Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Hii sirikali inatia kichefuchefu sana. Simlaumu huyu mama, yeye ametumwa tu na bosi wake, huu ni mkakati maalum, uhakiki gani unachukua mwaka mzima na hauishi.

Hii ni dhuluma ya wazi kwa watumishi, kuwanyima stahili zao zilizopo kisheria kwa visingizio vya hovyo.

Mungu wa Mbinguni anawaona hakika!!
 
Huyu shemeji sasa tumekuchoka,sasa kama kuna mtu hajaleta cheti wakati wa uhakiki kwanini usimtoe kazini na ubakize wale cream?.Usitufanye watumishi kama ngazi ya kupandia kwenye cheo chako.poor waziri.
 
Umesema kweli ndugu yangu! Kuna mkufunzi mwezetu hapa chuo cha ualimu morogoro mjini. cheti chake cha kidato cha nne amemupa ndugu yake anakitumia arusha! hivyo basi wahakiki wapite huku. anaitwa Neema huyo mkufunzi.
Punguza unoko wewe....
 
Wanavyozidi kichelewesha hata kati ya hao 2,100 walioomba wataripoti hata 500.
 
Kwa stahili hii watoto watafeli sana maana hakuna anayefanya kazi kwa moyo na huku anadharauliwa na muajiri wake namna hii,uhakiki gani ambao hakuna MWISHO?.
 
Kazini kwangu naangalia zaidi uwezo wa kufanya kazi na siyo vyeti. Maana nakulipa kutokana na kile unachokizalishia kampuni, siyo kwa idadi ya makaratasi uliyo nayo au miaka uliyokaa darasani.

Ninachotegemea ni kuwa anayesema amesoma vizuri au ana ufaulu wa juu, atende kazi kuwazidi wenye elimu ndogo na wale ambao hawakufaulu kwa viwango vya juu katika masomo yao.
 
What if wameelekea private?hypothesis haijakaa poa hata kidogo
 
Baliniambianga njia ya mwongo ni fupi . ,mwezi wa tatu ni kesho tuu maana almost zimebak cku 26 tuu kufika machi mosi....hizo Ajira na kupanda vyeo twasubir kwahamu...
Usishangae huyu mama akaja na kisingizio kingine
 
Walimu zaidi ya 5000 waingia mitini

Takwimu hiyo imetajwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Angela Kairuki wakati akizungumza na watumishi wa umma wanawake katika Manispaa ya Dodoma katika wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kairuki alikuwa akizungumzia suala la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, na kusisitiza kuwa ifikapo mwezi Machi mwaka huu watumishi wote wa umma ambao watakuwa hawajawasilisha vyeti vyao vya kitaaluma watafukuzwa kazi.

Amebainisha kuwa katika zoezi lililofanywa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (Nida) waligundua watumishi wengi hawana vyeti na baadhi yao wanatumia vyeti feki hasa wa kada ya ualimu kwa kuwa wana uhakika wa ajira pindi wanapomaliza vyuo.

"Kulikuwa na taarifa kuwa kuna zaidi ya walimu 8,000 waliokuwa wanatakiwa kuajiriwa lakini baada ya serikali kutangaza nafasi hiyo ni walimu 2,100 tuu ndiyo walioomba nafasi mpaka sasa. Sasa hapo suala la kujiuliza je hao wengine mpaka sasa wako wapi kama hawana vyeti feki!? Nataka niwaambie kuwa hakuna mwenye cheti feki atakayesalimika kwenye Utumishi wa umma," amesema Kairuki.

Amesema ni bora aonekane ni waziri anayechukiwa na jamii kuliko kulifumbia macho suala la vyeti feki kwa watumishi wa umma.

"Tumetoa muda wa kutosha kwa watumishi wa umma kuwasilisha vyeti vyao vya kitaaluma bila shaka walifika mpaka hapa kwenu lakini jambo la kusikitisha ni kwamba mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi bado hawajawasilisha," alisema Kairuki.....Vyeti hawajaleta na hata namba ya utambulisho (index number) hawaleta sasa wanataka tuwafanyaje??? Nawamegemea tu siri na mkawaambie na wenzenu itakapofika Machi Mosi hawajawasilisha vyeti vyao tunawafukuza kazi."

Amesema kama serikali itaharakisha zoezi hilo watumishi wa umma wanaostahili watapandishwa vyeo na mishahara yao kwa kuwa zoezi hilo limesitishwa kutokana na uhakiki wa vyeti.
Kazi nzuri. Lakini pia akumbuke kuwa muda ni mwalimu pia. Mwez March siyo mbali.
 
Umesema kweli ndugu yangu! Kuna mkufunzi mwezetu hapa chuo cha ualimu morogoro mjini. cheti chake cha kidato cha nne amemupa ndugu yake anakitumia arusha! hivyo basi wahakiki wapite huku. anaitwa Neema huyo mkufunzi.
Duuh, we ni noma.
 
Huyu mama angejua tumechoka kusikiliza hizo habari za uhakiki kila siku angekaa tu kimya azungumzie mambo mengine.
Hivi hiyo wizara yake haina au hakuna mambo mengine ya kufanya zaidi ya uhakiki?
Hili swala lishakuwa kero basi tu tunavumiliana.
Hakuna kazi zingine ni bora tuonekane kwenye media kidogo kuwa tunafanya kazi.
 
Kwa maneno haya ya Kairuki ya uhakiki kila cku wala simlaumu yeye hata kidogo maana ndiyo maagizo aliyopewa kuwa akomalie uhakiki ili wajaribu kukusanya fedha za kuajiria watu ahadi wanazotoa kuwa kila baada ya miezi miwili watamaliza uhakiki ni kwa sababu wanadhani huenda ndani ya muda huo watakuwa wamepata fedha wanajikuta bado hivyo wanazidisha danadana
 
Wewe utakuwa na cheti fake. Kwa sisi tuliokesha tunasoma, tulikesha tunawaza kufaulu, tuliugua pressure ili tufaulu, halafu wengine waje wafoji na tuwe nao ofisi moja, yaani haingii akilini, wafukuzwe wote kabisa, sitaki kusikia cheti fake ofisini kwangu.
Kwa taarifa yako sijaajiriwa popote na vyeti vyangu vyote original sina hata pressure yoyote.
Tatizo huyo mama kakomalia uhakiki halafu hationi ukiisha wala advantage ya huo uhakiki zaidi tu ya kuzidi kuchelewesha stahiki za watumishi wa umma.
Uhakiki gani mwaka mzima.
 
Back
Top Bottom