Angekuwa ndiyo Lowassa...

Angekuwa ndiyo Lowassa...

Na mvi ameshakua waziri, wazirmkuu, Mkurugenzi wa kituo cha mikutano AICC na nyadhifa nyingi lakini hakuna sehemu katika hizo ambayo amekaa na hakujinufaisha yeye binafsi. Ma mvi ataendelea kua Fisadi ata akiwa mjumbe wa nyumbani kwake wizi na dhuluma zipo kwenye damu. Watanzania hatuwezi kunywasumu kwa kuilamba, hataingia ikulu. K
ama mnampenda mpeni uenyekiti wa Chama chenu.
 
Sabalkheri wanaJF na Alhamisi njema kwenu nyote na popote pale mlipo pembe ya dunia hii.

Sasa leo hebu tulonge kidogo ki-nadharia tete. Nimekaa kwa muda mrefu sana sasa nikijiuliza juu ya swali hili bila kupata jibu la uhakika.

Tuseme ingetokea mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA ndo angeibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha urais mwaka jana.

Halafu baada ya kuanza kazi akafanya mengi kama aliyoyafanya rais wetu wa sasa MTUKUFU Dkt. John Pombe Joseph Magufuli...

Yaani akapiga marufuku safari za hovyo hovyo za nje ya nchi, akaagiza baadhi ya sikukuu za kitaifa tubadili namna tunavyozisherehekea kitaifa, akawa ni mtu wa kukaa nchini muda mwingi na kutuma wawakilishi pale inapobidi, akatumbua majipu hadharani na faraghani, akanunua ndege mpya kwa lengo la kufufua shirika letu la ndege, na kadhalika na kadhalika.

Swali ibuka ni je, watu wanaompinga rais Magufuli sasa hivi, pia wangempinga Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?

Au wangemmiminia sifa kemkem na kusema kwamba acha awanyooshe maana walikuwa wamezoea?

Mkuu, umepotoka na hizo fikra zako. Hakuna mtu anayempinga JPM kwa hayo uliyotaja hapo juu. Kwa nini usiwe muwazi ukataja mambo ya msingi ambayo watu wanaikosoa serikali iliyoko madarakani? Kwa mfano, EL angekuwa Rais kisha akapiga marufuku CCM kufanya shughuli za siasa kama maandamano na mikutano ya hadhara, wana CCM wangemsifia?
Toa mifano halisi ili iukusaidie pia kuona the bigger picture. Don't narrow down your thinking....
 
Sabalkheri wanaJF na Alhamisi njema kwenu nyote na popote pale mlipo pembe ya dunia hii..............

Swali ibuka ni je, watu wanaompinga rais Magufuli sasa hivi, pia wangempinga Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?

Au wangemmiminia sifa kemkem na kusema kwamba acha awanyooshe maana walikuwa wamezoea?

Mheshimiwa Ngabu asante kwa swali na mada husika.

Kama sasa hivi tunaishi maisha yasiyo halisi basi swali lako ni halali (legitimate) lakini kama tunaishi maisha halisi basi swali lako linakuwa limejikita kwenye dhana zaidi (abstract).

Magufuli anapimwa kama Rais lakini huwezi kumpima Lowassa kama Rais kwa vile yeye sio Rais.

Baada ya kusema hayo nataka kutumia vizuri fursa hii kujikita ndani zaidi ili kukomesha na kuondoa dhana/hisia/hoja na baadhi ya vimelea vya ugonjwa sugu wa saratani kwenye tawala za nchi hii toka awamu ya kwanza mpaka sasa. Kuna watu zamani na hata sasa, iwe ni kwa makusudi au malengo fulani lakini bado "kwa nia njema" zao wanataka kuididimiza nchi hii. Tukatae!

1. Siasa
Kwa awamu zote 5, CCM ndio chama kilichotoa Rais na Wabunge wengi wa nchi hii na hivyo kwa awamu zote 5, CCM ndio chama kilichotawala nchi hii. Haiwezekani kuitenga CCM na Rais/Serikali yeyote au awamu yoyote ile mpaka sasa, iwe kwa mazuri au mabaya. Kama ni mafanikio (ya ukweli) CCM inahusika kwa sehemu kubwa na pia kama ni matatizo CCM ndio pekee chanzo na mwajibikaji kwa sehemu kubwa. Hata akili za mwendawazimu tu zinaona kinyaa kujaribu kutenga au ku-spin kama ambayo imekuwa ikifanyika hasa nyakati za kampeni na majira haya katika siku za karibuni.

Ni ufinyu wa mawazo, ni ulevi, ni ukada, ni ubinafis tu unaomsukuma mtu kusema au kudhania (imply) Rais Magufuli sio sehemu ya matatizo ni makosa. Kama yuko CCM (na alikuwa CCM) he's ultimately part of the problems. Sasa kama anarekebisha makosa yao (CCM na Serikali zao) nitamuunga mkono lakini sitampongeza. Walitumia muda wetu na rasilimali zetu vibaya kwa hiyo kama sasa anataka kurekebisha basi mlango uko wazi, lakini ingebidi wafanye kwa gharama zao na sio za kwetu tena kama Taifa. Nasisitiza nitamuunga mkono kama yuko siriaz lakini sitampongeza. Why should I? Sana sana nitaweka sharti moja nalo ni: akikamilisha kazi hiyo na ionekane hivyo (kumerekebika), basi nitaweka hata kwenye wosia wangu, apongezwe wakati huo Mh. Magufuli apongezwe!

2. Elimu
Kutokana na hoja Na. 1, mafanikio na matatizo ya nchi hii katika sekta ya Elimu ni mbegu, zao na tunda la CCM na Serikali zake. PERIOD. Hakuna mbia wala mshirika. Elimu ya nchi hii ni ya kiwango cha chini mno. Elimu ya nchi hii haikujengwa kumsaidia mwananchi kwa kumwelimisha na kumjengea uwezo wa kutumia akili, utashi na mazingira yake ili kujikwamua kutoka katika umaskini, maradhi, ujinga, ufisadi nk. At best Elimu yetu imekuwa ni ya kuzalisha "tabaka la watawaliwa" kwa kiwango kikubwa na pia "tabaka la watumikia" kwa sehemu iliyobaki, in between lucky is all. Utumishi ni taaluma lakini kutumikia/kutumika sio taaluma; in fact unaweza kumfundisha nyani au mbwa na akatumikia/akatumika unayotaka vizuri tu lakini ni vigumu kumpata nyani/mbwa mtumishi (samahani simaanishi kuudhi au kudhalilisha ni mfano tu). Kiwango cha utumishi (quality of service) ni cha chini mno. Juhudi za Rais Mh. Magufuli katika eneo hili naziunga mkono lakini nina mashaka na matokeo yake kwa muda-wa-kati na mrefu ujao. Ni suala linalohitaji tiba sahihi zaidi ya ukali na adhabu kama anavyofanya sasa.

Laiti kiwango cha elimu kingekuwa bora na sio duni kama hiki tulichonacho bila shaka muda huu tusingekuwa tunaongea habari za Magufuli vs Lowassa nk. Nina hakika tusingewahitaji hawa wote wawili katika nafasi hiyo, tungekuwa na far better plethora of competent, good and relevant candidates. If anything, our current choices/options are closer to none and at best a useless and costly drama.

Mtazania wa kawaida ana uwezo mdogo sana wa kuelewa, kupambanua, kuchunguza na/au kuhoja hata mambo madogo na ya kawaida sana. Wengi hawana (kwa vile hawakupewa elimu nzuri/stahiki) uwezo. Viongozi wetu wengi (ambao nao ni zao la mfumo huo) ni kielelezo cha uduni huo. Nenda Vijijini, nenda Kata, nenda kwenye Halmashauri ukaone "maono na hekima za viongozi".Huku utaona kwa kiwango cha lami, uhalisia wa ukubwa wa tatizo ninalojaribu kulileta mezani. Kwa maoni yangu, umaskini wa Watanzania kwa sehemu kubwa chanzo chake ni eneo hili.

3. Jamii
Kwa sababu Na. 2 hapo juu, jamii ya Tanzania inaishi kwa umoja na amani kulingana tu na angle unayosimama kuangalia.
Kwanini? Mshikamano na umoja wa Kitaifa ni dhana ambayo kadiri itakavyoaminiwa na kutekelezwa kwa sehemu na raia basi mshikamano na umoja wa watu kama Taifa utaendelea kuwepo. Lakini, viko vigezo (factors) nyingine muhimu ambazo husababisha au kuchochea aidha umoja, mshikamano na amani kuendelea kuwepo au kupungua/kupotea. Moja ni elimu, jingine ni haki na usawa, jingine ni uwajibikaji wa pamoja na wa binafis, jingine ni maendeleo (kinyume cha umaskini) na jingine ni kujenga taasisi na mfumo imara mfano Bunge, Mahakama, Polisi, Majeshi, Taasisi za Huduma za kijamii nk nk

Katika awamu ya kwanza kama Taifa, pongezi kubwa ni kujenga Utaifa na kuondoa ukabila, udini na ukanda....hii ilitufanya tujitazame kama Taifa zaidi. Kuna baadhi ya mbinu/njia zilizotumika ambazo siziungi mkono, lakini kwa sehemu kubwa eneo hili ndio ambalo Mwalimu Nyerere alifanikiwa pengine kuliko mengine yote. Awamu zilizofuata hazikuwa na kubwa la kufanya, ingawa kwa bahati mbaya katika awamu ya 4 madoa na nyufa kadhaa zilijitokeza zenye vimelea hatari kwa Utaifa wetu. Mpaka sasa havijarekebishwa, kwa maoni yangu.

Ni budi kwa kila mmoja wetu kuenzi na kujiepeusha na mambo yanayotugawa kama Taifa. "Ni rahisi kubomoa kuliko kujenga" wahenga walinena.

4. Uchumi

Kwa muktadha Na. 1-3, hapa ndio kiini na kipimo cha utu. Mengine yote ni secondary, it is the economy and the well-being of the citizens that occupies the first and the only primacy of spots.
Maana nyingine, baada ya kuwa Taifa, tuna serikali na mipaka yetu ya nchi iko bayana jambo pekee na la kwanza ni ustawi (prosperous, well-being, development, advancement and security) ya raia/watu wa nchi. Sasa toka tuwe Taifa (huru) ni miaka 55, tujipime tuliko sasa na tulikopaswa kuwa vinaendana? Rasilimali muda + rasimilmali ghafi zingine vs matokeo ya tulipo vinaendana? Jibu la wazi na pekee ni HAPANA. Haviendani. Tuko nyuma kama Taifa, tuko nyuma kama binadamu. Hali yetu, huduma zetu iwe kwenye elimu, afya, uongozi na utawala bora, haki na usawa, mgawannyo wa keki ya Taifa nk nk kote huko tumefeli. Haihitaji siasa wala digirii wala ukada kujibu swali hili. Na kama uchumi ni kitu pekee cha kupima.

Baada ya kuweka msingi wa nyumba na kuanza kuanza kujenga tofali, hulazimiki tena kurudia kuweka msingi. Kufanya hivyo hutakaa ujenge nyumba, sababu hiyo nyumba haitakaa isimame, ifike ngazi ya kupauliwa nk. Baada ya hiyo misingi mitatu ya kwanza hapo juu (kwamba ni imara au la sio lengo la mada hii), nyumba hii ilipaswa kusonga mbele na kukamilika. Na ni uwezo wa uchumi pekee ndio ungewezesha hilo ila kwa bahati mbaya sana kwa awamu zote 5 tumeshindwa vibaya mno kwenye uchumi. Uchumi hupima muda na thamani.

Nikomee hapa kwa sasa, ila nikipata muda nitaandika makala kadhaa za uchambuzi HURU. Ni siasa za watu na matukio ndio zimetufikisha hapa. Tusiziendekeze, tujisahihishe. Rais Magufuli na CCM lazima watoke hapo kwenye u-watu, u-matukio, u-kada na Vyama vya upinzani navyo vitoke hapo kadhalika ili tulete pamoja nguvu zetu, elimu, uzoefu, akili nk tuikwamue nchi hii kabla haijaangamia.
 
MKUU ukiona umeingia upinzani kazi yako ni kupinga tu hata kama ni zuri,Mie ni heri ninyamaze kuliko kukaa upinzani.

Kibaya zaidi siasa za tz zimejaa unafiki,watu wanatumia siasa kwenye kila kitu, hawaoni mazuri ya upande wa pili hata kidogo!

Unataka wakosoe na mazuri pia? siku zote wakosoaji wanatafuta mabaya tu. Karibu kwenye ulimwengu halisia, don't live with illusions.
 
Na Lowassa alikuwa ni wa chama gani?
Wakikujibu hili utanistua.
Wafia vyama wasiochanganya na akili zao hawachelewi kukanusha kwamba Lowasa hakuwa CCM kabla ya CHADEMA.
Na zile video clip zetu za zamani tukimpiga madongo Lowasa hawachelewi kuzikanusha. Our politicians and their supporters can even change the past provided they are supplied with cash. Hii ndio Bongo Tanzania.
 
MKUU ukiona umeingia upinzani kazi yako ni kupinga tu hata kama ni zuri,Mie ni heri ninyamaze kuliko kukaa upinzani.

Kibaya zaidi siasa za tz zimejaa unafiki,watu wanatumia siasa kwenye kila kitu, hawaoni mazuri ya upande wa pili hata kidogo!
Lazima kuna watu wasifie na wengine wakosoe wote wakisifia meaning ni mtu perfect na hamna mtu perfect dunian....
 
Jamani mbona 2020 haiko mbali c tutampa Lowasa sasa sasaivi nchi ya Dr.Magufuli a.k.a jembe.
Namimi nadhani Lowasa atauweka wazi kuhusu RichM, tena tutajua saaingine chama cha Cdm kilikulupuka kumsema lowasa fisadi basi tutamshauri Lowasa kuwa ni hatari kukaa na watu wanao bora arudi agombe tena ccm. Ohoo richmond itafufuka.
 
Mazuri hakuna anayepinga.....km nayeye angezuia wenzie kutokutoa mchango angepingwa tu.......
 
Sabalkheri wanaJF na Alhamisi njema kwenu nyote na popote pale mlipo pembe ya dunia hii.

Sasa leo hebu tulonge kidogo ki-nadharia tete. Nimekaa kwa muda mrefu sana sasa nikijiuliza juu ya swali hili bila kupata jibu la uhakika.

Tuseme ingetokea mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA ndo angeibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha urais mwaka jana.

Halafu baada ya kuanza kazi akafanya mengi kama aliyoyafanya rais wetu wa sasa MTUKUFU Dkt. John Pombe Joseph Magufuli...

Yaani akapiga marufuku safari za hovyo hovyo za nje ya nchi, akaagiza baadhi ya sikukuu za kitaifa tubadili namna tunavyozisherehekea kitaifa, akawa ni mtu wa kukaa nchini muda mwingi na kutuma wawakilishi pale inapobidi, akatumbua majipu hadharani na faraghani, akanunua ndege mpya kwa lengo la kufufua shirika letu la ndege, na kadhalika na kadhalika.

Swali ibuka ni je, watu wanaompinga rais Magufuli sasa hivi, pia wangempinga Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?

Au wangemmiminia sifa kemkem na kusema kwamba acha awanyooshe maana walikuwa wamezoea?
Unauliza watu ambao wakati huyo Lowassa yuko upande huu mwingine walimsema maneno yote mabaya hasa hasa FISADI, leo hii ndio Messiah! Huitaji kuwa brain surgeon kujua wangempongeza au kumponda!
 
Nadhani kuna sehemu angefanya vizuri na sehemu nyingine asingefanya vizuri kwa kuwa ni nadharia basi tuichukukie kama nadharia ninavyoona ingekuwa kama ifuatavyo

1. Elimu - leo watu wanalalama kuhusu mikopo ambapo wanafunzi zaidi ya 66000 wa elimu ya juu wamekosa mikopo kinadharia Lowassa angefanya vizuri kwenye elimu japo kwenye "approach" yake kwenye baadhi ya mambo hawana tofauti na Magufuli (ubabe) unaweza rejea kwenye uchangiaji wa ujenzi wa shule za kata wakati akiwa waziri mkuu. Kwa kuwa ni nadharia pengine angefanya vizuri zaidi na kukosolewa au angefanya vibaya zaidi na kukosolewa na wengi zaidi

2. Kupambana na ufisadi, japo magufuli anajaribu kupambana na "pretty corruption" wakati zile "grand corruption" chache saana ndo zimeguswa na magufuli mfano kesi ya Kitillya na wengine sidhani kama hii ingeweza guswa kama Lowassa angekuwa rais nafikiri kinadharia. Angekosolewa

3. Kununua ndege. Kinadharia sidhani kama Lowassa angeweza kununua ndege kwenye kipindi cha mwaka mmoja wa utawala wake. Biashara ya usafiri wa anga bado tunasua sua. Mwanzo mwa miaka ya 2000's akina Elvis Musaba na wenzake walianzisha kampuni ya ndege "Africa one" lakini walishindwa ku-operate sikumbuki hata ilifia wapi. Serikali ya Magufuli ingepunguza burdens kwa local investors kwenye sector ya anga. Kwa hili asingefanya na asingekosolewa

4. Kupiga marufuku safari za nje, anadhani hapa asingefanya kama alivyofanya magufuli kabisa ila angepunguza safari kidogo safari kwenye ofisi yake kwingine nadhani watu wangeendelea na safari zao kama kawaida. Angesifiwa

5. Sikukuu za kitaifa asingebadilisha bado tungekuwa tunasherekea kama zamani na hapa hakuna mtu angemkosoa

6. Kuminya siasa. Hapa sidhani kama angeminya kungekuwa bado na uhuru wa kufanya siasa. Kwa kutominyaa siasa bado wasingemsifia

7. Kushughulikia uzembe bandarini( kufungwa kwa flow meter) hapa ni nusu kwa nusu inategemeana na nani alikuwa nyuma ya mpango huo. Angesifiwa/asingesifiwa bado ni nadharia tu

8. Kuhamia Dodoma, asingefanya ana asingesifiwa maana dodoma yenyewe ilikuwa imekaa kinadharia kuwa ni mji mkuu


Kwa kuwa ni nadharia, inawezekana angefanya vizuri zaidi au vibaya zaidi. Japo anayofanya magufuli si mabaya sana ila ana upungufu kwenye utawala bora na siasa safi kwa wote
 
Kabisa unamfananisha Lowassa na huyu nani wenu ....We lazima sio mzima
 
Angefanya hayo mambo kijinga jinga kama tunavoshuhudia yakifanywa kijinga jinga angepingwa tu..!!
 
Back
Top Bottom