Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Askari Muoga

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
6,112
Reaction score
4,663
Walimu zaidi ya 5000 waingia mitini

Takwimu hiyo imetajwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Angela Kairuki wakati akizungumza na watumishi wa umma wanawake katika Manispaa ya Dodoma katika wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kairuki alikuwa akizungumzia suala la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, na kusisitiza kuwa ifikapo mwezi Machi mwaka huu watumishi wote wa umma ambao watakuwa hawajawasilisha vyeti vyao vya kitaaluma watafukuzwa kazi.

Amebainisha kuwa katika zoezi lililofanywa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (Nida) waligundua watumishi wengi hawana vyeti na baadhi yao wanatumia vyeti feki hasa wa kada ya ualimu kwa kuwa wana uhakika wa ajira pindi wanapomaliza vyuo.

"Kulikuwa na taarifa kuwa kuna zaidi ya walimu 8,000 waliokuwa wanatakiwa kuajiriwa lakini baada ya serikali kutangaza nafasi hiyo ni walimu 2,100 tuu ndiyo walioomba nafasi mpaka sasa. Sasa hapo suala la kujiuliza je hao wengine mpaka sasa wako wapi kama hawana vyeti feki!? Nataka niwaambie kuwa hakuna mwenye cheti feki atakayesalimika kwenye Utumishi wa umma," amesema Kairuki.

Amesema ni bora aonekane ni waziri anayechukiwa na jamii kuliko kulifumbia macho suala la vyeti feki kwa watumishi wa umma.

"Tumetoa muda wa kutosha kwa watumishi wa umma kuwasilisha vyeti vyao vya kitaaluma bila shaka walifika mpaka hapa kwenu lakini jambo la kusikitisha ni kwamba mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi bado hawajawasilisha," alisema Kairuki.....Vyeti hawajaleta na hata namba ya utambulisho (index number) hawaleta sasa wanataka tuwafanyaje??? Nawamegemea tu siri na mkawaambie na wenzenu itakapofika Machi Mosi hawajawasilisha vyeti vyao tunawafukuza kazi."

Amesema kama serikali itaharakisha zoezi hilo watumishi wa umma wanaostahili watapandishwa vyeo na mishahara yao kwa kuwa zoezi hilo limesitishwa kutokana na uhakiki wa vyeti.
 
Waalimu wengi wana vyeti vya kidato cha nne na sita ambavyo siyo vyao au feki ndiyo maana hawaombi kazi licha ya serikali kutangaza nafasi hizo! Kudos Waziri Kairuki, kudos President Magufuli.
 
Huyu mama angejua tumechoka kusikiliza hizo habari za uhakiki kila siku angekaa tu kimya azungumzie mambo mengine.
Hivi hiyo wizara yake haina au hakuna mambo mengine ya kufanya zaidi ya uhakiki?
Hili swala lishakuwa kero basi tu tunavumiliana.
 
Baliniambianga njia ya mwongo ni fupi . ,mwezi wa tatu ni kesho tuu maana almost zimebak cku 26 tuu kufika machi mosi....hizo Ajira na kupanda vyeo twasubir kwahamu...
 
uyu mama anajifanya mjuaji ili ni tatizo la kuchagua viongozi walio toka maisha bora mama Angela kairuki
 
Waalimu wengi wana vyeti vya kidato cha nne na sita ambavyo siyo vyao au feki ndiyo maana hawaombi kazi licha ya serikali kutangaza nafasi hizo! Kudos Waziri Kairuki, kudos President Magufuli.
Umesema kweli ndugu yangu! Kuna mkufunzi mwezetu hapa chuo cha ualimu morogoro mjini. cheti chake cha kidato cha nne amemupa ndugu yake anakitumia arusha! hivyo basi wahakiki wapite huku. anaitwa Neema huyo mkufunzi.
 
Huo ni umbea wa tetesi tu na wewe unaonekana una chuki na huyo neema na umeamua kumdhalilisha humu maana hata andika yako inonesha kiwango chako cha elimu ni kidogo sana
 
Habari nyingine ni kero tu hivi we we Tanzania umeona tatizo kubwa ni vyeti feki huna ishu nyingine au njoo unikamate na Mimi mwenye cheti feki
 
Habari nyingine ni kero tu hivi we we Tanzania umeona tatizo kubwa ni vyeti feki huna ishu nyingine au njoo unikamate na Mimi mwenye cheti feki
huyu mama ajielewe sasa halikuwa Ana hakiki nini
 
Back
Top Bottom