Anguko la Jose Mourinho limfundishe kitu Magufuli

Anguko la Jose Mourinho limfundishe kitu Magufuli

Wameguswa kwani MIIKO NA MAADILI YA KUWA MFANYAKAZI WA UMMA ILITUPWA HUKO KITAMBO MH.RAISI KUIRUDISHA HAYA MABADILIKO WACHACHE WALIYOPO NA KUWEPO KWAO IMEKUWA SHEEDA NA RAISI NI TAASISI ISOMEKE HIVYO TUACHE MAZOEA YA KULEANA.UMEVURUNDA KAA PEMBENI NCHI HII NI WATANZANIA WENGI TENA WAZALENDO KWELI KWELI
 
Rais kufanya kazi kama waziri ni hatari sana
waziri wa ujenzi ana uhuru wa kufukuza kila anaemuona hafai
waliofukuzwa wanaweza kwenda mahakamani kupinga
wakishinda wanarudishwa....wakishindwa wanatafuta kazi kwingine

lakini Rais ni tofauti...yeye ana influence hadi mahakama....
hivyo anaweza fukuza watu kwa makosa na wasifanye lolote...

Vilevile hata wasio na kazi ni mzigo wake....waziri akufukuza kazi ndo basi
lakini Rais akifukuza hata robo tu ya wafanyakazi seikalini..huo mzigo ni wa kwake pia
mambo yata back fire...

Mimi naangalia tu maamuzi madogo kama ya kufukuza kazi wapishi wa Ikulu kwa madai kuwa first lady atapika.
Hawa si wana watoto mashuleni na familia zinazowategemea?
Kitu ambacho Magu anakisahau ni kuwa mafanikio ya watanzania ndio mafanikio yake!
Anakazi ya kujifunza namna ya kufanya vitu sahihi zaidi kuliko kufanya vitu visivyo sahihi kwa usahihi.
 
Andika lugha yoyote kati ya kiswahili na kiingereza nitakuelewa.
Usijali profession au terms

Nimeuliza kiwango chako cha elimu ili kwanza nijue kutokana na elimu yako ulielimika au ulimaliza madasa/vyuo elimu ukaiacha huko huko madarasani/vyuoni? kwa sababu 'coparative analysis' zinafanywa kwa 'issues' zinazoshabihiana. Mpira na siasa wapi na wapi?
 
Nimeuliza kiwango chako cha elimu ili kwanza nijue kutokana na elimu yako ulielimika au ulimaliza madasa/vyuo elimu ukaiacha huko huko madarasani/vyuoni? kwa sababu 'coparative analysis' zinafanywa kwa 'issues' zinazoshabihiana. Mpira na siasa wapi na wapi?

Sioni sababu ya kubishania namna ya kufanya analysis kama kigezo cha ukubwa wa elimu.
Mimi sijasoma saaana ila kwanza sahihisha neno 'coparative' lisomeke kwa namna ambayo litaleta maana.

Pili jitahidi kufikiria nje ya box.
Hii haikuwa paper kwamba nimepewa frame of reference na grounds of comparison.
Nilikuwa huru mno kuchagua na I had enough rationale for comparing.

Nimefocus kwenye team work, leadership skills and results. Item hizi ziko kwenye model zote mbili
Sijui kama nimekuwa mbunifu vya kutosha katika kufanya uchambuzi usichoshe lakini naimani nimejitahidi.
 
Magufuli, ULIAHIDI KUPANDISHA mishahara na PAYE kushuka.. mbona wafanyakazi hujawafanyia hayooo...??

1: Mishahara ni ileee ileeeeeeeeeee

2: PAYE iko pale paleeeeeeeeeeeeeeee


Wajinga ndio waliwao.... nimeamini..??


Magufuli au bado HUJAWA RAIS....!!?????

Watumishi wa umma wa dhiki kubwa sana sanaaa... tunawaona...!!

😨😨.. 👉 🚶🚶🚶🙆🙆... no money..!!
 
Kuna wenzetu ni kama walirogwa na Lowassa. Hawataki kabisa kuamini kuwa uchaguzi umekwisha, Lowassa alishindwa, na Magufuli ndo rais. Ukisoma bandiko la huyu raia, hutoshindwa kubaini maumivu makubwa aliyonayo, maumivu ya kutotawaliwa na Lowassa, na chuki ya kutawaliwa na Magufuli.

Uhuru wa kujieleza is fine lakini nasi tutumie haki ya kudharau wapuuzi wanaomwombea mabaya rais wetu. They are as sore losers as Lowassa (at least EL in a way hapigi kelele compared to waumini wake)

Mlalahoi
Mimi nimetoa ushauri na sijamuombea rais wenu mabaya.
Sasa haya ya El na waumini wake yanakujaje hapa?
 
Mawazo ya viroba haya. Au wewe Bavicha??????


Wadau Salaam na Heri ya x~mass na mwaka mpya!

Elimu na maarifa yanapatikana sehemu mbalimbali na kwa namna mbalimbali kama hauchoki kujifunza.
Kabla ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi sijawahi kudhani kama Magufuli anafaa kwa nafasi ya urais.

Lakini kwa sasa ndio anakalia kiti na demokrasia inatufundisha kuvumiliana bila kujali kama amekuwa rais kidemokrasia.

Kuna watu wamepongeza utendaji wake wa mwanzo wa kunyooshea vidole na kushusha lawama kwa watendaji wa serikali.
Kweli ameanza kwa makeke kama Mohamed Morsi kukata tawi alilokalia.

Ametumia nguvu kubwa kutuaminisha kuwa anafanya maamuzi kwa umakini mkubwa japo ukiangalia uteuzi wa kina Nape na Makamba unapata vipele vya baridi.

Anyway tusimnange sana kwa sasa ila tujaribu kutoa mtizamo wetu.
Jose Mourinho kocha gwiji kabisa wa Chelsea amepigwa chini.
Ni ajabu kuona mtaalamu huyu wa mpira mwenye vifaa vyote akishindwa kufanya kazi.Hakuwa na upungufu wa chochote kuanzia CV,wachezaji, fedha, mamlaka na support ya mashabiki lakini kazi ikashindikana.

Haijalishi uzuri wa mkakati wako kiuongozi lakini kama watu unaofanya nao kazi hawako nyuma yako basi hauwezi kufanikiwa.Mapungufu ya Mourinho yameonyesha umuhimu wa kuwaamini watendaji na kuwajengea kujiamini badala ya kuwatisha na kuwalaumu.

Kwa muda unaweza kuhamisha lawama za kushindwa kwako kuwasimamia watu kwa kuwaondoa kwa kisingizio cha mapungufu yao lakini baadae ukweli utabaki palepale na kushindwa kwako kutakua wazi.
Mourinho aliwatoa kina Lukaku, Andre Schurrle,Kevin de Bruyne na wengine wengi ila wakaenda kung'aa walikoenda na kina Costa,Fabregas,Willian wakaonekana kama kundi la watalii uwanjani.

Magufuli anapaswa kujua uongozi wa kileo ni mkakati pamoja na motivation.Uongozi wa kuamrisha na kutishia una nafasi kidogo sana ya mafanikio, tena ya muda mfupi.
Ni uongozi unaofaa zaidi jeshini wakati wa matatizo na hata hivyo majeshi mengi ya kisasa yameamua kuachana nao baada ya kuona ufinyu wa tija yake.

Mategemeo ya watanzania ni mengi kwa kadiri yalivyo matatizo yao.Ulaghai wa kufukuza, kusimamisha, kufungiana mageti,kuweka lock~up utadumu kwa muda tu.Kama suluhu za matatizo ya watanzania hazitapatikana ni dhahiri kwamba Magufuli anavinyemelea viatu vya Mohamed Morsi au aibu ya Mourinho.
 
Liverpoolfc tulikuwa na Rodgers; Wachezaji wale wale na habari ikashindikana.Tena wa kununua yeye mwenyewe, amekuja Clopp na kuna mabadiliko ya mara moja.Focus on leadership skills

Liverpool imebadilika? mmmh Ajabu mechi alizo cheza Rodgers na kulinganisha na za Clopp hadi sasa Rodgers ana point zaidi.... Liverpool ni Liverfool kamwe haiwezi badilika.... na Washabiki wake wana Moyo wa Plastic Jua likiwa kali wanalainika
 
Back
Top Bottom