Mjenda Chilo
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 1,473
- 529
Kula tano
Hivi huyo Lowassa ndo amekufanya umekuwa zuzu huku ukijiita ni msomi? Yani ulitaka magufuli aache kushughulikia uozo uliopo hapa nchini aanze kucheka cheka na watendaji huku akiahidi ajira? Hiyo ahadi ya kuongeza ajira ni mpya?
Mkuu penda kiasi, usipende sana wala kuchukia sana! Najua huipendi ccm na hivyo hata Magufuli afanyaje hutapenda. Cha kufanya wew tulia tu kwanza kwa sasa, muaache Rais afanye kazi yake, huyo Lowasa bado ana nafasi 2020
Wadau Salaam na Heri ya x~mass na mwaka mpya!
Elimu na maarifa yanapatikana sehemu mbalimbali na kwa namna mbalimbali kama hauchoki kujifunza.
Kabla ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi sijawahi kudhani kama Magufuli anafaa kwa nafasi ya urais.
Lakini kwa sasa ndio anakalia kiti na demokrasia inatufundisha kuvumiliana bila kujali kama amekuwa rais kidemokrasia.
Kuna watu wamepongeza utendaji wake wa mwanzo wa kunyooshea vidole na kushusha lawama kwa watendaji wa serikali.
Kweli ameanza kwa makeke kama Mohamed Morsi kukata tawi alilokalia.
Ametumia nguvu kubwa kutuaminisha kuwa anafanya maamuzi kwa umakini mkubwa japo ukiangalia uteuzi wa kina Nape na Makamba unapata vipele vya baridi.
Anyway tusimnange sana kwa sasa ila tujaribu kutoa mtizamo wetu.
Jose Mourinho kocha gwiji kabisa wa Chelsea amepigwa chini.
Ni ajabu kuona mtaalamu huyu wa mpira mwenye vifaa vyote akishindwa kufanya kazi.Hakuwa na upungufu wa chochote kuanzia CV,wachezaji, fedha, mamlaka na support ya mashabiki lakini kazi ikashindikana.
Haijalishi uzuri wa mkakati wako kiuongozi lakini kama watu unaofanya nao kazi hawako nyuma yako basi hauwezi kufanikiwa.Mapungufu ya Mourinho yameonyesha umuhimu wa kuwaamini watendaji na kuwajengea kujiamini badala ya kuwatisha na kuwalaumu.
Kwa muda unaweza kuhamisha lawama za kushindwa kwako kuwasimamia watu kwa kuwaondoa kwa kisingizio cha mapungufu yao lakini baadae ukweli utabaki palepale na kushindwa kwako kutakua wazi.
Mourinho aliwatoa kina Lukaku, Andre Schurrle,Kevin de Bruyne na wengine wengi ila wakaenda kung'aa walikoenda na kina Costa,Fabregas,Willian wakaonekana kama kundi la watalii uwanjani.
Magufuli anapaswa kujua uongozi wa kileo ni mkakati pamoja na motivation.Uongozi wa kuamrisha na kutishia una nafasi kidogo sana ya mafanikio, tena ya muda mfupi.
Ni uongozi unaofaa zaidi jeshini wakati wa matatizo na hata hivyo majeshi mengi ya kisasa yameamua kuachana nao baada ya kuona ufinyu wa tija yake.
Mategemeo ya watanzania ni mengi kwa kadiri yalivyo matatizo yao.Ulaghai wa kufukuza, kusimamisha, kufungiana mageti,kuweka lock~up utadumu kwa muda tu.Kama suluhu za matatizo ya watanzania hazitapatikana ni dhahiri kwamba Magufuli anavinyemelea viatu vya Mohamed Morsi au aibu ya Mourinho.
This is a very stupid analogy! unawezaje kulinganisha klabu ya mpira na nchi. kwa akili yako unadhani ukishafanikiwa kuwa kocha mzuri unaweza kuwa rais mzuri? Mpira wanashindana walio na uwezo sawa ktk ligi, serikali inaendeshwa bila mashindano. Kuna nani ndani ya nchi anayeshindana na Magufuli? Kama hana mshindani, kwa nini unalinganisha na mambo ya mpira? Mambo ya ushabiki.
Hayo mawazo ndo yamemfanya aliyeondoka asijue nini ni muhimu ktk nchi. Alipojenga uwanja wa mpira akadhani kaleta maendeleo. akaleta kocha anayekomba mamilioni. Buree!
Chelsea imeshindwa kwa sababu kuna timu zilizotangulia mbele yake kwa vigezo vya kimpira. Serikali unailinganisha na ligi ipi? Nani atakayemzidi Magufuli ili aonekane ameshindwa?
Pau jose kahujumiwa na wachezaji......na magufuli atahujumiwa na wewe!
jana chelsea kashinda na washabiki wakawazome
haujui mpira
Duh! Kwa taarifa yako hakuna mfano mzuri wa teamwork kama mfano wa timu ya mpira. Na wachezaji wa Chelsea wame mfunfisha Mourinho somo ambalo hatakaa asahau ktk maisha yake.Mleta mada tofautisha mpira wa miguu na siasa
Huo ulio utoa wewe ni mfano mfu. Huwezi fananisha timu ya mpira wa miguu na darasa la primary. Huwezi fananisha timu ya watu wazima na darasa la watoto ambao hawaja balehe na ambao ndio wapo kwenye balehe.Naweza kusema method of management zinazofaa Africa and outside Africa varies, wewe umetumia mfano wa Mourinho, na mimi natumia mfano huu; baada ya fimbo kukatazwa mashuleni, unaonaje maadili ya watoto wetu? Tafakari
Wewe sema hukuelewa jibu
Alafu uwe mtu wa kukubali kueleweshwa kwenye mambo usio na ufahamu nayo.
Usikomae bure!
Hizo fimbo ufanisi wake uko wapi kwenye kujenga tafakuri jadidi (Critical thinking) katika jamii yetu. Hao waliochapwa si ndiyo hao wanaulizwa maswali ambayo majibu yake wanayo lakini kutokana na hofu ya kucharazwa bakora waliyojengwa nayo tangu wakiwa shuleni, wanaishia kutetemeka mbele ya wanasiasa kama walivyokuwa wanatetemeka mbele ya waalimu enzi zao wakiwa shuleni!!
Tafsiri yangu staili hii ya kuongoza nchi kwa kukandamiza na kudhalilisha wengine kwa faida ya kisiasa wewe ndiyo unaona ndiyo njia sahihi ya kuongoza taifa letu? Yaani Mawazo anaweza akauawa waliomuua wanasemwa hawafahamiki, huku mtu kuitwa Kibaka jeshi zima linamvamia aliyemwita kibaka mwenzie. Kweli nimeelewa ni kwa nini CCM inaendelea kushinda chaguzi!!
Umewah kuangalia mpira?Barcelona na Granada zina uwezo sawa?you must be onsane
Mleta Andiko la Mourinho JF anataka tuamini Mpira unaochezwa ni kati ya CCM NA CHADEMA (UKAWA) BALI KASAHAU TIMU NYINGINEZO VYAMA VINGINE.NA KWA MTAZAMO WAKE NI MFANO ULIYOPWAYA.KUONGOZA NCHI NA KUFANANISHA TIMU YA MPIRA AME-UNDERATE SANA TENA.BADO KINDA AJITAHIDI KUJIBIDISHA KUSOMA
Naweza kusema method of management zinazofaa Africa and outside Africa varies, wewe umetumia mfano wa Mourinho, na mimi natumia mfano huu; baada ya fimbo kukatazwa mashuleni, unaonaje maadili ya watoto wetu?
Mkakati ni kutumbua majipu kwanza then motivation itafuata kwa watakaosalia.
Huwezi wamotivate wapigaji ndugu yangu lazima nyumba iwe safi ndo uanze kazi.
Alafu kumbuka alidumu kama Waziri for 15 years kwa mikakati kama hii anayoifanya Leo.Akiwa ujenzi Aliwai timua vijana 400 wa mizani kwa rushwa leave alone wakandarasi ambao aliwatimua,alichoma nyavu za wavuvi haramu etc.
Tatizo wapo ambao wameanza kumjua JPM akiwa Raisi trace him back ndo utajua undani wake toka akiwa mkemia kule mwanza then mwalimu alafu naibu Waziri waiziri then utaona kama analysis yako itahold water
Mleta Andiko la Mourinho JF anataka tuamini Mpira unaochezwa ni kati ya CCM NA CHADEMA (UKAWA) BALI KASAHAU TIMU NYINGINEZO VYAMA VINGINE.NA KWA MTAZAMO WAKE NI MFANO ULIYOPWAYA.KUONGOZA NCHI NA KUFANANISHA TIMU YA MPIRA AME-UNDERATE SANA TENA.BADO KINDA AJITAHIDI KUJIBIDISHA KUSOMA