga na kushusha bei. Wanasema madini yote duniani bila kujali yapo nchi gani ni yao wao ndio wamiliki
 
Mambo ya economics hay...ngoja nijifunze.

#MaendeleoHayanaChama
Hakuna cha economic blhblh namba sjui magraph wanayochora

Kipindi cha kiangazi dhahabu bei huwa inashuka,maana mitosis mikubwa inazalisha dhahabu nyingi
Yaani wanafanya kazi kwa ufanisi zaidi....

Ngoja mvua zianze utaona bei ikatavyopanda
Ila pia ni nzuri bado kwa wanunuzi wa dhahabu,kikubwa ulinde mtaji

Ova
 
Ndugu, wadau, nilitoa uzi hapo juu ili kupata ufafanuzi wa kichumi zaidi, lakini bahati mbaya naona watalaamu wapo kimya tu..
Anyway, kwa kutumia knowledge yangu ya ARU pale Darusalaam main campus katika moja ya kozi niliyo kuwa nachukua, economics pia nilisoma
Mjadala ulikuwa wazi,

By reference kwa Jamaa JPM (marehemu), dhahabu ilipanda kupindukia zaidi kiasi kwamba hata sisi wafanya biashara wa chini kqbisa tulifanikiwa kupata fedha ambazo hakuna biashara nyingine una weza kuilingqnisha nq dhahabu ya Tz.
Ikumbukwe kuwa Tz ni moja ya nchi mzalishaji mkubwa wa dhahabu duniani ikiwa na caratage ya daraja la juu sana, yaani (24k, 23k, 22k, na rarely 21k), hivyo Tz ni moja ya supplier mkubwa wa dhahabu duniani ikitanguliwa na nchi za DRC, South Africa kwa bara la Africa.
Sasa tukirejea enzi za utawala wa Magufuli kulitokea mgogoro uliosanuliwa na Mwamba mmoja anaitwa TAL, baada ya late presidaa Magufuli kuingilia kati harakati za madini na wawekezaji wa Madini (BARICK, GGM n.k) ambapo TAL aligeuka kuwa wakili wa hawa mabepari kutetea maslahi yao kisheria kama nguli wa Sheria Tz.
Mgogoro huu uliitwa usafirishaji wa makinikia ambapo ilibainika haukuwa mchanga mtupu bali na madini ndani yake.
TAL alidai na kuiambia serikali ya Magufuli endapo itaingilia mikataba walio ifunga ba kusaini kwa mikataba ya madini duniani, serikali ingeweza kushtakiwa MIGA kwa kuvunja mkataba kinyume cha makubaliano.
Magufuli alikaza kamba kana kwamba hakujali kabisa madhara yoyote ambayo yangeweza kutokea endapo angefeli mkakati wake kuizuia dhahabu isiendelee kuchukuliwa na mabepari haya.
Tulishuhudia sote dege la binafsi (private jet) la boss wa BARRICK bwana Tomson likitua pale JNIA kumfata mwamba wayamalize( dah! Alikuwa mwamba kweli na chuma wa misimamo kama talbani hivi)
Ikumbukwe kuwa kipindi hicho chote cha mgogoro, migodi kama ya BULYANHULU kahama, North Mara musoma ilisimama ualishaji hivyo kuathiri upatikanaji wa dhahabu ya Tz kwenye soko la Mabepari.
Kukosekana kwa dhahabu hii soko la dunia kuliifanya bei kupanda sana kwa sababu ilikuwa adimu tena sokoni, matajiri wakawa wanaipandilia bei ili angalau waipate hata magendo tu, maana haikuwa nyingi sojoni
Hivyo wachumi waka sema kuwa
Ikiwa upatikanaji wa bidhaa ukiwa mdogo mara nyingi uhitaji wa bidhaa hiyo kwa watu huwa mkubwa, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa bei yake sokoni yaani ( THE LOW THE SUPPLY~THE HIGH THE DEMAND=THE HIGH THE PRICE) vile vile, ikiwa upatikanaji wa bidhaa ni mkubwa mara nyingi uhitaji wa bidhaa hiyo huwa mdogo, ikiwa ni pamoja na kushuka kwa bei yake (THE HIGH THE SUPPLY THE LOW THE DEMAND=THE LOW THE PRICE)
Sasa kwa wale tunao ishi katika maeneo ya uwekezaji wa dhahabu yaani Bulyanhulu na North Mara kwa mfano, tunaweza kuwa mashuhuda kuwa, kipindi cha Mwamba, ndege za kubeba mizigo ya dhahabu kutoka ubeparini zilipungua sana kupelekea hata viwanja vyao vya kutua kuota majani kutokana na kutokutumika kwa mda mrefu bila ndege kutua viwanjani humo,
Baada ya mwamba kufariki na usukani kupokelewa na MGAWA ASALI,, viwanja hivi vilifufuliwa kwa kasi sana ikiwa ni pamoja na kufyekwa majani na ukarabati mwingine wa kimiundo mbinu ili kurahisisha utuaji wa ndege hizi kubeba matofali ya dhahabu kutoka Tz nchi ya WAGAWA ASALI.
Binafsi nakaa kakola ambako BARICK amewekeza, ndege nadhani inatua mara mbili ama mara tatu kwa wiki ikipakia matofali ya dhahabu kwenda ulaya na nabaki nakodoa tu macho juu huku ikienda kweli dah!
Hivyo upatikanaji wa dhahabu ya Tz kwenye soko la dunia ni nyingi sana kwa sasa ukilinganisha na kipindi cha Hayati Magufuli, na kuporomoka kwa bei tusishangae sana.
Nawasilisha...
By Epafra Clement, Jobless choka mbaya sana kutoka mitaa ya Bulyanhulu kakola
 
Back
Top Bottom