RIPOTI MAALUM Ufisadi wa kutisha TFF-4

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,124
RIPOTI MAALUM Ufisadi wa kutisha TFF-4
www.ippmedia.com/sw/habari/ripoti-maalum-ufisadi-wa-kutisha-tff-4

Pia ilielezwa changamoto ya ukosefu wa mwongozo wa utendaji na utoaji ajira uliosababisha hasara ya mamilioni ya shilingi na kuajiriwa kwa watu ambao hawana sifa stahiki, na wengine kupewa nyadhifa ambazo hazipo kwenye chati ya uongozi wa shirikisho.

Leo katika sehemu ya nne, ripoti hii inadokeza jinsi watendaji wa shirikisho walivyochota mabilioni ya shilingi kutoka kwenye akaunti ya fedha za udhamini wa timu ya taifa (Taifa Stars) na kuyatumia kwa shughuli nyingine kinyume cha taratibu na sheria za nchi.

Ripoti ya ukaguzi wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania kwa Taifa Stars iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inaelezwa kuwa, mbali na mambo mengine, TBL iliamua kufanya ukaguzi huo ili kujiridhisha kama shirikisho linazingatia makubaliano yaliyomo kwenye mkataba.

Inaelezwa katika ripoti hiyo ambayo uongozi wa juu wa TBL uliithibitishia Nipashe jana kwamba ilifanywa na Mkaguzi Mkuu wake wa ndani, Richard Magongo, kuwa kati ya Novemba 13, 2013 (siku 11 tangu uongozi wa sasa wa TFF uingie madarakani) na Februari 15, 2014, Dola za Marekani 315,577 (Sh. milioni 688.368) zilitumika bila ya nyaraka za kuthibitisha matumizi yake kinyume cha makubaliano ya mkataba wa pande hizo mbili.

Kati ya Novemba 11, 2013 na Machi 11, 2014, Dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni 831.616) pia zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF, ripoti inabainisha.

Mchanganuo wa ripoti hiyo unaonesha kuwa, miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia fedha hiyo ni pamoja na rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye Desemba 24, 2013 alilipwa Dola za Marekani 159 kupitia vocha yenye namba 1075 zikiwa ni gharama za malazi hotelini (Hotel accommodation).

Ripoti inaonesha kuwa, siku hiyo hiyo (Desemba 24, 2013), Malinzi alilipwa na TFF Dola 10,000 kupitia vocha namba 1077 (Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya fedha za Jamal Malinzi), kisha Februari 6, 2014 akalipwa Dola 15,934 (Loan Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya mkopo kutoka kwa Jamal Malinzi) na baadaye kulipwa Dola 69,471 kupitia vocha namba 1098 na Dola 63,735 kupitia vocha namba 1401.

Wengine waliopewa fedha hiyo ya udhamini wa TBL kwa Taifa Stars ni aliyekuwa msaidizi wa Malinzi, Juma Matandika, Ali Ruvu na mwingine aliyetajwa kwa jina la S. Madadi ambao kwa pamoja walilipwa Dola 1,084 kupitia vocha namba 828 Februari 6, 2014.

Ripoti pia inabainisha malipo ya Dola 3,500 Januari 16, 2014 kwa ajili ya ziara ya Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF jijini Nairobi.

Pia zimo Dola 4,630 zilizochotwa Desemba 24, 2013 kugharamia mtihani wa utimamu wa mwili kwa waamuzi (Cooper test for referees), Dola 4,120 zilizotolewa siku hiyo hiyo kwa ajili ya Ally Mayay na Ayubu Nyenzi kufanya ziara Uganda na Dola 1,638 ambazo zilitolewa siku hiyo hiyo zikiwa fidia ya malipo ya deni la TFF kulipia ziara ya uongozi wa shirikisho mkoani Mwanza.

Dola 4,023 zilitolewa Desemba 24, 2013 kwa ajili ya posho ya sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa wafanyakazi wa TFF na Dola 30,000 zilitumika kwa semina elekezi kwa makocha iliyofanyika Lushoto (coach retreat at Lushoto), ripoti inasema.

Inaongeza: "Dola 2,829 zilitumika kutoa rambirambi na misaada, Dola 3,298 zikakopeshwa kwa Chama cha Soka Mbeya huku Dola 989 zikitolewa kwa Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara zikiwa ni msaada."

Katika ripoti hiyo, inaelezwa kuwa, Dola 90,000 zilitumika kulipia fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wa aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen na Dola 34,177 zikatumika kununua magari mawili aina ya Toyota Hiace.

Ripoti inaeleza kuwa, kulikuwa na mawasiliano rasmi kati ya maofisa wa TFF na TBL kabla ya kufanya malipo kwa Poulsen na ununuzi wa magari hayo.

UTATA DOLA 174,177
Hata hivyo, inaelezwa katika ripoti hiyo kuwa, ukaguzi ulibaini malipo ya jumla ya Dola 174,177 (yakiwamo manunuzi ya magari hayo mawili), si tu kwamba yalikuwa kinyume cha mkataba wa makubaliano kati ya TFF na TBL, bali pia hakuna stakabadhi zozote za kuyathibitisha.

Ripoti hiyo inaonesha Kampuni ya Selous Commission Agent (T) Ltd ililipwa ma TFF Dola 34,177 Machi 11, 2014, ikiwa ni gharama ya manunuzi ya Toyota Hiace mbili.

Licha ya kulipiwa kiasi hicho cha na TFF, ripoti inaeleza kuwa, kadi ya usajili wa moja ya magari hayo ilikuwa chini ya Juma Sharif (wakati ukaguzi unafanyika mwaka 2014).

Aidha ukaguzi huo ulibaini kuwa Hiace nyingine ililipiwa ushuru wa stempu wa Sh. 20,000 hivyo kuonyesha wazi kuwa TFF ilidanganya thamani ya gari hilo."

"Hatukuyaona magari hayo wakati wa ukaguzi. Kibaya zaidi, hati za malipo za mzabuni aliyeteuliwa kuipatia magari hayo hazina namba za VRN na TIN. Magari hayo yana bima ndogo (third party)."

Ripoti hiyo pia inaonesha kuwa kampuni ya Executive Solution ililipwa jumla ya Dola 140,000 kwa kuipa hifadhi Taifa Stars badala ya gharama hizo kulipwa moja kwa moja kwenye hoteli husika.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Machi 13, 2014, Executive Solution walilipwa na TFF jumla ya Dola 55,000 kupitia hundi namba 35 (Dola 5,000) na namba 36 (Dola 50,000) kisha kulipwa Dola 35,000 Machi 28, 2014 na Dola 50,000 Aprili 14.

Pia inaelezwa katika ripoti hiyo kuwa, wakati Kifungu cha 3(7) cha mkataba wa makubaliano ya TFF na TBL kinalitaka shirikisho kuipa kampuni ripoti ya matumizi ya fedha za udhamini ya kila robo mwaka, ukaguzi ulibaini matumizi ya Dola 202,425 hayakuwamo kwenye ripoti ya fedha iliyotolewa na shirikisho kwenda kwa kampuni hiyo kwa ajili ya ukaguzi.

ITAENDELEA KESHO
 
Hivi hii TAKUKURU iko wapi? Kwa nini isifanye kazi kama ile ya FBI, FIFA? Kuna watu wanastahili kuwa Segerea lakini bado wapo mtaani.
Sishangai kuona soka la TZ limedidimia ghafla katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Malinzi aondoke na afunguliwe mashtaka
 
Kabisa Mkuu hapa kwetu haya majizi yanalindana. Huyu si ajabu kishajenga mtandao mkubwa wa kumlinda mpaka ndani ya CCM na Serikali. Hivyo yuko busy anapakua tu huku akikumbuka ule msemo maarufu, "Kizuri kula na wa kwenu/ndugu zako"
Wakati si milele kaka yana mwisho
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huwezi amini roho inaniuma kuona taasisi kubwa ya serikali inalipa kwa kutumia dola katika nchi ambayo tunaambiwa uchumi unakua.

Tukiacha hilo, sasa hawa jamaa hawajui kama siku hizi maisha yamebadilika?
Hawajui kama kuna kukaguana na kutenda kwa kadri ya mkataba unavyotaka?
Halafu unaibaje kitu ambacho hua kinafuatiliwa na itajulikana tu kama hiki kinaibwa?
Au ni basi tu kiburi?
Au ni ujinga basi?
Au ni kwa vile viongozi wetu ni k3?
Au ni umarioo maana kujilea kwa hela za mwenzako si mchezo.
 
Malinzi nahisi hana akili sawa, akataka hadi ahamie posta wakati tff ina ofisi zake Ilala, yaani jamaa alikua anataka awe mbali na TBL sijui alidhani akikaa mbali ndiyo hawatajua?
Au anawaonea aibu wakiwa karibu karibu haibi sana? Sasa tufanye angekua Posta si tungekuta anauza hadi vifaa vya ofisi?

Ah walinzi hua tunachoka akili mida hii, msinijudge sana.
 
Hakuna mwenye nia ya kupeleka soka letu mbele zaidi ya kujitajirisha..wanakuza vitambi tu..upigaji mwingine unakuja kwenye hii timu ya vijana..ngoja uone idadi ya maafisa watakaondoka kwenda Gabon utafikiri wanaenda cheza wao..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi hii TAKUKURU iko wapi? Kwa nini isifanye kazi kama ile ya FBI, FIFA? Kuna watu wanastahili kuwa Segerea lakini bado wapo mtaani.
Sishangai kuona soka la TZ limedidimia ghafla katika kipindi cha miaka minne iliyopita. Malinzi aondoke na afunguliwe mashtaka
Mkuu haya mashirkisho ya soka duniani kuanzia ngazi ya FIFA dunia mpaka ktk Ma Continents na mashirikisho ktk nchi mojamoja yamejiwekea taratibu na kanuni ngumu sana na hakika ni ngumu sana kwa taasisi nyingine hasa za kiusalama kuwaingilia ktk anga zao hata hao FBI walifanya kazi ya ziada kilisambaratisha genge la akina Sep Blatter, Platin, na akina Isa Ayatouh na mtandao wao waliokuwa kwa miongo kadhaa wanalalamikiwa na dunia nzima kwa ubadhirifu, rushwa na ufisadi uliokithiri. Amini usiamini haya mambo unayoyasoma ktk ripoti hii yapo tangu enzi za FAT ya akina Ndolanga, Michael Wambura, na akina Aden Rage. Panahitajika watu wenye strong determination kuwasambaratisha hawa jamaa ktk mtandao wao. Hapa panataka hata serikali ijitoe muhanga maana ukiwagusa tu utasikia Nchi inatengwa
 
Kuna mtu alishawahi kuleta ripoti kama hii humu,Malinzi alimponda sana na wengine humu eti wanamuonea wivu Malinzi kwe uchaguzi ujao.......haya na hii kanusheni sasa na huyo Malinzi wenu.
Nilishawahi kusema humu hakuna Kiongozi mmbaya amemfikia Malinzi kwe soka yaani huyu ni hovyo mpaka basi
 
Hii watakanusha bila shaka. Ila sioni pa kutokea hapo. Kama Rage alifungwa y not Malinzi. Mfumo wa michezo hasa soka ni genge la wezi tu na hawasemi. Haji Manara abarikiwe.
 
Huwezi amini roho inaniuma kuona taasisi kubwa ya serikali inalipa kwa kutumia dola katika nchi ambayo tunaambiwa uchumi unakua.

Tukiacha hilo, sasa hawa jamaa hawajui kama siku hizi maisha yamebadilika?
Hawajui kama kuna kukaguana na kutenda kwa kadri ya mkataba unavyotaka?
Halafu unaibaje kitu ambacho hua kinafuatiliwa na itajulikana tu kama hiki kinaibwa?
Au ni basi tu kiburi?
Au ni ujinga basi?
Au ni kwa vile viongozi wetu ni k3?
Au ni umarioo maana kujilea kwa hela za mwenzako si mchezo.
Brother, haya Mambo ya ufisadi ktk mashirikisho ya soka yanalalamikiwa sana hata na wadau na wahisani wakubwa wa soka duniani kv ADIDAS, PUMA, AON, COCACOLA, EMIRATES na makampuni mengine mengi yanayowekeza mamilioni ya dola ktk soka diniani kupitia FIFA yaani hii ni saratani.
 
Hii watakanusha bila shaka. Ila sioni pa kutokea hapo. Kama Rage alifungwa y not Malinzi. Mfumo wa michezo hasa soka ni genge la wezi tu na hawasemi. Haji Manara abarikiwe.
Wanaowakosoa wote lazima wapigwe pini,ukijiuliza kosa la Manara lilitakiwa kumfungia mwaka mzima? Hovyo Malinzi
 
Kuna vitu vingine ukivisoma humu jf unapandwa na hasira...

Hii nchi utadhani haina viongozi.... Hivi huyu jamaa si analipwa kwa kodi za wananchi?

Hivi kwanini wapenda soka tusiandamane kumshinikiza malinzi ajiuzulu? Maana maandamano hayata husiana na siasa... Malinzi anabaka soka la Tanzania......
 
Wewe mda wote unaleta mambo ya siasa za Chadema na CCM hivi huna vituvingine vya kuchangamsha ubongo wako? Wewe unashangaa mambo wanayofanya TFF ila kama Mbowe atafanyiwa uchunguzi wa matumizi ya Fedha za ruzuku ambazo ni kodi za wananchi, Wizi na utafunaji wake wa fedha hizo za ruzuku kwa muda aliokaa madarakani ni zaidi ya wizi unaofanywa na TFF.
 
Back
Top Bottom