Spike Lee aliyekuambia hela ya ruzuku ya chama kingine cha siasa ukiacha kile kilicho madarakani ni kwa ajili ya maendeleo ni nani? Kabla hujaleta mada hapa hebu soma kwanza machapisho ujue undani wa unachotaka kusema. Sasa na CUF na vyama vingina si vinapata ruzuku? Wao umewaweka upande gani? Mnatumika sana kuisakama CDM ila jeuni kwamba Watanzania hawadanganyiki tena!!! Leteni kila pumba na washawasha hapa lakini hakuna anayekubali kuwashwa tena!! Pro SSM na wake zake na wanawe at work!!! Mpaka 2015 mtakuwa umezusha weee na hakuna wa kuasikiliza. Waite na rafiki zangu Rejao, Ritz, Zomba, Chama, et al... waje wakuunge mkono.
Anguko la waliokutuma ndilo liko njiani maana wameshinda kutekeleza azma ya maisha bora kwa kila mtanzania badala yake tumekuwa na maisha bora ya mafisadi, walarushwa, wabadhirifu, wezi, majangili hadi polisi wamo, yaani ni uozo mtupu. Unajua asilimia 69.5 ya Watanzania wanakula mlo mmoja kwa siku ambao ni chini ya dola moja gharama yake? Shule mmeshinda hadi mnapeleka alama Chee na Deee sekondari!!! Ni kitu gani mmefaulu? Mkiangalia hata katika Millenium Development Goals, mlichoweza ni kidogo sana wakati hela ya Donors ni kibao na mnatia tumboni kwa uroho wenu tu na sasa wameamua wanataka kubwaga manyanga!! Aibu yenu!!