Hii ni simple research niliyo ifanya lakini ina mashiko sana kubali au kataa lakini ndio ukweli,
1. chadema ni chama cha siasa kilicho ibuka na kujipatia wanachama wengi kwa muda mfupi sana kiasi
2. kukosa misingi imara ya kiuongozi kuanzia ngazi za matawi,kata,majimbo mpaka taifani.
3. that is why kila mtu ndani ya chama ana sauti au kwa lugha nyingine kila mtu ndani ya chama ni mbabe.
4. kwa ccm kupenya ndani ya cdm na kuwarubuni baadhi ya viongozi wa chama ktk ngazi zote na hatimae hata zinapo fanyika chaguzi utakuta ccm wanashinda kiurahisi sana kwenye maeneo mengi ya mijini na vijijini.
5. NIDHAMU YA KIUONGOZIkwa wanachama wote kwa ujumla,.
Mkuu Asante sana kwa Research yako ambayo imewakilisha majibu fulani kwa maswali ambayo umekuwa ukijiuliza, lakini embu tufanye critical thinking Kidogo.
1. Unaposema Kimeibuka kwa muda mfupi una maanisha nini? muda mfupi toka lini? Mfumo wa vyama vingi Tanzania umeanza mwaka 1992 na CHADEMA kama vilivyo vyama vingine vya upinzani vya NCCR_Mageuzi na CUF vilisajiriwa mwaka 1992. Hivyo CHADEMA ni miongoni mwa vyama vichache sana vya mwanzo vya upinzani? sasa kwanini umesema kimeibuka? na Pia kwanini usema muda mfupi? unalinganisha na nini? kwani hata CCM wanachokiita CHAMA kikongwe kisahiriwa upya kwa sheria mpya ya vyama vingi mwaka 1992 kwa hiyo ukizungumzia perspective ya usajili kwa sheria yetu ya vyama vya siasa tuliyo nayo sasa CCM, CUF, NCCR-Mageuzi, CHADEMA vimesajiriwa 1992.
2. Misingi ya Uongozi ni Nini? Mimi nadhani CHAMA kinaongozwa kwa kufuata kanuni, taratibu zilizokubaliwa na vikao halali vya chama zikisimamiwa na KATIBA. Kwa hiyo kama viongozi wanafanya maamuzi yaliyo ndani ya kanuni, taratibu na makubaliano ya vikao halali vya CHAMA kwa kuzingatia katiba basi hapo hatuwezi kusema kuna Ombwe la Uongozi. CHADEMA siku zote wamesema wamezingatia hayo, unless wewe unataka kuwa-prove wrong kuwa sio wakweli, kwa hiyo leta evidence kuonyesha kuwa uongozi umeyumba kw akufanya maamuzi haya na haya yasiyo zingatia katiba, kanuni na taratibu za chama. (Evidence based)
3. Kivipi unasema kila mtu ndani ya CHAMA ni Mbabe? nikupe mfano, UDP walijaribu kumfukuza Cheyo wakakwaa kisiki, NCCR_Mageuzi wakajaribu kumfukuza Mrema, matokeo yake CHAMA kikafa natura death, Lakini CHADEMa imewafukuza akina Kitila Mkumbo, M/Kiti wa Mkoa wa ARusha Samsoni Mwigamba, wametoka na CHAMA bado ni Imara. M/M/Kiti Bara Arfi kajiuzuru lakini chama hakijatetereka au wewe unaonaje?? Kama "CHAMA" kikiamua hata kuwatimua Mbowe na Dr. Slaa watatoka na Chama kitaendelea kusonga mbele? au vipi? kwa hiyo siuooni ubabe wowote ndani ya chama kutoka kwa wanachama labda unipe mifano ambayo kwenye utafiti wako uliizingatia kufikia hitimisho hilo.
4. Mpaka sasa kwa kuangalia uwingi wa kadi zainazorudishwa katika mikutano ya hadhara, CHADEMA ndio inaongoza kuchukua wanachama wa CHADEMA, na pia inaongoza kwa kuingiza wanachama wapya. Umetumia kigezo gani kusema CCM inawarubuni wanachama na viongozi wa CHADEMA? kuna mfano wowte hai juu ya hili? CCM haiwezi kubebeshwa lawama kwa matatizo mengi ambayo CHADEMA inaweza ikawa inayapata, mengine ni ya kimuundo, mengine kisera na hata hulka za viongozi wetu na wapambe wao. CCM amekuwa kama shetani ambaye wanawadamu wanamsingia kila aina ya dhambi. CHADEMA inahitaji kujitafakari internally na kujipima na vyama vilivyo simama na kuona namna gani vina handle issue zao na wanaongoza vipi vyama, kwa mfano waharaka haraka angalia ODM wanavyo handle kesi ya akina Abwabu Vs Grace Zani ya kugombea nafadi ya Ukatibu mkuu na hatimaye uchaguzi kuvunjika.
5. Concept ya NIDHAMU ni HOJA ya kubuniwa iliyotengenezwa maalum kwa mkakati maalum kuwarubuni wanachama na wafuasi wa CHADEMA ili kukubaliana na baadhi ya hoja ambazo baadhi ya viongozi walitaka kuzipitisha dhidi ya wanachama au viongozi wenzao. Nidhamu ni relative term, kwenye katiba au kanuni za chama hazijaainisha wazi wazi kuwa mambo gani yakitendwa na mwanachama yataitwa ni utovu wa nidhamu, mtu anaweza akasema Peopleeees kabla ya mwenyekiti na mwanachama mwingine akasimamia hoja kuwa ulikuwa ni ukiukaji wa maadili na utovu wa nidhamu, madamu anayesema hilo ni kiongozi wa juu mwenye influence kuna hatari ya huyo mwanachama aliyesema Peopleees kufukuzwa uanachama wake.
Nashukuru sana kwa reserach yako nzuri na findings ulizozipata zimetupa kitu cha kujadili