Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,655
- 729,717
Nazizungumzia Uganda Burundi na Rwand.
Kwanza ni nchi zenye muingiliano wa mengi yanayojulikana na mengi pia yaliyojificha.
Lakini kitakachoziangusha ni u binafsi uroho wa madaraka visasi na hofu ya watawala wa sasa.
Tumeona kilichotokea Uganda kwenye uchaguzi mkuu uliomalizika tumeona ya Burundi, Rwanda bado hali si mbaya sana.
Zimbabwe ya miaka ya 90 ilikuwa inakimbiza kiuchumi, sarafu yao ya Zimdollar ilikuwa na thamani kubwa uroho huu wa madaraka umeifanya Zimbabwe ifike ilipofikia sasa.
Nchi nilizotaja ni wanachama ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki, kuna tatizo kubwa sana tunalifuga hapa mana naona hakuna kuambizana ukweli wala kukemean.
Museveni kashinda kwa hila za wazi kabisa kama ilivyokuwa hapa kwetu, lakini sikuona ndani ya jumuiya akikemewa na yeyote.
Mbaya zaidi tumeikaribisha Sudan kusini kwenye huu umoja, matatizo ya Sudan kusini yanaeleweka yanafanana kwa kiasi kikubwa na nchi nilizotaja
Kuwa na washirika wa namna hii ndani ya jumuiya sidhani kama ni jambo lenye afya sana.
Tuwe makini tusije kupumbazwa na umoja wenye maslahi binafsi toka kwa viongozi wetu.
Ni Kenya pekee ndio wanaweza kusimama kifua mbele na kujivunia demokrasia na usawa ni wao tu ambao chama kilichopo madarakani ni chama cha upinzani, kwengine kote upinzani unaminywa kwa nguvu ya ajabu na ukatili mkubwa mno.
Anguko lolote kwenye hizo nchi litakuwa na athari za moja kwa moja ndani ya jumuiya
TUJITAFAKARI