Anguko la Jose Mourinho limfundishe kitu Magufuli

Anguko la Jose Mourinho limfundishe kitu Magufuli

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,346
Reaction score
9,846
Wadau Salaam na Heri ya x~mass na mwaka mpya!

Elimu na maarifa yanapatikana sehemu mbalimbali na kwa namna mbalimbali kama hauchoki kujifunza.
Kabla ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi sijawahi kudhani kama Magufuli anafaa kwa nafasi ya urais.

Lakini kwa sasa ndio anakalia kiti na demokrasia inatufundisha kuvumiliana bila kujali kama amekuwa rais kidemokrasia.

Kuna watu wamepongeza utendaji wake wa mwanzo wa kunyooshea vidole na kushusha lawama kwa watendaji wa serikali.
Kweli ameanza kwa makeke kama Mohamed Morsi kukata tawi alilokalia.

Ametumia nguvu kubwa kutuaminisha kuwa anafanya maamuzi kwa umakini mkubwa japo ukiangalia uteuzi wa kina Nape na Makamba unapata vipele vya baridi.

Anyway tusimnange sana kwa sasa ila tujaribu kutoa mtizamo wetu.
Jose Mourinho kocha gwiji kabisa wa Chelsea amepigwa chini.
Ni ajabu kuona mtaalamu huyu wa mpira mwenye vifaa vyote akishindwa kufanya kazi.Hakuwa na upungufu wa chochote kuanzia CV,wachezaji, fedha, mamlaka na support ya mashabiki lakini kazi ikashindikana.

Haijalishi uzuri wa mkakati wako kiuongozi lakini kama watu unaofanya nao kazi hawako nyuma yako basi hauwezi kufanikiwa.Mapungufu ya Mourinho yameonyesha umuhimu wa kuwaamini watendaji na kuwajengea kujiamini badala ya kuwatisha na kuwalaumu.

Kwa muda unaweza kuhamisha lawama za kushindwa kwako kuwasimamia watu kwa kuwaondoa kwa kisingizio cha mapungufu yao lakini baadae ukweli utabaki palepale na kushindwa kwako kutakua wazi.
Mourinho aliwatoa kina Lukaku, Andre Schurrle,Kevin de Bruyne na wengine wengi ila wakaenda kung'aa walikoenda na kina Costa,Fabregas,Willian wakaonekana kama kundi la watalii uwanjani.

Magufuli anapaswa kujua uongozi wa kileo ni mkakati pamoja na motivation.Uongozi wa kuamrisha na kutishia una nafasi kidogo sana ya mafanikio, tena ya muda mfupi.
Ni uongozi unaofaa zaidi jeshini wakati wa matatizo na hata hivyo majeshi mengi ya kisasa yameamua kuachana nao baada ya kuona ufinyu wa tija yake.

Mategemeo ya watanzania ni mengi kwa kadiri yalivyo matatizo yao.Ulaghai wa kufukuza, kusimamisha, kufungiana mageti,kuweka lock~up utadumu kwa muda tu.Kama suluhu za matatizo ya watanzania hazitapatikana ni dhahiri kwamba Magufuli anavinyemelea viatu vya Mohamed Morsi au aibu ya Mourinho.
 
Naweza kusema method of management zinazofaa Africa and outside Africa varies, wewe umetumia mfano wa Mourinho, na mimi natumia mfano huu; baada ya fimbo kukatazwa mashuleni, unaonaje maadili ya watoto wetu?
 
Lowassa ndo wa kujifunza make alipanda akfikia kuiona Tz yote yake wakati hakuwa na mamlaka na sahivi anaishia kufoji popularity
 
Bado hiyo ni safisha safisha, nyumba imejaa uchafu sana. Mpe muda wa usafi. Mpe muda wa kuwaka new furniture. Mpe muda wa kumanage. Ndio uone motivation principles zikifanya kazi. Wanaotolewa ni matapeli tu. Mfano hao police fake 210.
 
Yaani kwa mimi naona mchemko wa mfananisho wako.

Unazani Jose angekuwa na uwezo wa kuondoa wale viburi wachache ingekuwaje?

Sasa Magufuli ni juu nenda kafanye uzembe anakuondoa hasubiri mwenye mali au mwenye kumiliki nchi aamue as hakuna

Upo?
 
Kamwwe hataweza kufanikiwa. Tanzania chini ya CCM siyo nchi ya kujivunia!

Utatumbuaje jipu na wewe ni jipu bana. Haki na usawa bila upendeleo ikitendwa kwa uwaz huyu sasa anayejiita mtumbua jipu atapona?

Kinachoitajika sasa hiv ni kusameehana maridhiano na makubaliano. Sasa unatumbua wengine jipu na wewe jipu

Si tupo humu humu JF
 
Mimi naona management ya club imefanya haraka sana maana wazembe wamo mle mle ndani

Liverpoolfc tulikuwa na Rodgers; Wachezaji wale wale na habari ikashindikana.Tena wa kununua yeye mwenyewe, amekuja Clopp na kuna mabadiliko ya mara moja.Focus on leadership skills
 
Lowassa ndo wa kujifunza make alipanda akfikia kuiona Tz yote yake wakati hakuwa na mamlaka na sahivi anaishia kufoji popularity

Lowassa amefikaje kwenye hii mada. Muache rais wetu!
 
Naweza kusema method of management zinazofaa Africa and outside Africa varies, wewe umetumia mfano wa Mourinho, na mimi natumia mfano huu; baada ya fimbo kukatazwa mashuleni, unaonaje maadili ya watoto wetu? Tafakari

Waafrika ni binadamu kama binadamu wengine duniani.
Ukisema kuongoza Afrika na nnje ya Afrika kuna tofauti ni kudhalilisha utu wa mwafrika.
Ni kuto kutambua kazi ya uhuru.
Ni kuwa na mawazo sawa na mkoloni, ni kujipinga mwenyewe!
 
Waafrika ni binadamu kama binadamu wengine duniani.
Ukisema kuongoza Afrika na nnje ya Afrika kuna tofauti ni kudhalilisha utu wa mwafrika.
Ni kuto kutambua kazi ya uhuru.
Ni kuwa na mawazo sawa na mkoloni, ni kujipinga mwenyewe!

Swadakta mkuu
 
baada ya fimbo kukatazwa mashuleni, unaonaje maadili ya watoto wetu? Tafakari
Hizo fimbo ufanisi wake uko wapi kwenye kujenga tafakuri jadidi (Critical thinking) katika jamii yetu. Hao waliochapwa si ndiyo hao wanaulizwa maswali ambayo majibu yake wanayo lakini kutokana na hofu ya kucharazwa bakora waliyojengwa nayo tangu wakiwa shuleni, wanaishia kutetemeka mbele ya wanasiasa kama walivyokuwa wanatetemeka mbele ya waalimu enzi zao wakiwa shuleni!!

Tafsiri yangu staili hii ya kuongoza nchi kwa kukandamiza na kudhalilisha wengine kwa faida ya kisiasa wewe ndiyo unaona ndiyo njia sahihi ya kuongoza taifa letu? Yaani Mawazo anaweza akauawa waliomuua wanasemwa hawafahamiki, huku mtu kuitwa Kibaka jeshi zima linamvamia aliyemwita kibaka mwenzie. Kweli nimeelewa ni kwa nini CCM inaendelea kushinda chaguzi!!
 
This is a very stupid analogy! unawezaje kulinganisha klabu ya mpira na nchi. kwa akili yako unadhani ukishafanikiwa kuwa kocha mzuri unaweza kuwa rais mzuri? Mpira wanashindana walio na uwezo sawa ktk ligi, serikali inaendeshwa bila mashindano. Kuna nani ndani ya nchi anayeshindana na Magufuli? Kama hana mshindani, kwa nini unalinganisha na mambo ya mpira? Mambo ya ushabiki.

Hayo mawazo ndo yamemfanya aliyeondoka asijue nini ni muhimu ktk nchi. Alipojenga uwanja wa mpira akadhani kaleta maendeleo. akaleta kocha anayekomba mamilioni. Buree!

Chelsea imeshindwa kwa sababu kuna timu zilizotangulia mbele yake kwa vigezo vya kimpira. Serikali unailinganisha na ligi ipi? Nani atakayemzidi Magufuli ili aonekane ameshindwa?

Punguza presha
Comparing models doesn't make them same, unless there is no meaning of comparisons.
The differences of models can be different but the likes can also be like.
 
Back
Top Bottom