UFISADI TFF: Bil 1.1 zachotwa ndani ya wiki 1, PCCB washikwa na kigugumizi kumpeleka Malinzi Kortini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Ufisadi TFF, zaidi ya bil 1.1 zachotwa ndani ya wiki moja, Nani anamlinda Malinzi nyuma ya pazia? na PCCB wanaogopa kumpandisha kizimbani Bwana Malinzi kwasababu gani ikiwa uchunguzi wameshakamilisha?

Ndugu zangu wanaJF, Maafisa wa Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa PCCB makao makuu wamekamailisha uchunguzi dhidi ya pesa zilizochotwa katika akaunti ya TFF ndani ya wiki moja zaidi ya TZS bil 1 za kitanzania mwezi Agosti 2016.

Aidha PCCB ilishawahoji Jamal Malinzi rais wa TFF, Mwesigwa Selestine katibu mkuu wa TFF zaidi ya mara nne kutaka maelezo juu ya pesa hizo zilitolewa katika akaunti ya shirikisho na kwenda kusikojulikana. Inasemekana fedha hizo zimetumika kwenye kampeni za chaguzi za mikoa kuelekea uchaguzi mkuu wa TFF mwaka huu 2017.

Naomba ifahamike kuwa Shirikisho la mpira wa miguu(TFF) walipokea fedha hizo kutoka FIFA kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu nchini hususani vijana na wanawae, lakini katika hali ya kushangaza zimechukuliwa kwa matumizi binfasi ya wakuu wa taasisi hiyo bila kufuata taratibu za kikatiba zinazoliongoza shirikisho hilo.

Inasemekana kati ya Julai – Agosti pesa zaidi ya bil 1.2 zilichotwa katika akaunti ya TFF, baada ya Malinzi na Mwesigwa kufoji muhtasari na sahihi za wajumbe wa Utendaji kwenda benki ukionyesha kuwa wametoa baraka ya kubadilisha anayesaini hundi za malipo(signatory) za taasisi hiyo.

Hata hivyo kabla ya kuchota pesa hizo Bwana Malinzi alimuagiza ndugu Mwesigwa kumuandikia barua ya kwenda likizo kwa lazima aliyekua mkurugenzi wa fedha TFF, Edgar Masoud kisha kumuajiri binti anayeitwa Nsia na kumkabidhi nafasi ya kusaini hundi za malipo, ambapo ndani ya wiki moja waliweza kuchota dola za kimarekani 425,000 (sawa na mil 910,000,000 za kitanzania) bila ridhaa ya kamati ya utendaji.

Hata Edgar aliporejea ofisi baadaya likizo yake kumalizika katikati ya mwezi Agosti, alipewa barua ya kuachishwa kazi ndani ya mwezi huo huo, Edgar alifungua kesi ya madai dhidi ya TFF kuvunja mkataba wake inayotarajiwa kutolewa hukumu mwezi Februari mwishoni.

Aidha Malinzi alitoa maelekezo ya kulipwa kiasi cha milioni 70 za kitanzania swahiba wake kwa Michael Wambura, ambaye deni lake dhidi ya TFF lilishafutwa tangu enzi za utawala wa Leodgar Tenga, baada ya kamati ya utendaji wakati huo kukataa madai hayo na kufikiwa muafaka wa kutolipwa.

PCCB imeshakamilisha kuwahoji wajumbe wote wa kamati ya Utendaji wanaoishi Dar es salaam ambao ni Ayoub Nyenzi, Wilfred Kidao, Georfey Nyange ‘Kaburu’, Ahmed Mgoyi, Ramdhan Nassib na makamu wa Rais TFF Wallace Karia waliotoa ushahidi dhidi ya malipo hayo kufanyika pasipo idhini ya kikao ya Kamati ya Utendaji.

Katika sakata hilin wengine walioitwa kutoa ushahidi kutoka Sekretatiat ya TFF ni Daniel Msangi (Kaimu Mkurugenzi wa Fedha), Jonas Kiwia (Mkurugenzi wa mashindano), Salum Madadi (Mkurugenzi wa Ufundi), Hellen Adam (Mlipaji), Boniface Wambura (Afisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi).

Katika hali ya kushangaza, Malinzi amekua akilia kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye kupitia msaidizi wake Juma Matandika (anayetoka sehemu moja na waziri mkuu – Ruangwa, lakini pia ndio mwenye kesi na PCCB ya kuomba rushwa Geita Gold mil 25 ili timu yao ipande daraja) kuwa watu wa mpira wanamuonea wivu, kitu kinachoonyesha kama PCCB kushikwa na kigagaziko kuwapandisha kizimbani Malinzi pamoja na Mwesigwa.

> Malinzi na Mwesigwa wanatakiwa kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi, kufoji muhtasari wa kikao na sahihi za wajumbe wa kamati ya utendaji na kupeleka benki jina la Nsia, kisha kuchota fedha hizo zaidi ya bil 1 kwa matumizi yao binafsi ya kampeni za chaguzi za mikoa bila idhini ya Kamati ya Utendaji.

Ndugu zetu mliopewa dhama PCCB chonde chonde acheni kumtazama nyani usoni, mna vielelezo vyote kuhusu kuchotwa kwa fedha hizo, muhtasari uliofojiwa pamoja na sahihi za wajumbe, ila mbona hamuwafikishi kizimbani wahusika?

Naomba kuwasilisha.....
 
Huyo Jonas Kiwia ni yule aliekuwa akiishi Washngton DC,ndio kaamua kuja kujichafua kwenye soka la Bongo?
 
Hata tetemeko likiwakuta na serikali kuwakejeli hawachukiagia hawa kwa maana wanajua wanapoizabulia makofi hii sirikali.
H ahaa ha aha aha ahaa so unamaanisha wanalipiza na kupooza machungu.
 
Hata tetemeko likiwakuta na serikali kuwakejeli hawachukiagia hawa kwa maana wanajua wanapoizabulia makofi hii sirikali.
Hahaha yani wakishapiga waliopigwa wanabaki kubishana wenyewe kama wamepigwa au hawajapigwa.
Hatukawii kusikia je pesa bilion moja 1.2 zilizohamishwa zilikiwa za TFF au za Mali nzi?
Report PCCB inasema kwamba zilikuwa za malinza na bla bla nyingi kama kipindi cha bunge na sakata na escrow wengine wanazikana kwamba siyo za kwao wengine wanazikubari
 
Jamaa wa PCCB unaambiwa wamepata Kigugumizi kumfikisha Mkuluwa TFF Mahakamani kwasababu ataupoteza Urais na siajabu huko PCCB zishatembea noti za kutosha
 
Chezea nchomile weye???
Hahaha yani wakishapiga waliopigwa wanabaki kubishana wenyewe kama wamepigwa au hawajapigwa.
Hatukawii kusikia je pesa bilion moja 1.2 zilizohamishwa zilikiwa za TFF au za Mali nzi?
Report PCCB inasema kwamba zilikuwa za malinza na bla bla nyingi kama kipindi cha bunge na sakata na escrow wengine wanazikana kwamba siyo za kwao wengine wanazikubari
 
TFF UCHAFU HAUISHAGI HUKO....NGPJA TUWALETEE MAKONDA HUKO HEHEHE

OVA
 
Malinzi ni mjanja mjanja aliyepata dhamana ha kuongoza mpira wa miguu nchi hii.. AzamTv wanalalamika fedha za FA Cup waliyoa zote mil 500, cha ajabu akaelekeza zikasaidie chaguzi za mikoa na kuacha vilabu vinavyoshiriki michuano hiyo vikijtoa wengine kupewa laki 7 badala ya mil 3 walizokubaliana na wadhamini kwa kila timu.
 
Kumbe huyu mkuu wa soka anamadudu mengi eeeeh?
 
Back
Top Bottom