TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,561
- 28,558
This is a very interesting thread!
na wewe utakuwa na pii echii dii ya korosho.Swali zuri kama hizo trilioni tano zilizoko BOT hazitoshi....itakopa kwenye mabenki kama mkopaji mwingine...lakini sio kukopa pesa zake mwenyewe.....itakopa pesa za mabenki
Kuna siku nilimsikia Dr. Charles Kimei akisema uamuzi wa serikali kutunza fedha Bank Kuu hautaathiri commercial banks!Basi nimekufananisha maana ID hii tumewahi jadili nayo mambo haya kwa kina sana!!
Anyway uchumi wetu unayumba kutokana na govt kupunguza sana matumizi coz chumi changa kama zetu zinahitaji sana kuwa boosted na govt expenditure kama serikali haitumii basi mzunguko unadorora na kuziathiri pia benki...
Nimemsikia Magufuli akijisifu kuwapa kazi nyingi TBA za serikali hii pia inaua uchumi coz TBA ni serikali so serikali inazungusha pesa mfukoni kwake badala ya kuwapa kazi makampuni watakaolipa kodi na kuajiri vijana wengi zaidi!
Hii ya CRDB kutoka kupata faida ya 30 billion mpaka hasara ya 2 billion ni msiba!! Hii si figisu ni kitu dhahiri kwani benki zote transactions zake pamoja na mitiririko yote ya fedha zao zipo monitored na BoT ni vigumu kudanganya!!
Jambo lingine lilichangia kuanguka huku ni hofu za wateja dhidi ya serikali!! Serikali ya JPM imeonesha dhahiri kutotabirika!! Hakuna mwekezaji au tajiri yeyote anayeweza wekeza pesa zake kusikotabirika!! So wengi waliondoa fedha zao benki ili kuondokana na hofu dhidi ya serikali isiyotabirika so benki zinakosa amana na mitaji....
Kingine ni madeni yasiyolipika kama vile mikopo ya watumishi hewa.... madeni ya biashara zilizoanguka kama hoteli n.k n.k
Katika ishu JPM anahitaji kuwa serious ni uchumi!! Hayo mengine anayohangaika nayo yatampotezea muda tu huku nchi ikielekea ilipo Zimbabwe... ni suala la muda tu utatuambia!!
CC Kobello Pohamba Richard
safi sana mkuu....Kwa uamuzi wa sasa, serikali inajipa hasara yenyewe maana mabenki yasipoweza kufanya kazi, uchumi utasinyaa, mapato ya serikali nayo yatasinyaa. Kwanza hiyo pesa ya serikali siyo yake, ni ya kwetu sisi walipa kodi. Kama wanaolipa kodi ndiyo hao hao wanaoitumia, kuna ubaya gani? Nadhani kulikuwa na njia bora zaidi ambayo serikali ingeweza kufanya kuliko uamuzi wa ghafla ambao mwishowe utawaathiri wananchi na serikali yenyewe.
Pesa zilizokuwa za mashirika mf..TANAPA, Ewura, Tanroads, ni pesa za nani?Hivi kweli wewe una akili? Serikali inawezaje kukopa pesa zake yenyewe tena kwa riba? Kila mnachoambiwa mnadaka tu kama makinda ya ndege yanavyoletewa wadudu mama zao na kupanua midomo yao na kumeza? Huwezi hata kujiuliza? Pesa yako mwenyewe halafu ukopeshwe? Ni aibu kuamini uongo wa namna hii!
acheni kufikiri kilayman, kwani hao wahindi si watanzania???, selikari ya chama chenu si ndo inawapa uraia??Wanaokopa na kupewa pesa ni wahindi sio hawa makabwela. Muhindi akienda benki anachukua pesa anayotaka kumbe ni pesa ya serikali. Waache waisome no, wanyonge wakienda kukopa benki usumbufu wake unakua mkubwa sana.
Mabenki hayakuanzishwa ili yafanye biashara na serikali, yalianzishwa ili yafanye biashara na wananchi....wauze share kwa wananchi ...halafu watuambie zile share za watu zimekwenda wapiKwa uamuzi wa sasa, serikali inajipa hasara yenyewe maana mabenki yasipoweza kufanya kazi, uchumi utasinyaa, mapato ya serikali nayo yatasinyaa. Kwanza hiyo pesa ya serikali siyo yake, ni ya kwetu sisi walipa kodi. Kama wanaolipa kodi ndiyo hao hao wanaoitumia, kuna ubaya gani? Nadhani kulikuwa na njia bora zaidi ambayo serikali ingeweza kufanya kuliko uamuzi wa ghafla ambao mwishowe utawaathiri wananchi na serikali yenyewe.
Hizo taasisi za serikali zilianzishwa na nani? Wakurugenzi wake wanateuliwa na nani? Kama ni independent mbona kila siku wanatumbuliwa? Huwezi tofautisha serikali na taasisi zake hata siku moja.na wewe utakuwa na pii echii dii ya korosho.
tofautisha serikali na taasisi za serikali.
kuna baadhi ya taasisi za umma,kwa mujibu wa sheria ambazo inaziunda, ni entity ambazo zinajitegemea,independent,zina uwezo wa kuwa na akaunti zake.
pia kuna serikali yenyewe,hii inayokusanya kodi za mawese,kodi za mkaa,hii ndio inatakiwa iwe na akaunti benki kuu na ihifadhi pesa zake huko
Hahahahaaaaaaah! Watakufa wengiiMabenki hayakuanzishwa ili yafanye biashara na serikali, yalianzishwa ili yafanye biashara na wananchi....wauze share kwa wananchi ...halafu watuambie zile share za watu zimekwenda wapi
serikali ilikopa fedha katika mashirika ya pensheni ili ijenge UDOM,Pesa zilizokuwa za mashirika mf..TANAPA, Ewura, Tanroads, ni pesa za nani?
Duh! We jamaa hamna kitu kabisa? Ina maana hadi leo hujawahi kusikia kwamba serikali inadaiwa kiasi hiki au kile na mifuko ya hifadhi ya jamii? Unahitaji kukumbushwa kwamba majengo yote ya serikali including UDOM na nyumba za Polisi pale Kilwa Road ni mkopo wa mifuko ya hifadhi ya kijamii kwa serikali? Unahitaji kukumbushwa kwamba pale Machinga Complex ambayo ilijengwa na NSSF, riba inazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka kwavile serikali haijanza kulipa? Kama serikali haiwezi kukopa kwa riba; sasa kwanini gharama ya mkopo inapanda mwaka hadi mwaka?Hizo taasisi za serikali zilianzishwa na mitaji kutoka wapi? Yaani serikali itoe mitaji yake kuanzisha taasisi halafu pesa za taasisi hizo useme sio zake...TANESCO kila mwaka inaendeshwa kwa hasara, ni nani anaeibeba Tanesco? Kama sio serikali kutoa ruzuku unafikiri Tanesco ingekuwepo sasa hizi? Kwa hiyo Tanesco ikipata hasara serikali iwasaidie, lakini pesa zake isiziguse haziwahusu sio? Are you crazy?
Kajole hujaona hasara ya serikali kwenda kuficha hela BOT? yaani mfano unaduka unatoa hela kwenye mzunguko unaenda kuzichimbia chini ya ardhi kwamba zisliwe na mchwa. BOT hawafanyi biashara yoyote mkuu kwa hyo serikali imetoa hela nyingi kwenye mzunguko. Hapa ndipo tunapo toka kuishi kama malaika na kwenda kuishi kama mashetaniSerikali kutunza fedha zake BOT ni sahihi kabisa maana one and traditional function of BOT is a " banker of the Government". hapa kuna tatizo kwny hzi commercial banks zetu.
Tofautisha kati ya CRDB GROUP na CRDB BANK .... Wee jamaa yaani (God forbid)Statement ndivyo zinavyoonesha lakini the problem ni kwamba, Deposit ya 2 Billion si lolote mbele ya Loss (Profit)ya 2 Billion kwa sababu, endapo tuta-assume ni loss incurred from loan default basi tungesema hiyo 2 billion ni roughly 20% of total loan default.
But all in all, inaonekana hali si nzuri manake hata ukipitia indicator moja moja, nyingi performance yake imeshuka! Hata number of employees nayo imee-drop kutoka 2809 hadi 2449! Tunajua hawajapunguza wafanyakazi lakini inaonesha hakuna replacement kwa wanaostaafu au kuacha kazi!
Ningelijua ningelianza kutiririka, ila juzi member humu walisema Tanzania huenda ikaingia kwenye recession, kama sio depression kabisa.Wewe hujui?
umenikumbusha ile hadithi ya kwenye biblia....wale vijana waliopewa talanta,mmoja aliichimbia chini,mwenzie akaenda kuizalisha.Kajole hujaona hasara ya serikali kwenda kuficha hela BOT? yaani mfano unaduka unatoa hela kwenye mzunguko unaenda kuzichimbia chini ya ardhi kwamba zisliwe na mchwa. BOT hawafanyi biashara yoyote mkuu kwa hyo serikali imetoa hela nyingi kwenye mzunguko. Hapa ndipo tunapo toka kuishi kama malaika na kwenda kuishi kama mashetani
Ulivyo sema wewe, kama serikali ingepima madhara yake kabla ya maamuzi ....ni sawa kama unaendesha serikali kibinadamu. Lakini serikali haiwndeshwi kindugu au kibinadamu, serikali imsendeshwa kisheria. Hakuna nchi yoyote duniani inaweza kuruhusu mabenki ya kibiashara kuendeshwa kwa mtaji wa bure. Moja kati ya biashara ya benki ni kukopa na kukopesha. Nikupe Mfano mdogo, ungekuwa na kuku wa mayai, ukagunduwa jirani yako anakuibia mayai yako, ungempa muda wa kuendelea kukuibia kwasababu anawatoto wa kuwalisha na utamdhuru maisha yake? Au ungepigilia miumari haraka sana kuzuia asije tena kwenye banda lako? Sasa kitendawili hicho ndicho kilikwa huko kwenye mabenki. Na JPM hakuweza kuvumikia hata dakika nyingine moja wakati wanahisa wa mabenki wanalamba faida ya bure.Hata kama ilikuwa hivyo au inavyotakiwa. Utawala wowote wenye weledi hauwezi kuchukua uamuzi wa ghafla bila ya kupima madhara yake. Huzitazami benki unapofanya maamuzi, unaitazama nchi.