Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Walimu zaidi ya 5000 waingia mitini

Takwimu hiyo imetajwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Angela Kairuki wakati akizungumza na watumishi wa umma wanawake katika Manispaa ya Dodoma katika wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kairuki alikuwa akizungumzia suala la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, na kusisitiza kuwa ifikapo mwezi Machi mwaka huu watumishi wote wa umma ambao watakuwa hawajawasilisha vyeti vyao vya kitaaluma watafukuzwa kazi.

Amebainisha kuwa katika zoezi lililofanywa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (Nida) waligundua watumishi wengi hawana vyeti na baadhi yao wanatumia vyeti feki hasa wa kada ya ualimu kwa kuwa wana uhakika wa ajira pindi wanapomaliza vyuo.

"Kulikuwa na taarifa kuwa kuna zaidi ya walimu 8,000 waliokuwa wanatakiwa kuajiriwa lakini baada ya serikali kutangaza nafasi hiyo ni walimu 2,100 tuu ndiyo walioomba nafasi mpaka sasa. Sasa hapo suala la kujiuliza je hao wengine mpaka sasa wako wapi kama hawana vyeti feki!? Nataka niwaambie kuwa hakuna mwenye cheti feki atakayesalimika kwenye Utumishi wa umma," amesema Kairuki.

Amesema ni bora aonekane ni waziri anayechukiwa na jamii kuliko kulifumbia macho suala la vyeti feki kwa watumishi wa umma.

"Tumetoa muda wa kutosha kwa watumishi wa umma kuwasilisha vyeti vyao vya kitaaluma bila shaka walifika mpaka hapa kwenu lakini jambo la kusikitisha ni kwamba mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi bado hawajawasilisha," alisema Kairuki.....Vyeti hawajaleta na hata namba ya utambulisho (index number) hawaleta sasa wanataka tuwafanyaje??? Nawamegemea tu siri na mkawaambie na wenzenu itakapofika Machi Mosi hawajawasilisha vyeti vyao tunawafukuza kazi."

Amesema kama serikali itaharakisha zoezi hilo watumishi wa umma wanaostahili watapandishwa vyeo na mishahara yao kwa kuwa zoezi hilo limesitishwa kutokana na uhakiki wa vyeti.


Usikute hawa wote (walimu feki) walishamiri enzi za utawala wa Kikwete. Yule bwana alitenda majanga mengi sana hapa Tanzania na ndiyo maana aliwaambia watanzania kuwa mtanikumbuka maana alijuwa rais atakayekuja hataweza kuendekeza upuuzi alioufuga yeye. Sasa naelewa kwa nini watanzania wengi wanalia huku mitaani na kumkumbuka Kikwete.
 
Kwani hizo ajira za walimu walizitangaza lini? Na ukitaka kuomba unapitishia wapi TAMISEMI MAKAO MAKUU AU UTUMISHI DAR? Nifungueni jamani plz!
 
Kwani hizo ajira za walimu walizitangaza lini? Na ukitaka kuomba unapitishia wapi TAMISEMI MAKAO MAKUU AU UTUMISHI DAR? Nifungueni jamani plz!
waliambiwa watume vyeti tu
 
Mama kakosa cha kusema ama ndio kiki kwa mukulu? Mwalimu wa sayansi na hesabu hawezi kusota mda wrote huu anasubiri ajira,weng wako private na maisha yanaenda,utawatafuta sana hao 8,000 na huwapat na endelea kuongeza idadi ya visingizio utashinda
 
Ni muda sasa tangu zoezi la uhakiki lianze, wangi wamenyimwa haki zao za msingi kwa kisingizio cha uhakiki. Hali hiyo inakatisha tamaa kwa watumishi wawajibikaji.,Serikali iwape watumishi stahiki zao na kutafuta njia mbadala na sahihi ya kupambana na watumishi hewa la sivyo huu wimbo utakuwa wa kila siku.
 
Umesema kweli ndugu yangu! Kuna mkufunzi mwezetu hapa chuo cha ualimu morogoro mjini. cheti chake cha kidato cha nne amemupa ndugu yake anakitumia arusha! hivyo basi wahakiki wapite huku. anaitwa Neema huyo mkufunzi.
Maneno yako yana viemelea vya uchochezi
 
uyu mama anajifanya mjuaji ili ni tatizo la kuchagua viongozi walio toka maisha bora mama Angela kairuki
Kweli ukiwa maskini hadi akili nazo Zinakuwa za kimaskiniskini tu. Kuna uhusiano gani wa utendaji bora wa kazi na umaskini? Utendaji kazi bora hautegemei unatoka kundi gani bali ni commitment ya mtu binafsi na sheria na taratibu za nchi husikia ndio zinazodetermine performance ya kiongozi hasa wa umma. Viongozi wangapi waliotokea kwenye familia maskini lakini ndio wamegeuka miungu watu utadhani hata hawajawahi kuwa maskini katika maisha yao yote!
 
Tuacheni siasa,na wale waliorekebishiwa mishahara na baadae kurejeshwa kwenye madaraja ya awali watarajie nini?
Kimsingi sioni uhusiano wa wao na uhakiki sana sana HEWA WA KUNDI HILO WANGENG'OKA KWA NJIA ILE ILE(huku wakiwa kwenye madaraja mapya).
 
Habari nyingine ni kero tu hivi we we Tanzania umeona tatizo kubwa ni vyeti feki huna ishu nyingine au njoo unikamate na Mimi mwenye cheti feki
Sisi Waafrika tunabehave kama watoto hatujui tunachotaka maishani. Mojawapo ya kero kubwa katika utumishi wa umma ilikuwa ni watumishi hewa na watumishi wasiyo na shifa za nyadhifa zao. Hata waheshimiwa wabunge wamekuwa wakilongelea sana hili suala kwa miaka mingi. Sasa serikali imechukua hatua nzuri ya kuondoa watumishi hewa na wasio na sifa zinazohitajika mnaanza kulaumu tena. Sasa mlitaka waache tu au wafanyenje? Ndugu kama ni ajira zitakuja tuu tuwe wavumilivu na kama ni mshahara utapanda tu lakini kumbuka mshahara pekee haukufanyi uwe millionnare au billionare
 
Mkuu ulimwomba akakunyima?? Hili suala limekaa kama lina wivu was kimapenzi ndani yake.
 
Kwani hizo ajira za walimu walizitangaza lini? Na ukitaka kuomba unapitishia wapi TAMISEMI MAKAO MAKUU AU UTUMISHI DAR? Nifungueni jamani plz!
Pole sana ndugu. Hizo ajira zilitoka December kwa walimu wa sayansi na hesabu tu. Bahati mbaya idadi haijatimia.
 
lakini kuna point,kama watu hawajatuma maombi maana yake nini??? watu wana vyeti feki sehemu nyingi sana....vyombo vya usalama ndo kaabisaaaaaa
 
Aangaloe na upande mwingne wa shiling asifkirie kwmba walioacha kutuma maomb wan vyet fek laaah wengne wameamua kujiingza kwny mishe nyngne za maisha na wengne wameajiriwa na private sector baada ya kuona wameachwa zaid ya mwaka wako mtaan hopless sasa yy ajidanganye tu wameingia mitin kwa sababu nyepes anayoiwaza
 
Safi sana Mama, hao waliokimbia ni wahalifu na ndo kati ya waliochangia kutuharibia Elimu katika nchii hii..... Nakupongeza sana....Tufungue ukurasa mpya na ulio safi.....mwezi March....Inabidi usiishie hapo watafutwe popote walipo na wachukuliwe hatua stahiki
 
Umesema kweli ndugu yangu! Kuna mkufunzi mwezetu hapa chuo cha ualimu morogoro mjini. cheti chake cha kidato cha nne amemupa ndugu yake anakitumia arusha! hivyo basi wahakiki wapite huku. anaitwa Neema huyo mkufunzi.
Majungu tuu
 
Huyu mama angejua tumechoka kusikiliza hizo habari za uhakiki kila siku angekaa tu kimya azungumzie mambo mengine.
Hivi hiyo wizara yake haina au hakuna mambo mengine ya kufanya zaidi ya uhakiki?
Hili swala lishakuwa kero basi tu tunavumiliana.
Wenyewe wanaita porojo.
 
huyu mama ajielewe sasa halikuwa Ana hakiki nini
hakika alieshiba amtambui mwenye njaa. na pia selikali ya Tanzania no wababa ishaji amuwezi waambia watu kua zoezi litachukia miezi miwili alafu lichukue miezi zaidi ya sita apo mlikurupuka.
 
Back
Top Bottom