Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,404
CCM kama ilivyo kwa waasisi wake TANU na ASP vilianzishwa ili kupigania uhuru wa mtu mweusi kutoka katika mikono ya weupe wachache. Ili kufanikisha hili ililazimu kuwaunganisha wananchi kwa njia mbali mbalimbali ikiwemo propaganda, viongozi wa jadi, viongozi wa dini nk.
Baada ya uhuru, lengo lilikua kusaidia nchi nyingine za Afrika kupata Uhuru. Vyama rafiki kama Frelimo, Swapo, ANC nk vilijiunga na sisi. Adui bado alikua ni Kaburu na Beberu. Kwa nia njema kutokana na uchaguzi wa nchi zetu, viongozi wetu waliamua kufuata mfumo wa Kijamaa ili kugawa kilichopo kwa watu wote sawa. Siasa za kijamaa zilitufanya kuwa wahanga wa Vita Baridi kwani tulikuwa upande wa Urusi na China. Mabeberu walituona ni tishio.
Nyakati zinebadilika, sasa hivi tunapigania mabadiliko ya kiuchumi na maisha bora. Mass Media imeleta mabadiliko makubwa. Vijijini watu wanafahamu kuwa wanaweza kuishi kwa umeme wa solar na wakavuna maji ya mvua na kuishi maisha bora zaidi. Mpinzani wetu si Kaburu tena bali ni sisi wenyewe tunataka kuishi maisha bora.
Propaganda za kutubagua na viongozi wa upinzani haziwezekani. Hawa viongozi ni ndugu zetu, tulijua nao, tulisoma nao na wengine ni ninamuonea zetu. Hawa si Makaburu wala si mabeberu. Kama vilivyoanguka vyama vingine vya siasa vilivyopigania uhuru. CCM haipiganii tena ukombozi.