Mourinho; Rodri alikataa ofa kubwa Real Madrid

Mourinho; Rodri alikataa ofa kubwa Real Madrid

Miss Halima

Senior Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
170
Reaction score
382
Kocha wa Real Madrid, José Mourinho, hatimaye amezungumza baada ya Real Madrid kushindwa kumsajili Rodri, ambaye alijiunga na wapinzani wao Barcelona, siku ya Jana.

Mourinho alifichua kwamba Real Madrid, walitoa ofa kubwa lakini rodri aliikataa,

“Nilizungumza naye mara kadhaa na Real Madrid ilimpa ofa nzuri sana. Nadhani tuna uhusiano mzuri sana na City. Bila kufanya mazungumzo na City, klabu ilifanya mawasiliano na Rodri na ikampa ofa kubwa. Rodri alikuwa na mashaka, alisita, na mashaka yake yakaanza kunifanya na mimi kuwa na mashaka,” alisema Mourinho.

“Hakuna jambo baya la kusema, Lakini Real Madrid ni klabu yenye hadhi kubwa kiasi kwamba haiwezi kuwa na wachezaji ambao wanaendelea kuwa na mashaka. Unapomtafuta mchezaji na yeye anakuuliza, ‘Ni lini natakiwa kuja?’ Hiyo ndiyo dhana fulani tuliyonayo. Lakini alikuwa na heshima sana kwetu. Namwombea kila la heri... siyo sana, kwa kweli, lakini namtakia kila la heri,” Mourinho alisema.

“Simkosi Rodri. Hatuwakosi wachezaji. Sisemi kwamba hakutakuwa na usajili mwingine kwa sababu dirisha la usajili bado liko wazi, lakini kama unaniuliza moja kwa moja kama kwangu dirisha limefungwa... ndiyo, limefungwa. Naipenda sana hii timu,” Mourinho alimalizia.

rodrigo.png
 
Rodri hawezi kufit pale Los Blancos, ndio maana kataka Camp Nou.
 
Real Madrid inawavutia wachezaji wa kazi chafu kama akina Claude Makelele, Enzo Fernandez, nk. Mpira laini laini uko Barcelona.
 
Hapa atakuja atakuja ndugu makovu Scars atakwambia Barca wamepigwa kwa Rodri.

Wakati wao walimpa ofa nono zaidi na akawakataa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom