Angetile Osiah ang'olewa TFF

Angetile Osiah ang'olewa TFF

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,393
Kikao cha kwanza cha kamati mpya ya utendaji ya TFF kimempa likizo katibu mkuu wa kuajiriwa, Angetile Osiah mpaka mkataba wake utakapomalizika Desember na watamlipa stahiki zake.

Kikao kiko chini ya Rais Jamal Malinzi, kimeamua kwamba ofisa habari bwana Boniface Wambura atakaimu nafasi ya Angetile kuanzia leo.

Source: Mwanaspoti FB page
 
Mwanzo mzuri... Ikiwezekana pia huu uonozi uliomaliza muda wake uwajibishwe.
 
Wambura Yukon fiti, ila huyo an gentile sijui nyamlani wamekula pesa ya tff bureee
 
Ngeta anaongea sana na ana kibri sana yule jamaa...bora kawekwa kando.
 
uteuzi ndiyo huo umeshaanza , mambo ya kambi hayo na juhudi za kampeni
 
Jamal endelea kupunyua mmoja baada ya mwingine
 
Kama ana makosa si achukuliwe hatua za kisheria na/au kinidhamu tu, kuliko kutumia hela ya umma (hata kama ni ya TFF) kumlipa mshahara na mrupurupu mfanyakazi aliyelala nyumbani? Ndiyo matumizi sahihi ya fedha ya umma hayo? Tujuwe hatahuyo Wambra atalipwa cha juu kwa kufanya kazi ya mtu mwingine!
 
Hili ni miongoni mwa yale yaliyotarajiwa....

Ndiyo maana na wao walipambana hadi dakika ya mwisho..
 
Kuna tetesi huenda Michael Wambura akapewa Ukatibu Mkuu
 
Kituko cha pili.

1. Kufuta hukumu zote mara baada ya kuchaguliwa wakati hukumu hizo zilitolewa na kamati ambazo kikatiba ni huru. Anayewasamehe watu kienyeji hivyo tegemea pia atawahukumu kienyeji. Huu ndo mwisho wa TFF kama taasisi. It's a one man show now.

2. Kiongozi mweledi hawezi kuanza kwa kumfukuza ntendaji mkuu wa taasisi. Hii ni visasi na ubinafsi. Ndio hulka yao hawa jamaa hata Dioniz pale Gymkhana Club upande wa golf ndivyo alivyofanya na kupaharibu
 
Kama ana makosa si achukuliwe hatua za kisheria na/au kinidhamu tu, kuliko kutumia hela ya umma (hata kama ni ya TFF) kumlipa mshahara na mrupurupu mfanyakazi aliyelala nyumbani? Ndiyo matumizi sahihi ya fedha ya umma hayo? Tujuwe hatahuyo Wambra atalipwa cha juu kwa kufanya kazi ya mtu mwingine!

Tunataka mafaniko mapya ktk soka lasivyo tuwekeze Timu ya akina dada Tanzanite na Twiga Stars. Mbona hujauliza JK anazo mlipa Ekelege wa TBS na Jairo wa nishati na Madini!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom