Angetile Osiah ang'olewa TFF

Angetile Osiah ang'olewa TFF

Sawa sawa kama kuna baadhi ya watu walikuwa wakionekana wapowapo tu basi wapumzike tu make kila siku kwa mfano tunalia na JK kumweka Mwandosya hana wizara maalumu na afya yake ilivyo so what?

haya akina Lukuvi na Wassira wana msaada gani kwenye baraza la mawaziri? ...mwacheni Malinzi afanye kazi yake si katoa siku 100?ama mlifikiri hizo siku ni kunywa tu na kulala?kuna watakaonuna na kucheka,ndo hivyo.
 
Ande haki bila kumuonea mtu
wabadhirifu wawajibishwe haraka sana.
 
Ukisikia safisha ya Malinzi chini ya vijna alio nao ndiyo hiyo imeanza kaa mkao wa kula lazima kieleweke.Matola,Matola,Matola Over!

Matola,gfsnowin.
 
Last edited by a moderator:
Tunataka mafaniko mapya ktk soka lasivyo tuwekeze Timu ya akina dada Tanzanite na Twiga Stars. Mbona hujauliza JK anazo mlipa Ekelege wa TBS na Jairo wa nishati na Madini!!
1. Mafanikio hayaji kwa kimwondoa kila anayekutikana madarakani.
2. Si kila mshabiki wa mpira ni mshabiki wa siasa chelema kama unavyoonekana ndivyo ulivyo. Mifano unayoitoa hainihusu kwa sababu unaowatolea hiyo mifano hawanihusu.
 
Kifuatacho TFF ni Julio kufungiwa kujihusisha na mambo ya soka kwa miaka 20 (ishirini).


Mkuu Julio hana adabu alishazoea ugomvi,nakumbuka mapem mwaka huu wakati wa mechi ya simba na Toto Africans pale mwanz alipigwa ngumi baada ya kuanzisha ugomvi akavimba jicho mshari sana huyu jamaa!
 
1. Mafanikio hayaji kwa kimwondoa kila anayekutikana madarakani.
2. Si kila mshabiki wa mpira ni mshabiki wa siasa chelema kama unavyoonekana ndivyo ulivyo. Mifano unayoitoa hainihusu kwa sababu unaowatolea hiyo mifano hawanihusu.

Mkuu hujasomeka vizuri hebu weka maandishi sawa sawa ili ueleweke vizuri,samahani mkuu!!
 
Kikao cha kwanza cha kamati mpya ya utendaji ya TFF kimempa likizo katibu mkuu wa kuajiriwa, Angetile Osiah mpaka mkataba wake utakapomalizika Desember na watamlipa stahiki zake. Kikao iko chini ya Rais Jamal Malinzi, kimeamua kwamba ofisa habari bwana Boniface Wambura atakaimu nafasi ya Angetile kuanzia leo.
Source: mwanaspoti FB page

ni mawe juu ya mawe,
 
Kituko cha pili.1.Kufuta hukumu zote mara baada ya kuchaguliwa wakati hukumu hizo zilitolewa na kamati ambazo kikatiba ni huru.Anayewasamehe watu kienyeji hivyo tegemea pia atawahukumu kienyeji.Huu ndo mwisho wa TFF kama taasisi.Its a one man show now.
2.Kiongozi mweledi hawezi kuanza kwa kumfukuza ntendaji mkuu wa taasisi.Hii ni visasi na ubinafsi.Ndio hulka yao hawa jamaa hata dioniz pale gymkhan club upande wa golf ndivyo alivyofanya na kupaharibu
Ni one man show kweli. Kama alivyo yule jamaa wa ujenzi. Naona Jazba ndiyo inayoongoza TFF kwa sasa.
 
weka ndani Tenga


Mkuu kwa mara ya Kwanza utasikia Hakimu Nyamlani anashitakiwa na kufikishwa mahakamani mbele ya hakimu kama yeye!tulia na usikilizie,na analijua hili muosha huoshwa!hii ndio Dunia hadaa Malimwengu shujaa!

@ gfsnowin
 
Ni one man show kweli. Kama alivyo yule jamaa wa ujenzi. Naona Jazba ndiyo inayoongoza TFF kwa sasa.


Kama wao walivyoongozwa na Jazba mpaka kumuengua Jamal Malinzi kwenye kinyang'anyiro cha urais mapema mwaka huu kabla ya uchaguzi kufutwa na FIFA.
 
Sawa sawa kama kuna baadhi ya watu walikuwa wakionekana wapowapo tu basi wapumzike tu make kila siku kwa mfano tunalia na JK kumweka Mwandosya hana wizara maalumu na afya yake ilivyo so what?

haya akina Lukuvi na Wassira wana msaada gani kwenye baraza la mawaziri? ...mwacheni Malinzi afanye kazi yake si katoa siku 100?ama mlifikiri hizo siku ni kunywa tu na kulala?kuna watakaonuna na kucheka,ndo hivyo.
Ndege wa aina moja huruka pamoja. Na kwa jina lako (Rweyemamu?) haiyumkini basi huyu Malinzi ni home boy wako!
 
Kifuatacho TFF ni Julio kufungiwa kujihusisha na mambo ya soka kwa miaka 20 (ishirini).

mkuu julio akifungiwa tutakosa msisimko kwenye ligi, alafu kumbuka uyu jamaa ni kocha wa timu ya taifa
 
Ni sawa kabisa hata rais akiingia
madarakani lazima apange safu yake upya. Big up Malinzi
 
Mwanzo mzuri... Ikiwezekana pia huu uonozi uliomaliza muda wake uwajibishwe.

Hata JK alianza hivi hivi alipopata Urais kwa mara ya kwanza akatinga soko la Tandale kujionea Uozo. Mi nabaki nacheka tu!
 
Kama wao walivyoongozwa na Jazba mpaka kumuengua Jamal Malinzi kwenye kinyang'anyiro cha urais mapema mwaka huu kabla ya uchaguzi kufutwa na FIFA.

Nimefurahi kusikia jamaa kang'olewae. Mimi ni mmoja wa watu wliotaka jamaa atoswe hii imo kwenye waraka wangu kwa Malinzi. Bado Sayuni ( Kayuni)
 
Kama wao walivyoongozwa na Jazba mpaka kumuengua Jamal Malinzi kwenye kinyang'anyiro cha urais mapema mwaka huu kabla ya uchaguzi kufutwa na FIFA.

Jino kwa jino, undava undava, ukenge ukenge na ng'ato gi ng'ato; mwendo mdundo, Malinzi kanyaga twende!
 
mkuu julio akifungiwa tutakosa msisimko kwenye ligi, alafu kumbuka uyu jamaa ni kocha wa timu ya taifa

Mgomvi sana, kule Mwanza alipigana, Tanga usiseme: Kama siyo yeye zile vurugu za pale Taifa zisingetokea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom