Kuna tetesi huenda Michael Wambura akapewa Ukatibu Mkuu
Sasa hivi mtajuta kwanini mmemchagua mfanyabiashara aongoze mpira na hivi ndio ameanza kupanga timu yake ya wizi!!! Atawajaza WASHOMILE wenzie ili waibe vizuri.
Kuna tetesi huenda Michael Wambura akapewa Ukatibu Mkuu
Kuna tetesi huenda Michael Wambura akapewa Ukatibu Mkuu
Samahani kwa kukosa kueleweka, ila hoja zangu ni kwamba:Mkuu hujasomeka vizuri hebu weka maandishi sawa sawa ili ueleweke vizuri,samahani mkuu!!
Osiah ambaye aliapa kwamba Malinzi na Wambura hawataingia madarakani ndo mtu wa visasi...Nchi ya visasi, kuanzia siasani mpaka michezoni..
hahahah.. kuzaliwa tu Tanzania tayar umeingia kwenye maajabu ya dunia.
Ndege wa aina moja huruka pamoja. Na kwa jina lako (Rweyemamu?) haiyumkini basi huyu Malinzi ni home boy wako!
Kituko cha pili.
1. Kufuta hukumu zote mara baada ya kuchaguliwa wakati hukumu hizo zilitolewa na kamati ambazo kikatiba ni huru. Anayewasamehe watu kienyeji hivyo tegemea pia atawahukumu kienyeji. Huu ndo mwisho wa TFF kama taasisi. It's a one man show now.
2. Kiongozi mweledi hawezi kuanza kwa kumfukuza ntendaji mkuu wa taasisi. Hii ni visasi na ubinafsi. Ndio hulka yao hawa jamaa hata Dioniz pale Gymkhana Club upande wa golf ndivyo alivyofanya na kupaharibu
thanx God mgonjwa out. Bado Sunday Kayuni.
Tatizo letu sisi wabongo ukimsamehe mtu ndio unampa nafasi ya kukumaliza!Nadhani kuna naafasi ya kushauri zaidi. MANDELE NELSON, Alichokifanya mara baada ya kutoka jela, ni kuwasamehe wale wote ambao walimfanyizia. Wakati mwingine, adhabu kubwa kabisa ya kumpatia mkosefu ni kumsamehe. Ni vigumu sana na ndiyo maana kila anayeanza na MUNGU humaliza na MUNGU.
Kuna tetesi huenda Michael Wambura akapewa Ukatibu Mkuu
Kikao cha kwanza cha kamati mpya ya utendaji ya TFF kimempa likizo katibu mkuu wa kuajiriwa, Angetile Osiah mpaka mkataba wake utakapomalizika Desember na watamlipa stahiki zake.
Kikao kiko chini ya Rais Jamal Malinzi, kimeamua kwamba ofisa habari bwana Boniface Wambura atakaimu nafasi ya Angetile kuanzia leo.
Source: Mwanaspoti FB page
Nadhani tunakosea kutofautisha baina ya kusamehe na kusahau. Mandela aliwasamehe wote waliohusika na mateso yake ya miaka 27 Gerezani. Walimkosea, kwa sababu alikuwa ni raia mzawa aliyetaka kuona uongozi wa nchi yake unapatikana kwa ridhaa ya walio wengi. Hilo lilionekana kosa, tena la uhaini, mbele ya makaburu. Lakini ni sheria batili mbele ya ile ya kimataifa. Malinzi hakuwa amefungwa hata kwa maana ya kiuongozi wa michezo. Alihukumiwa kwa kanuni zilizokuwa zikitawala soka wakati ule. Baada ya kulalamika kupitia kanuni hizohizo (ndio maana hakuenda Mahkamani), kanuni zile zikabatilika na amefanikiwa kushinda kupitia kanuni mbadala. Waliyomziwia wakati ule walikuwa wakitafsiri kanuni za wakati ule. Hawakumkosea yeyote. Kwa hivyo anachotakiwa kufanya ni kusahau, siuo kusamehe. Hata kwa Wambura,kukaimishwa nafasi hiyo sio lazima awe amesamehewa kwa tafsiri potofu ya neno hilo. Pengine ndio njama ya kumtafutia anguko kubwa zaidi. Kama asali inatosha kuua mtu, ya nini kumpa sumu? Viongozi wa TFT aliyoikuta wabaki au wasibaki, lililo sahihi kwa Malinzi ni kusahau. Sio kusamehe kwa sababu ni dhana inyo sahihi. Hajakosewa.
Mimi nimegundua kwamba wewe ni miongoni mwa wanaoendekeza usultani, maana unataka kila mmoja awe na mawazo sawa na yako, ambayo ni sawa na ya huyo Malinzi wako.Mimi nimegundua kuwa wewe ni mmoja wa viongozi wa FFT (Football Fitna of Tanzania) walioachwa na Tenga umeogopa sana unadhani unaweza kujiokoa through kumshawishi Malinzi kwa kuwa ni Jamii forum
Jino kwa jino, undava undava, ukenge ukenge na ng'ato gi ng'ato; mwendo mdundo, Malinzi kanyaga twende!
Nimeipenda zaidi hii mkuu,Ng'ato gi ng'ato!!,hii huwa inatumiwa katika hatua za mwisho kabisa na ukishasikia imetamkwa ujuwe hakuna msalie mtume tena hapo,jua kimechafuka,na kinachafuka kweli!