Angekuwa ndiyo Lowassa...

Angekuwa ndiyo Lowassa...

Kuna kitu ambacho wachangiaji wengi hawajakiona hapa. Mazingira ya urais wa Lowassa yangekuwa tofauti kabisa na ya sasa (ya urais wa Magufuli) kutokana na kuwa na agenda tofauti. Kimsingi, kuna "variable" ingeongezeka: Lowassa angetawala chini ya Katiba ya Warioba; jambo linalofanya huu mlinganisho "hypothetical" kati ya urais wake na wa Magufuli kuwa batili. Ikumbukwe kuwa Lowassa aligombea urais akiungwa mkono na vuguvugu la Ukawa, na agenda yao kubwa ikiwa ni kupitisha Katiba ya Warioba mara moja. Na tofauti kubwa kati ya katiba ya sasa na ya Warioba ni kwamba, wakati katiba ya sasa inampa Rais Magufuli mamlaka makubwa yasiyohojika ya kiutawala, katiba ya Warioba ingemdhibiti "Rais" Lowassa kwa kuzipa uhuru na nguvu kubwa taasisi za kiutawala. (Jambo la kuzingatia hapa ni kuwa katiba ya sasa ni mbovu na haitufikishi kokote).
Na katiba hii mkuu kaipiga teke......
 
Hampendi Lowassa wenu asemwe eh?

Halafu hapo hapo usikute nyie ndo mlikuwa mstari wa mbele kumlaani wakati alipokuwa CCM.
Kweli nilimlaumu sana Lowassa kwa kuwa sikuujua ukweli. Kwa sasa naujua ukweli na nimejifunza kuacha siasa za kishamba za '' watu'' badala yake '' issues''
 
Wengi wanamchukia Mtukufu kwa kauli zake....hasa zile za kibabe... achana na zinazokwenda na kejeli + vijembe ndani yake...na upande anatugeukia na kutuomba tumuombee.....Waliomtangulia hawakuwa na Lifestyle ya dizaini yake....kila kitu yeye ndie mfanyaji....Poa, tunamuombea mabadiriko....mbeleni atachenji...
 
Sabalkheri wanaJF na Alhamisi njema kwenu nyote na popote pale mlipo pembe ya dunia hii.

Sasa leo hebu tulonge kidogo ki-nadharia tete. Nimekaa kwa muda mrefu sana sasa nikijiuliza juu ya swali hili bila kupata jibu la uhakika.

Tuseme ingetokea mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA ndo angeibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha urais mwaka jana.

Halafu baada ya kuanza kazi akafanya mengi kama aliyoyafanya rais wetu wa sasa MTUKUFU Dkt. John Pombe Joseph Magufuli...

Yaani akapiga marufuku safari za hovyo hovyo za nje ya nchi, akaagiza baadhi ya sikukuu za kitaifa tubadili namna tunavyozisherehekea kitaifa, akawa ni mtu wa kukaa nchini muda mwingi na kutuma wawakilishi pale inapobidi, akatumbua majipu hadharani na faraghani, akanunua ndege mpya kwa lengo la kufufua shirika letu la ndege, na kadhalika na kadhalika.

Swali ibuka ni je, watu wanaompinga rais Magufuli sasa hivi, pia wangempinga Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?

Au wangemmiminia sifa kemkem na kusema kwamba acha awanyooshe maana walikuwa wamezoea?
Mke wake angekua kashafungua NGO na kuanza sanaa
 
Angekuwa ni anafanya upuuzi wa ivyo nisinge msuport na nisingempigia kura Tena. Na ningemtukana kimoyonoyo kama watz wengi wanavyomtukana magufuli.
 
hakun
MKUU ukiona umeingia upinzani kazi yako ni kupinga tu hata kama ni zuri,Mie ni heri ninyamaze kuliko kukaa upinzani.

Kibaya zaidi siasa za tz zimejaa unafiki,watu wanatumia siasa kwenye kila kitu, hawaoni mazuri ya upande wa pili hata kidogo!
hakuna watu wanafiki kama ccm kwa taarifa yako
 
Unafikiri lizabon angesemaje? Kama siyo kusema anataka kuua muungano na kubadili jina la Tanzania kurudi Tanganyika kwa sababu kafuta sherehe za Uhuru.
 
Bavicha kundi la manyang'au wachonganyishi wapenda unafiki. Mlimuua chacha wangwe kwa maslahi wa wachache wenu.
 
Wabunge wenu wamepigwa na njaa wameamua kuingia bungeni wakati walisema hawataingia mjengoni.
 
Sabalkheri wanaJF na Alhamisi njema kwenu nyote na popote pale mlipo pembe ya dunia hii.

Sasa leo hebu tulonge kidogo ki-nadharia tete. Nimekaa kwa muda mrefu sana sasa nikijiuliza juu ya swali hili bila kupata jibu la uhakika.

Tuseme ingetokea mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA ndo angeibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha urais mwaka jana.

Halafu baada ya kuanza kazi akafanya mengi kama aliyoyafanya rais wetu wa sasa MTUKUFU Dkt. John Pombe Joseph Magufuli...

Yaani akapiga marufuku safari za hovyo hovyo za nje ya nchi, akaagiza baadhi ya sikukuu za kitaifa tubadili namna tunavyozisherehekea kitaifa, akawa ni mtu wa kukaa nchini muda mwingi na kutuma wawakilishi pale inapobidi, akatumbua majipu hadharani na faraghani, akanunua ndege mpya kwa lengo la kufufua shirika letu la ndege, na kadhalika na kadhalika.

Swali ibuka ni je, watu wanaompinga rais Magufuli sasa hivi, pia wangempinga Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?

Au wangemmiminia sifa kemkem na kusema kwamba acha awanyooshe maana walikuwa wamezoea?
Ukosoaji ungekuwepo hata angefanya mazuri kiasi gani, serikali inayokosa ukosoaji ni sawa na kipofu anayejiendea tu pasipo muongozo wa mtu au fimbo, na hii ipo duniani kote na hata kwenye serikali za kiimla hazikosi wakisoaji. Na hata kwenye maisha yako kama huna mkosaji gombana hata na jirani yako utajua madhaifu yako ili uweze kuyarekebisha kwa sababu ndio atakuwa mkosoaji wako mkuu na utasikia kupitia majirani zako wengine
 
Back
Top Bottom