Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Anguko la Mabenki nchini? CRDB yapata hasara ya Sh. Bilioni 2

Tunajenga Tanzania moja lakini serikali inagombania fito,eti inasema benki zilikuwa zinatumia fedha za serikali kukopesha wananchi na kupata faida.

Ebbo!!, sasa na bakhresa,mengi,mohamed dewji na matajiri wengine wanaoweka fedha benki nao wazitoe kwa hoja kwamba benki huwa wanatumia hela zao kukopesha?

je wakishakopesha, serikali ikienda kuangalia balansi,au ikienda kuzichukua huwa inaambiwa "fedha zenu hazipo,tumezikopesha"....si huwa wanazikuta!!tena zikiwa na riba!!

je wanaokopa ni akina nani? si hawa akina hawa,asha,mwajuma,abdallah,masanja.....watanzania wenzetu ili wakaanzishe biashara zao ndogo ndogo wajikomboe na umasikini!,

sasa serikali imeona hawa watanzania.wanakopa fedha benki wanazifaidi(na inaamini eti zinazokopwa ni za serikali tu),ikaamua izitoe,sasa inamkomoa nani? inazikomoa benki au wafanyabiashara wadogo na wa kati ambao sasa hawapati mikopo na wanalia hali ngumu!

halafu unapokusanya pesa na kwenda "kuzificha" benki kuu unazuia mzunguko,benki kuu itayahifadhi malundo kwa malundo ya pesa tu,haiwezi kwenda tandale kumkopesha mama ntilie,haiwezi kwenda mtaa wa kongo kumkopesha mjasiliamali,

kwa maana nyingine,"unakomba"hela zoote za nchi,"unazificha,halafu unataka watu wafanyeje? manake huku ni kuficha hela.

kingine,hiyo CRDB ni benki ya nani?si ni benki ya mtanzania? kama kwa.miaka zaidi ya 20wameonyesha uaminifu kwa kutopoteza hata senti ya umma iliyohifadhiwa pale,kwa nini wewe ukae mwezi tu serikalini eti uwazidi akili mwinyi,mkapa na kikwete!!

tunagombania fito,na kwa kuwa tunagombania fito,hakika nyumba haitaisha,ukishika fito unanyanganywa,na mimk ukishika fito nakunyanganya......tutagombana weee mwishowe akija aliyetupa kazi (mtanzania)kutaka akabidhiwe nyumba,tutakoma 2020

Wanaokopa na kupewa pesa ni wahindi sio hawa makabwela. Muhindi akienda benki anachukua pesa anayotaka kumbe ni pesa ya serikali. Waache waisome no, wanyonge wakienda kukopa benki usumbufu wake unakua mkubwa sana.
 
Hapa kazi tu! Jamaa anahifadhi fedha za taasisi zake za serikali Benki Kuu ambayo kimsingi haifanyi biashara ya fedha Bali kusimamia monetary policy. Matokeo yake money circulation nchini imedorora, na commercial banks zinalazima kukopa Benki Kuu. Hii imesababisha interest rates against loans kupanda sana. Wakopaji wanashindwa kukopa, hivyo investments nazo kudorora. Kwa mwenendo huu kwa nini nchi isiingie kwenye recession! Tuendelee kuimba " Hapa kazi tu" kiushabiki lakini kwa bahati mbaya uchumi haujui "ushabiki"
Nimeipenda sentensi yako ya mwisho "uchumi haujui ushabiki" niongezee uchumi hauna itikadi.
 
inazichukua tu eti eehh!!

kuna pesa nyingi za mashirika ya pensheni,ikitaka inazichukua tu eti? halafu wastaafu watalipwa na wajomba zako
kuna pesa za tanesco,ikitaka inazichukua tu eti eeh halafu tutatumia gesi ya tumboni kwako eehh
Inazichukua sababu ni zake.. ..Mitambo ya Tanesco ilinunuliwa na pesa za nani?
 
Serikali yoyote ambayo inaondoa 5 Trilioni shilings kwenye mzunguko wa pesa nchini ni kuziweka idle ni Serikali isiyojitambua na haistahili kuwepo madarakani. Benefits za 5 Trilioni shillings kuwa kwenye mzunguko wa pesa ni kubwa mno ukilinganisha na hasara kubwa ya kuziondoa pesa hizo na kuziweka idle
Huelewi unaleta ubishi wa kitoto bila kuelewa hata chembe ya mambo ya uchumi.

Hizo bilioni tano zimekaa idle karibu mwaka sasa zingekuwa zinazunguka nchini si ajabu Srikali ingekuwa imeshapata faida ya hata nusu Trilioni hata zaidi.

Hizo trilioni tano sasa ziko BOT serikali ikizitaka itaenda kuzichukua bila kutoa riba....Unataka zipelekwe CRDB halafu wakazikope kwa riba kubwa? Kuna mabenki mengi serikali haikuwa inaweka pesa zake huko yako vizuri yanaendelea kufanya biashara halali na wananchi.....CRDB kuna shareholders wameweka fedha zao huko nashangaa wanalilia pesa za serikali.....hii benki ilikuwa inaendeshwa kijanja janja wacha ife
 
inazichukua tu eti eehh!!

kuna pesa nyingi za mashirika ya pensheni,ikitaka inazichukua tu eti? halafu wastaafu watalipwa na wajomba zako
kuna pesa za tanesco,ikitaka inazichukua tu eti eeh halafu tutatumia gesi ya tumboni kwako eehh
Hizo pesa za pensheni serikali imeshazichukua inajengea viwanda....Waambie wakurugenzi wazizuie basi uone kitakachowatokea.
 
Mkuu Lusungo, serikali nayo fedha na kuanzia mwakani itaiambia BOT iingize fedha kwenye mzunguko.

Lakini ni lazima serikali ibane matumizi ili kuwe na uwiano na mapato na matumizi.

Hili la hizi benki tumelijadili sana hapa JF na sasa umefika wakati wake kwamba ni zile benki halisi ndizo zitaweza kusalimika lakini zile za binafsi haziwezi kusalimika kwani pia zilikuwa zikitumika kutorosha fedha nje ya nchi na ufisadi mwingine.

Kuhusu watu kuficha fedha kwa hofu ya serikali hii kutotabirika hio nadhani ni hofu tu ila wapo watu ambao walitorosha fedha kwa kuhofia kuulizwa wamezipataje.

Ila bado wapo wafanyabiashara wanafedha zao kwenye mabenki na wanaendela na shughuli zao kama kawaida.

Lakini serikali ikianza kuongeza fedha kwenye mzunguko baada ya mipango yake yote kukamilika ambayo inafanya sasa hivi na BOT, basi hali itakuwa shwari.

Mkuu, mambo ambayo yalikuwa yakitendeka hapa nchini ni mambo ya hatari sana kuhusu uchumi wetu yaani haukuwa uchumi wa Tanzania, ulikuwa ni uchumi wa kigeni ulotawaliwa na dola na shilingi yetu ilifika hadi tshs 3800 kwa UGP 1! Yaani ilikuwa ikielekea Tshs 4,000!

Sasa hivi utashangaa ukiingia Azania Bancorp unaona tellers wako na kazi zingine lakini BOT staff wapo nyuma ya counters wanashughulikia masuala muhimu.
Kuna wakati kuishi kwa matumaini ni jambo jema maana hupunguza msongo wa mawazo. Nothing is on the ground to guarentee good economy for Tanzania in the near future.
 
Hizo trilioni tano sasa ziko BOT serikali ikizitaka itaenda kuzichukua bila kutoa riba....Unataka zipelekwe CRDB halafu wakazikope kwa riba kubwa? Kuna mabenki mengi serikali haikuwa inaweka pesa zake huko yako vizuri yanaendelea kufanya biashara halali na wananchi.....CRDB kuna shareholders wameweka fedha zao huko nashangaa wanalilia pesa za serikali.....hii benki ilikuwa inaendeshwa kijanja janja wacha ife
Usijitoe akili wewe...yaani unatangaza kumuunga mkono JPM ili upate nafasi ya kuongea utumbo?

Unapoambiwa zamani serikali pesa zake zilikuwa kwenye mabenki ya biashara; majority ni pesa za taasisi zake kv NSSF, PPF, TPA, and the like! There's no way serikali inaweza kuzichukua hizo pesa kadri watakavyo... NO WAY! Zile za TRA ambazo serikali ndio hasa inaweza kutamba nazo, zilikuwa zinakaa kwenye mabenki kwa muda mfupi... selected branches zinakuwa na TRA Collection & Revenue Accounts ambazo zinakuwa transferred biweekly to HQ of a particular bank na HQ wana-transfer to Treasury... haziwezi kukaa kwenye mabenki zile wakati serikali yenyewe inazihitaji mapema iwezekanavyo kwa ajili ya matumizi yake!

Pesa nyingine ambayo ni ile ambayo tayari imeshaingia kwenye bajeti ya matumizi... kwamba, Quarter X, kila halmashauri inapata kiasi fulani cha fedha a Road Fund na hizi zinakuwa kwenye commercial banks. Sasa pesa kama hii hata kama itabaki Hazina still serikali haiwezi kuichukua kama ipendavyo kv tayari itakuwa kwa ajili ya Halmashauri X!
 
Serikali yoyote ambayo inaondoa 5 Trilioni shilings kwenye mzunguko wa pesa nchini ni kuziweka idle ni Serikali isiyojitambua na haistahili kuwepo madarakani. Benefits za 5 Trilioni shillings kuwa kwenye mzunguko wa pesa ni kubwa mno ukilinganisha na hasara kubwa ya kuziondoa pesa hizo na kuziweka idle
Huelewi unaleta ubishi wa kitoto bila kuelewa hata chembe ya mambo ya uchumi.

Hizo bilioni tano zimekaa idle karibu mwaka sasa zingekuwa zinazunguka nchini si ajabu Srikali ingekuwa imeshapata faida ya hata nusu Trilioni hata zaidi.
Nani kakuambia ziko idle huko BOT? Serikali inazitumia kwenye miradi ya maendeleo na kulipa mishahara ya watumishi....kwa hiyo zinarudi kwenye mzunguko bila serikali kwenda CRDB kuzikopa kwa riba....hakuna pesa inayokaa idle, juzi serikali wamepunguza deni la Taifa unafikiri hizo pesa wamezitoa mbinguni?
 
Kama wamepata hasara wanawaambia share holders hiyo hasara imetokana na nini? Bank zote zilikuwa zinafanya biashara na pesa za watu (mashirika ya umma nk.) Wacha waisome number wafanye shughuli za ki-bank sio kukaa na kungoja baraka ya kuwaibia walipa kodi. They need to change how they operate.
wewe serikali inashare kubwa CRDB, bank ikipata kupata hasara maana yake selikari itakosa gawio (dividend) na corporate tax , hivyo kupunguza mapato ya selikari kwenye kodi na yasizo ya kodi,

hii kazi mliyopewa kuitetea selikari ni ngumu
 
Nani kakuambia ziko idle huko BOT? Serikali inazitumia kwenye miradi ya maendeleo na kulipa mishahara ya watumishi....kwa hiyo zinarudi kwenye mzunguko bila serikali kwenda CRDB kuzikopa kwa riba....hakuna pesa inayokaa idle, juzi serikali wamepunguza deni la Taifa unafikiri hizo pesa wamezitoa mbinguni?
kama serikali imefanya hivyo kuondoa pesa zake katika mabenki ili isikope kwenye mabenki kwa riba

mbona bajeti inaeleza kwamba serikali itakopa kutoka mabenki ya ndani na nje kiasi cha zaidi ya trilioni saba?

ni wazi kwamba bajeti haijitoshelezi,hakuna jinsi utaacha kwenda kukopa
 
Wengi hapa manatarifa zisizo sahihi, siku zote katika nchi, mabenki ya kibiashara yanafanya kazi na serikali ili kuendeleza uchumi. Benki ya biashara haichapishi hela, inategemea hela toka benki kuu ya nchi kwa njia ya mkopo au ununuzi bond za serikali. Benki ya biashara hukopa kutoka benki kuu, kwa njia ya riba ya chini, na intumia fedha hiyo kukopesha watu wa kawaida, wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo, bila kusahau makampuni pia. Mikopo hiyo inawekewa riba ilio juu kuliko ile ikiyo kopea benki kuu. Sisi tukilipa mokopo yetu, benki inakata cha juu na kurudisha ilichokopa benki kuu kama ilivyo kubaliana awali.

Sasa serikali nilivyo ondoa fedha zake za makusanyo na matumizi kutoka benki za biashara haikutakiwa kuathiri uwezo wa benki ya biashara kujiendesha kwasababi benki ya biashara bado inauwezo wa kukopa kutoka benki kuu na kutumia hiyo hela kuisambaza kwa wafanyabiashara ili na wao waweze kuendeza uchumi. Benki za biashara zililemaa na pesa rahisi ya serikali maana hawailipi riba, na wanaweza kutumia hela hiyo hiyo ya serikali kuwakopesha watu wengine tena kwa riba ile ile ya juu. Lakini mabenki yamekutwa katika wakati mgumu kwasababu hawakutarajia kama serikali itakata mrija wa fedha zake kwenye mabenki ya binafsi. Mabenki mengine hata mitaji yao ilikuwa imeswekwa kwenye biashara nyingine, na sio rahisi kurudisha hiyo hela haraka bila hayo mabenki kupoteza hela au kupata hasara.

Ni wakati wa mabenki kuwa wabunifu na kuja na product zingine ambazo zitavutia wateja kuingia kwenye milango yao ya benki na kufanya biashara kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Hata kama ilikuwa hivyo au inavyotakiwa. Utawala wowote wenye weledi hauwezi kuchukua uamuzi wa ghafla bila ya kupima madhara yake. Huzitazami benki unapofanya maamuzi, unaitazama nchi.
 
Usijitoe akili wewe...yaani unatangaza kumuunga mkono JPM ili upate nafasi ya kuongea utumbo?

Unapoambiwa zamani serikali pesa zake zilikuwa kwenye mabenki ya biashara; majority ni pesa za taasisi zake kv NSSF, PPF, TPA, and the like! There's no way serikali inaweza kuzichukua hizo pesa kadri watakavyo... NO WAY! Zile za TRA ambazo serikali ndio hasa inaweza kutamba nazo, zilikuwa zinakaa kwenye mabenki kwa muda mfupi... selected branches zinakuwa na TRA Collection & Revenue Accounts ambazo zinakuwa transferred biweekly to HQ of a particular bank na HQ wana-transfer to Treasury... haziwezi kukaa kwenye mabenki zile wakati serikali yenyewe inazihitaji mapema iwezekanavyo kwa ajili ya matumizi yake!

Pesa nyingine ambayo ni ile ambayo tayari imeshaingia kwenye bajeti ya matumizi... kwamba, Quarter X, kila halmashauri inapata kiasi fulani cha fedha a Road Fund na hizi zinakuwa kwenye commercial banks. Sasa pesa kama hii hata kama itabaki Hazina still serikali haiwezi kuichukua kama ipendavyo kv tayari itakuwa kwa ajili ya Halmashauri X!
Hizo taasisi za serikali zilianzishwa na mitaji kutoka wapi? Yaani serikali itoe mitaji yake kuanzisha taasisi halafu pesa za taasisi hizo useme sio zake...TANESCO kila mwaka inaendeshwa kwa hasara, ni nani anaeibeba Tanesco? Kama sio serikali kutoa ruzuku unafikiri Tanesco ingekuwepo sasa hizi? Kwa hiyo Tanesco ikipata hasara serikali iwasaidie, lakini pesa zake isiziguse haziwahusu sio? Are you crazy?
 
Kumbe rais alikuwa sahihi aliposema kuwa wakati serikali inahangaika kukopa ili kupata fedha za maendekeo kutoka mabenki, mabenki hayo hayo yanatumia fesha hizohizo za serikali kuikopesha serikali. Kwa maana kuwa serikali inakopa fedha zake yenyewe.
Hata wewe kama ni mteja wa benki, siku ukikopa, unakopa hela yako mwenyewe na za ndugu zako na marafiki zako ambao wameweka fedha zao benki.
 
kama serikali imefanya hivyo kuondoa pesa zake katika mabenki ili isikope kwenye mabenki kwa riba

mbona bajeti inaeleza kwamba serikali itakopa kutoka mabenki ya ndani na nje kiasi cha zaidi ya trilioni saba?

ni wazi kwamba bajeti haijitoshelezi,hakuna jinsi utaacha kwenda kukopa
Swali zuri kama hizo trilioni tano zilizoko BOT hazitoshi....itakopa kwenye mabenki kama mkopaji mwingine...lakini sio kukopa pesa zake mwenyewe.....itakopa pesa za mabenki
 
Serikali ilikiwa inafaidikaje na pesa zake huko kwenye mabenki? We umeambiwa serikali ilikuwa inakopa pesa zake kwa riba kubwa huko kwenye mabenki...sasa hivi pesa za serikali ziko BOT ikizitaka hakuna cha kukopa kwa riba
Hivi kweli wewe una akili? Serikali inawezaje kukopa pesa zake yenyewe tena kwa riba? Kila mnachoambiwa mnadaka tu kama makinda ya ndege yanavyoletewa wadudu mama zao na kupanua midomo yao na kumeza? Huwezi hata kujiuliza? Pesa yako mwenyewe halafu ukopeshwe? Ni aibu kuamini uongo wa namna hii!
 
Kumbe rais alikuwa sahihi aliposema kuwa wakati serikali inahangaika kukopa ili kupata fedha za maendekeo kutoka mabenki, mabenki hayo hayo yanatumia fesha hizohizo za serikali kuikopesha serikali. Kwa maana kuwa serikali inakopa fedha zake yenyewe.
Kwa uamuzi wa sasa, serikali inajipa hasara yenyewe maana mabenki yasipoweza kufanya kazi, uchumi utasinyaa, mapato ya serikali nayo yatasinyaa. Kwanza hiyo pesa ya serikali siyo yake, ni ya kwetu sisi walipa kodi. Kama wanaolipa kodi ndiyo hao hao wanaoitumia, kuna ubaya gani? Nadhani kulikuwa na njia bora zaidi ambayo serikali ingeweza kufanya kuliko uamuzi wa ghafla ambao mwishowe utawaathiri wananchi na serikali yenyewe.
 
Bank kubwa Tanzania CRDB bank imepata hasara ya Sh Billion 2 katika hesabu zake za robo mwaka (Quarterly Financial Statements) Suala limenistua sana baada ya kuona Twiga Bancorc ilikua insolvent/ ilifilisika hivi karibuni.

Wajuzi wa mambo naomba mtujuze hii private bank (CRDB) wame conceal profit to avoid Tax liability au kweli wame incur loss naomba TRA walifatilie hili huenda CRDB wame conceal profit for the quarter

Taarifa za fedha zinaonesha kuwa mikopo mingi haijalipwa (underperforming Loans) lakini pia CRDB walikua wana accumulated tax/deni la kodi la muda mrefu.

Mwaka 2015 in 3rd quarter kama hii walipata faida ya Sh. 37.9 Billion after statutory deduction/Tax

Banking and Financial Institution
Act ya (2006) Section 32(3) inazitaka Taasisi hizo kuandaa taarifa za fedha.

Waliosoma Uhasibu kidogo mnaweza mkapitia Financial Statements (Balance sheet na Statement of Income Statement)

Operating costs:
1.salaries and benefits
2. Fees and commissions
3. Other operating costs.
Total almost 30bn more than same period last year.
 
Back
Top Bottom