Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Angela Kairuki: Zaidi ya walimu 5000 waingia mitini

Umesema kweli ndugu yangu! Kuna mkufunzi mwezetu hapa chuo cha ualimu morogoro mjini. cheti chake cha kidato cha nne amemupa ndugu yake anakitumia arusha! hivyo basi wahakiki wapite huku. anaitwa Neema huyo mkufunzi.
Pilipili yakuwashia nin! Nyie ndo mnaoleta majungu makazini...umbea umbea umbea.
 
Mimi najiuliza hivi baada ya kukaa muda wote huu bila kupewa stahiki zao za harali, watalipwa fidia? Au watalipwa kuanzia pale kuanzia pale waliposimamishiwa stahiki zao? Au ndio wataambiwa mwafaaaaaa
 
Hao wenye vyeti ndio walizalisha zero mbopo na somangila
 
Walimu zaidi ya 5000 waingia mitini

Takwimu hiyo imetajwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Angela Kairuki wakati akizungumza na watumishi wa umma wanawake katika Manispaa ya Dodoma katika wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kairuki alikuwa akizungumzia suala la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma, na kusisitiza kuwa ifikapo mwezi Machi mwaka huu watumishi wote wa umma ambao watakuwa hawajawasilisha vyeti vyao vya kitaaluma watafukuzwa kazi.

Amebainisha kuwa katika zoezi lililofanywa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (Nida) waligundua watumishi wengi hawana vyeti na baadhi yao wanatumia vyeti feki hasa wa kada ya ualimu kwa kuwa wana uhakika wa ajira pindi wanapomaliza vyuo.

"Kulikuwa na taarifa kuwa kuna zaidi ya walimu 8,000 waliokuwa wanatakiwa kuajiriwa lakini baada ya serikali kutangaza nafasi hiyo ni walimu 2,100 tuu ndiyo walioomba nafasi mpaka sasa. Sasa hapo suala la kujiuliza je hao wengine mpaka sasa wako wapi kama hawana vyeti feki!? Nataka niwaambie kuwa hakuna mwenye cheti feki atakayesalimika kwenye Utumishi wa umma," amesema Kairuki.

Amesema ni bora aonekane ni waziri anayechukiwa na jamii kuliko kulifumbia macho suala la vyeti feki kwa watumishi wa umma.

"Tumetoa muda wa kutosha kwa watumishi wa umma kuwasilisha vyeti vyao vya kitaaluma bila shaka walifika mpaka hapa kwenu lakini jambo la kusikitisha ni kwamba mpaka sasa kuna baadhi ya watumishi bado hawajawasilisha," alisema Kairuki.....Vyeti hawajaleta na hata namba ya utambulisho (index number) hawaleta sasa wanataka tuwafanyaje??? Nawamegemea tu siri na mkawaambie na wenzenu itakapofika Machi Mosi hawajawasilisha vyeti vyao tunawafukuza kazi."

Amesema kama serikali itaharakisha zoezi hilo watumishi wa umma wanaostahili watapandishwa vyeo na mishahara yao kwa kuwa zoezi hilo limesitishwa kutokana na uhakiki wa vyeti.
Walitangaza kwa walimu wa masomo ya sayansi siyo walimu wote
 
Matatizo ya akili yako ndogo. Ukipandisha madaraja na mishahara ya watumishi wakati bado kuna watumishi hewa na wasio na sifa stahiki aka vyeti feki unajua implication Yake? Nadhani kuna umuhimu wa wachungaji wa humu jf kuwa wanachukua muda kutafakari kabla ya kupost maana kuna watu kibao humu wanakurupukia hoja wasiziokuwa na uelewa nazo
Dunia ya sasa huwez kufanya watu ni mazuzu kama unavyotaka kuaminisha umma. Cha msingi ni kuvuta tu subira. Lakini sababu zitolewazo ni nyepesi hasa kwa watu wasiohusika.
 
Back
Top Bottom