Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Kama unajua sifa za fisi alie shiba udi doubt..
Fisi alie shiba hata akiona mzoga anaweza usiufuate akalala na kucheza cheza au akaenda kuuma na kuchezea kwa kuuburuta..

Sasa subiri hitaji la walimu lionekana ndio mtajua sasa!!
 
Hivi wanaokagua wenzao na wenyewe wanakaguliwaje?
 
Walimu zaidi ya 5000 waingia mitini

Takwimu hiyo imetajwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Angela Kairuki wakati akizungumza na watumishi wa umma wanawake katika Manispaa ya Dodoma katika wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kairuki alikuwa akizungumzia suala la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, na kusisitiza kuwa ifikapo mwezi Machi mwaka huu watumishi wote wa umma ambao watakuwa hawajawasilisha vyeti vyao vya kitaaluma watafukuzwa kazi.

Amebainisha kuwa katika zoezi lililofanywa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (Nida) waligundua watumishi wengi hawana vyeti na baadhi yao wanatumia vyeti feki hasa wa kada ya ualimu kwa kuwa wana uhakika wa ajira pindi wanapomaliza vyuo.

"Kulikuwa na taarifa kuwa kuna zaidi ya walimu 8,000 waliokuwa wanatakiwa kuajiriwa lakini baada ya serikali kutangaza nafasi hiyo ni walimu 2,100 tuu ndiyo walioomba nafasi mpaka sasa. Sasa hapo suala la kujiuliza je hao wengine mpaka sasa wako wapi kama hawana vyeti feki!? Nataka niwaambie kuwa hakuna mwenye cheti feki atakayesalimika kwenye Utumishi wa umma," amesema Kairuki.

Amesema ni bora aonekane ni waziri anayechukiwa na jamii kuliko kulifumbia macho suala la vyeti feki kwa watumishi wa umma.

"Tumetoa muda wa kutosha kwa watumishi wa umma kuwasilisha vyeti vyao vya kitaaluma bila shaka walifika mpaka hapa kwenu lakini jambo la kusikitisha ni kwamba mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi bado hawajawasilisha," alisema Kairuki.....Vyeti hawajaleta na hata namba ya utambulisho (index number) hawaleta sasa wanataka tuwafanyaje??? Nawamegemea tu siri na mkawaambie na wenzenu itakapofika Machi Mosi hawajawasilisha vyeti vyao tunawafukuza kazi."

Amesema kama serikali itaharakisha zoezi hilo watumishi wa umma wanaostahili watapandishwa vyeo na mishahara yao kwa kuwa zoezi hilo limesitishwa kutokana na uhakiki wa vyeti.
hoja hafifu!
kama ulitarajia watu 8000 waombe kazi kasha wakaja 2000, then conclusion yako ni kuwa hao wengine ni kwasababu ya vyeti feki ndio maana hawakuja kuomba kazi!
anasemaje kuhusu maslahi ya walimu? labda hawajawa motivated kwa kuwa malipo hayaridhishi!
vipi kuhusu kupanuka kwa soko la shule binafsi, labda wamekimbilia huko?
upatikanaji wa ajira kama network marketing ambayo huchukua watu wengi wenye taaluma za kati na mishahara kiduchu kama walimu?
vipi ktk hao 2100 ameajiri wangapi?
 
Nilisema hapo awali siasa ni upuuzi fulani, wanaotokwa na povu wengi kwa hotuba ya kairuki. Wengi wao walikuwa wanufaika wa hizo feki feki, hatutaraji leo wafurahie!
Pelekeni vyeti mkahakikiwe fullstop.
 
Vyeti feki ni issue Tz na baadhi ya watumishi wana hilo tatizo kiukweli.

Na wakati wa Kamanda Kova kuna watu walikamatwa watengenezaji maarufu wa vyetu mpaka vya Masters hapa Dar.

Na wengine walikamatwa Kigoma lakini sijawahi kusikia kesi zao Mahakamani.
 
Uyu mama bila kusimamiwa au kukemewa anaharibu utumishi eti umesitisha kupanda madaraja sababu ya uhakiki
 
Yeye na wizara yake ni jipu. Haiwezekan kazi anayojua ni uhakiki tu kwani hakuna shughuli nyingine ya kufanya. Mwaka sasa wizara ipo kwenye uhakiki tu imesahau kuboresha maslahi ya watumishi wa umma, mazingira ya kazi ni mabovu, hovyo sana n.k
 
Kero kero anajuaa suala la usalama wa nchi kufukuza walimu 8,000? Muda wote huo alikuwa anahakiki kitu gani?? Hana ajenda ingine......katika JD yake??
 
Hana dhamira ya dhati huyo mama,pia hatambui kama amekanyaga haki za watu wengi kwa kisinguzio cha uhakiki hewa , kila siku wimbo ni ule ule tu, bora akae kimya.
 
Huyu mama angejua tumechoka kusikiliza hizo habari za uhakiki kila siku angekaa tu kimya azungumzie mambo mengine.
Hivi hiyo wizara yake haina au hakuna mambo mengine ya kufanya zaidi ya uhakiki?
Hili swala lishakuwa kero basi tu tunavumiliana.
Da fatu vipi una cheti feki nini? Kama huna cheti feki au si kanjanja huko uliko huwezi kerwa na utaratibu wa kuwasaka makanjanja waliokuwa wanafanya kusoma kudharaulike. Zoezi likikamilika ajila zitamwagwa na wote wenye vyeti sahihi walioenda Shule watapatiwa ajila na watafurahia sana.
 
Kwa kazi anayofanya Waziri Kairuki kwa kuelekezwa na Rais Dr Magufuli, ukiona mtu yeyote analalama ujue kuwa yamempata either yeye mwenyewe au watoto wake au ndugu wa karibu wanatumia/wametumia vyeti feki kupata nafasi walizonazo! Mimi mwenyewe najua mwalimu mmoja kishafundisha zaidi ya miaka 25 lakini hawezi kusema sentenso hata mmoja iliyosahihi kwa lugha ya Kiingereza, just imagine mwalimu wa daraja la grade A ya enzi hizo kapata kazi hiyo kwa cheti fake au cha ndugu! hawezi kuwakilisha kwa uhakiki kwani atanaswa tu ndiyo maana ya waalimu elfu tano hawajathubuti kuwakilisha vyeti vyao! Kudos Kairuki, kudos Rais Magufuli.
 
Huyu mama angejua tumechoka kusikiliza hizo habari za uhakiki kila siku angekaa tu kimya azungumzie mambo mengine.
Hivi hiyo wizara yake haina au hakuna mambo mengine ya kufanya zaidi ya uhakiki?
Hili swala lishakuwa kero basi tu tunavumiliana.
Wewe utakuwa na cheti fake. Kwa sisi tuliokesha tunasoma, tulikesha tunawaza kufaulu, tuliugua pressure ili tufaulu, halafu wengine waje wafoji na tuwe nao ofisi moja, yaani haingii akilini, wafukuzwe wote kabisa, sitaki kusikia cheti fake ofisini kwangu.
 
Kwa kazi anayofanya Waziri Kairuki kwa kuelekezwa na Rais Dr Magufuli, ukiona mtu yeyote analalama ujue kuwa yamempata either yeye mwenyewe au watoto wake au ndugu wa karibu wanatumia/wametumia vyeti feki kupata nafasi walizonazo! Mimi mwenyewe najua mwalimu mmoja kishafundisha zaidi ya miaka 25 lakini hawezi kusema sentenso hata mmoja iliyosahihi kwa lugha ya Kiingereza, just imagine mwalimu wa daraja la grade A ya enzi hizo kapata kazi hiyo kwa cheti fake au cha ndugu! hawezi kuwakilisha kwa uhakiki kwani atanaswa tu ndiyo maana ya waalimu elfu tano hawajathubuti kuwakilisha vyeti vyao! Kudos Kairuki, kudos Rais Magufuli.
Kuna mwl mkuu alileta fuso usiku usiku akabeba vyake akatimuka, unachezea Dkt Magufuli wewe. Yaani elimu ilidharaulika kweli kweli, ila sasa lazima watie heshima.
 
Huenda yuko sahihi kwa upande mmoja, au pia asiwe sahihi hata kidogo.
Ila mimi naona kuwa tatizo la hao walimu 5000 kutojitokeza sio kwa sababu ya vyeti feki. Au labda watoe takwimu, tangu waanze kukagua vyeti feki wamepata vingapi??! Ili tuweze kufanya comparison.
Utaratibu wa utumaji wa vyeti ulikua mgumu sana,.. Ilikua ni lazima uscan vyeti ndo uvitume.
Wengi kati ya waliomaliza chuo 2015 walirudi vijijini kwao, huko wanascan vipi vyeti?
Na hata hivyo bado ilikua ni ngumu kupata lile tangazo lao kama huna smartphone.. Wamejiuliza, katika hao 5000 wangapi wana smartphone? Au walitangaza rediono au kwenye tv? Jibu hapana
Pia, shule za private zipo nyingi sana..
Mtu umemueka kutoka 2015 amalize chuo hadi 2017 unamwambia atume cheti, inataka moyo kama mtu huyu ambaye ni mwalimu wa Sayansi ameshapata shule ya private inayomlipa 1M kwa mwezi, then umrudishe kwnye 700k.. Siku hizi watu wanataka mpunga wa fasta, sio mpunga wa serikalini.

Mwisho, nakiri kuwa nami ni mmoja wa wahitimu waliomaliza 2015, na sina cheti feki hata kimoja.. Lakini nimekauka kwa sababu hapa nilipo nalipwa vizuri, ni nyumbani, mishe nyingi na sina stress..
Nitume cheti afu unipange kijijini ndani ndani huko nikaanze upya? Ili iweje?
Tangu 2015 tumalize chuo hadi sasa mlikua wapi?
 
Huyu Mama kashakuwa kituko tayari kwa ngonjera na sarakasi za uhakiki
 
Walimu zaidi ya 5000 waingia mitini

Takwimu hiyo imetajwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Angela Kairuki wakati akizungumza na watumishi wa umma wanawake katika Manispaa ya Dodoma katika wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kairuki alikuwa akizungumzia suala la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, na kusisitiza kuwa ifikapo mwezi Machi mwaka huu watumishi wote wa umma ambao watakuwa hawajawasilisha vyeti vyao vya kitaaluma watafukuzwa kazi.

Amebainisha kuwa katika zoezi lililofanywa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (Nida) waligundua watumishi wengi hawana vyeti na baadhi yao wanatumia vyeti feki hasa wa kada ya ualimu kwa kuwa wana uhakika wa ajira pindi wanapomaliza vyuo.

"Kulikuwa na taarifa kuwa kuna zaidi ya walimu 8,000 waliokuwa wanatakiwa kuajiriwa lakini baada ya serikali kutangaza nafasi hiyo ni walimu 2,100 tuu ndiyo walioomba nafasi mpaka sasa. Sasa hapo suala la kujiuliza je hao wengine mpaka sasa wako wapi kama hawana vyeti feki!? Nataka niwaambie kuwa hakuna mwenye cheti feki atakayesalimika kwenye Utumishi wa umma," amesema Kairuki.

Amesema ni bora aonekane ni waziri anayechukiwa na jamii kuliko kulifumbia macho suala la vyeti feki kwa watumishi wa umma.

"Tumetoa muda wa kutosha kwa watumishi wa umma kuwasilisha vyeti vyao vya kitaaluma bila shaka walifika mpaka hapa kwenu lakini jambo la kusikitisha ni kwamba mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi bado hawajawasilisha," alisema Kairuki.....Vyeti hawajaleta na hata namba ya utambulisho (index number) hawaleta sasa wanataka tuwafanyaje??? Nawamegemea tu siri na mkawaambie na wenzenu itakapofika Machi Mosi hawajawasilisha vyeti vyao tunawafukuza kazi."

Amesema kama serikali itaharakisha zoezi hilo watumishi wa umma wanaostahili watapandishwa vyeo na mishahara yao kwa kuwa zoezi hilo limesitishwa kutokana na uhakiki wa vyeti.
Sawa mama tumekusikia,ila utekeleze basi. Tumechoka maneno matupu.Hawa vihiyo ndio wanaochangia kuharibu elimu ya watoto wetu.
 
Kure kwa maafande hawezi kuzungumzia. Walimu ndo wepesi kusimangwa na kunsotwa tu. Mume wangu bola aache tu hii ajila
 
Back
Top Bottom