Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 891
Wadau Salaam na Heri ya x~mass na mwaka mpya!
Elimu na maarifa yanapatikana sehemu mbalimbali na kwa namna mbalimbali kama hauchoki kujifunza.
Kabla ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi sijawahi kudhani kama Magufuli anafaa kwa nafasi ya urais.
Lakini kwa sasa ndio anakalia kiti na demokrasia inatufundisha kuvumiliana bila kujali kama amekuwa rais kidemokrasia.
Kuna watu wamepongeza utendaji wake wa mwanzo wa kunyooshea vidole na kushusha lawama kwa watendaji wa serikali.
Kweli ameanza kwa makeke kama Mohamed Morsi kukata tawi alilokalia.
Ametumia nguvu kubwa kutuaminisha kuwa anafanya maamuzi kwa umakini mkubwa japo ukiangalia uteuzi wa kina Nape na Makamba unapata vipele vya baridi.
Anyway tusimnange sana kwa sasa ila tujaribu kutoa mtizamo wetu.
Jose Mourinho kocha gwiji kabisa wa Chelsea amepigwa chini.
Ni ajabu kuona mtaalamu huyu wa mpira mwenye vifaa vyote akishindwa kufanya kazi.Hakuwa na upungufu wa chochote kuanzia CV,wachezaji, fedha, mamlaka na support ya mashabiki lakini kazi ikashindikana.
Haijalishi uzuri wa mkakati wako kiuongozi lakini kama watu unaofanya nao kazi hawako nyuma yako basi hauwezi kufanikiwa.Mapungufu ya Mourinho yameonyesha umuhimu wa kuwaamini watendaji na kuwajengea kujiamini badala ya kuwatisha na kuwalaumu.
Kwa muda unaweza kuhamisha lawama za kushindwa kwako kuwasimamia watu kwa kuwaondoa kwa kisingizio cha mapungufu yao lakini baadae ukweli utabaki palepale na kushindwa kwako kutakua wazi.
Mourinho aliwatoa kina Lukaku, Andre Schurrle,Kevin de Bruyne na wengine wengi ila wakaenda kung'aa walikoenda na kina Costa,Fabregas,Willian wakaonekana kama kundi la watalii uwanjani.
Magufuli anapaswa kujua uongozi wa kileo ni mkakati pamoja na motivation.Uongozi wa kuamrisha na kutishia una nafasi kidogo sana ya mafanikio, tena ya muda mfupi.
Ni uongozi unaofaa zaidi jeshini wakati wa matatizo na hata hivyo majeshi mengi ya kisasa yameamua kuachana nao baada ya kuona ufinyu wa tija yake.
Mategemeo ya watanzania ni mengi kwa kadiri yalivyo matatizo yao.Ulaghai wa kufukuza, kusimamisha, kufungiana mageti,kuweka lock~up utadumu kwa muda tu.Kama suluhu za matatizo ya watanzania hazitapatikana ni dhahiri kwamba Magufuli anavinyemelea viatu vya Mohamed Morsi au aibu ya Mourinho.
Kuna wenzetu ni kama walirogwa na Lowassa. Hawataki kabisa kuamini kuwa uchaguzi umekwisha, Lowassa alishindwa, na Magufuli ndo rais. Ukisoma bandiko la huyu raia, hutoshindwa kubaini maumivu makubwa aliyonayo, maumivu ya kutotawaliwa na Lowassa, na chuki ya kutawaliwa na Magufuli.
Uhuru wa kujieleza is fine lakini nasi tutumie haki ya kudharau wapuuzi wanaomwombea mabaya rais wetu. They are as sore losers as Lowassa (at least EL in a way hapigi kelele compared to waumini wake)