Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Uyu mama bila kusimamiwa au kukemewa anaharibu utumishi eti umesitisha kupanda madaraja sababu ya uhakiki
Matatizo ya akili yako ndogo. Ukipandisha madaraja na mishahara ya watumishi wakati bado kuna watumishi hewa na wasio na sifa stahiki aka vyeti feki unajua implication Yake? Nadhani kuna umuhimu wa wachungaji wa humu jf kuwa wanachukua muda kutafakari kabla ya kupost maana kuna watu kibao humu wanakurupukia hoja wasiziokuwa na uelewa nazo
 
Mama kakosa cha kusema ama ndio kiki kwa mukulu? Mwalimu wa sayansi na hesabu hawezi kusota mda wrote huu anasubiri ajira,weng wako private na maisha yanaenda,utawatafuta sana hao 8,000 na huwapat na endelea kuongeza idadi ya visingizio utashinda
Cheti cha kufoji kinazuia nini watu wengine kupandishwa vyeo, kwa matamko kama haya asitegemee ufaulu wowote kuongezeka.
 
Kwa taarifa yako sijaajiriwa popote na vyeti vyangu vyote original sina hata pressure yoyote.
Tatizo huyo mama kakomalia uhakiki halafu hationi ukiisha wala advantage ya huo uhakiki zaidi tu ya kuzidi kuchelewesha stahiki za watumishi wa umma.
Uhakiki gani mwaka mzima.
Watumishi 560,000 na kwa technology hii si hawa unawahikiki ndani ya siku moja!, mbona kura tulipiga siku moja zaidi ya watu 14,000,000? tena watu wasio na ulewa wengi wa BVR. Tuache sanaa Watanzania
 
Da fatu vipi una cheti feki nini? Kama huna cheti feki au si kanjanja huko uliko huwezi kerwa na utaratibu wa kuwasaka makanjanja waliokuwa wanafanya kusoma kudharaulike. Zoezi likikamilika ajila zitamwagwa na wote wenye vyeti sahihi walioenda Shule watapatiwa ajila na watafurahia sana.
Wanakera na uhakiki usioisha.
Sina vyeti fake.
 
Waziri anzia kwenye Bunge,tumbua wabunge wenye sifa fake.Nenda pia Mahakamani utapata kujiridhisha juu ya utata wa kutoa haki.Kagua vyombo vya usalama pia,bila hivyo hautamaliza sifa fake.
 
Umesema kweli ndugu yangu! Kuna mkufunzi mwezetu hapa chuo cha ualimu morogoro mjini. cheti chake cha kidato cha nne amemupa ndugu yake anakitumia arusha! hivyo basi wahakiki wapite huku. anaitwa Neema huyo mkufunzi.
Hakukuwa na sababu ya kutaja jina
 
Walimu zaidi ya 5000 waingia mitini

Takwimu hiyo imetajwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Angela Kairuki wakati akizungumza na watumishi wa umma wanawake katika Manispaa ya Dodoma katika wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kairuki alikuwa akizungumzia suala la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, na kusisitiza kuwa ifikapo mwezi Machi mwaka huu watumishi wote wa umma ambao watakuwa hawajawasilisha vyeti vyao vya kitaaluma watafukuzwa kazi.

Amebainisha kuwa katika zoezi lililofanywa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (Nida) waligundua watumishi wengi hawana vyeti na baadhi yao wanatumia vyeti feki hasa wa kada ya ualimu kwa kuwa wana uhakika wa ajira pindi wanapomaliza vyuo.

"Kulikuwa na taarifa kuwa kuna zaidi ya walimu 8,000 waliokuwa wanatakiwa kuajiriwa lakini baada ya serikali kutangaza nafasi hiyo ni walimu 2,100 tuu ndiyo walioomba nafasi mpaka sasa. Sasa hapo suala la kujiuliza je hao wengine mpaka sasa wako wapi kama hawana vyeti feki!? Nataka niwaambie kuwa hakuna mwenye cheti feki atakayesalimika kwenye Utumishi wa umma," amesema Kairuki.

Amesema ni bora aonekane ni waziri anayechukiwa na jamii kuliko kulifumbia macho suala la vyeti feki kwa watumishi wa umma.

"Tumetoa muda wa kutosha kwa watumishi wa umma kuwasilisha vyeti vyao vya kitaaluma bila shaka walifika mpaka hapa kwenu lakini jambo la kusikitisha ni kwamba mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi bado hawajawasilisha," alisema Kairuki.....Vyeti hawajaleta na hata namba ya utambulisho (index number) hawaleta sasa wanataka tuwafanyaje??? Nawamegemea tu siri na mkawaambie na wenzenu itakapofika Machi Mosi hawajawasilisha vyeti vyao tunawafukuza kazi."

Amesema kama serikali itaharakisha zoezi hilo watumishi wa umma wanaostahili watapandishwa vyeo na mishahara yao kwa kuwa zoezi hilo limesitishwa kutokana na uhakiki wa vyeti.
Vyeti feki ni jipu BORA WATUMBULIWE
 
Huyu naye akatiki kwenye media kwa swala moja , mbona hatuambii kuhusu shule kufanya vibaya sababu ni nini?
 
Huyu mama ni mnafiki kam wanafiki wengine
 
Pole sana ndugu. Hizo ajira zilitoka December kwa walimu wa sayansi na hesabu tu. Bahati mbaya idadi haijatimia.
Asante ndugu yangu....wacha tuendelee kumsikiiza Mungu maana yeye hajawahi kushindwa kwenye maisha yetu
 
Asante ndugu yangu....wacha tuendelee kumsikiiza Mungu maana yeye hajawahi kushindwa kwenye maisha yetu
Usiwe na wasiwasi, mambo yatakaa Sawa. Kila lililo na mwanzo.......
 
Umesema kweli ndugu yangu! Kuna mkufunzi mwezetu hapa chuo cha ualimu morogoro mjini. cheti chake cha kidato cha nne amemupa ndugu yake anakitumia
arusha! hivyo basi wahakiki wapite huku. anaitwa Neema huyo mkufunzi.

Acha zako wewe
 
hakuna watu wanafanya kazi katika mazingira magumu kama walimu mfano walimu wa shule ya makanjiro kwa pm wilaya ya ruangwa kuna walimu wameacha kazi kwa sababu ya ushirikina kike kijiji mwalimu wa kike haruhusiwi kuzaa akipata mimba inatoka wazee wa kijiji walishasema ni mali yao wao ndo waamuzi
 
Back
Top Bottom