Angekuwa ndiyo Lowassa...

Angekuwa ndiyo Lowassa...

Sabalkheri wanaJF na Alhamisi njema kwenu nyote na popote pale mlipo pembe ya dunia hii.

Sasa leo hebu tulonge kidogo ki-nadharia tete. Nimekaa kwa muda mrefu sana sasa nikijiuliza juu ya swali hili bila kupata jibu la uhakika.

Tuseme ingetokea mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA ndo angeibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha urais mwaka jana.

Halafu baada ya kuanza kazi akafanya mengi kama aliyoyafanya rais wetu wa sasa MTUKUFU Dkt. John Pombe Joseph Magufuli...

Yaani akapiga marufuku safari za hovyo hovyo za nje ya nchi, akaagiza baadhi ya sikukuu za kitaifa tubadili namna tunavyozisherehekea kitaifa, akawa ni mtu wa kukaa nchini muda mwingi na kutuma wawakilishi pale inapobidi, akatumbua majipu hadharani na faraghani, akanunua ndege mpya kwa lengo la kufufua shirika letu la ndege, na kadhalika na kadhalika.

Swali ibuka ni je, watu wanaompinga rais Magufuli sasa hivi, pia wangempinga Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?

Au wangemmiminia sifa kemkem na kusema kwamba acha awanyooshe maana walikuwa wamezoea?

Tukisema ukweli,
Lowasa asingeweza yafanya haya ambayo Magufuli ameyafanya
Kwanza angeingiza nchi kwenye mgogoro mkubwa wa kiuchumi ( Naamini angekopa saana)

Pili ingemchukua miaka zaidi ya mitatu kulipa fadhila kwa wale waliompiga support hususani za fedha

na kikubwa zaidi rasilimali za nchi zote zingekuwa rehani

Ni mtizamo TU
 
sikiliza wewe nyani ..

lowasa asingeanza na madawati...angeanza na walimu...

lowasa asingeanza na ndege...angeanza na madawa hospitali..

lowasa asingeanza na chato airport angeanza na mikopo ya wanafunzi..

lowasa asingeanza na ukada..and so much more
 
Siku moja nilipita karibu Na nyumba moja uswahilini nikasikia mama mmoja anamsifia mmewe;
"Mme wangu nakushukuru umefanya jambo la maana kuondoa kinyesi hicho, maana harufu ilikuwa nusu ituue".
Mbali kidogo na pale kulikuwa na watoto wawili wanaongea;
Wa kwanza, "nimekuja kwenu kwa sababu kwetu kunanukaaa!!!"
Wa pili, "kuna nini mpaka kunuke!?"
Wa kwanza, "Baba alirudi usiku kalewa kajisaidia haja kubwa sebuleni".
Nikajua Ni yule mme MTU. Lakini nikamshangaa zaidi yule mama
 
Uko wapi unafiki wangu?
Tukisema ukweli,
Lowasa asingeweza yafanya haya ambayo Magufuli ameyafanya
Kwanza angeingiza nchi kwenye mgogoro mkubwa wa kiuchumi ( Naamini angekopa saana)

Pili ingemchukua miaka zaidi ya mitatu kulipa fadhila kwa wale waliompiga support hususani za fedha

na kikubwa zaidi rasilimali za nchi zote zingekuwa rehani

Ni mtizamo TU

Kweli ni mtizamo tu lakini wa-KIJINGA!
 
Kwenye manifest ya lowasa hakuna kufungia safari za nje, kwa hiyo asingeleta hizo swaga angefanya kazi ya kuleta maendeleo kwa mujibu wa ahadi za kwenye kampeni. Anachokifanya mukulu ni kuendesha duka kwa matukio. Na inapoelekea tunakuja kuwa ukoo wa kambale. Ref: yanayotokea Arusha nk.
 
Wapi uhandisi ulipoonekana? Kwa wanafunzi kuitwa ****** na wengine kukosa mikopo? Kwa mahosipitali kukosa dawa? Plz be realistic & objective stop being so much in love with your Party.
Nimehoji hiyo comparison
 
Sabalkheri wanaJF na Alhamisi njema kwenu nyote na popote pale mlipo pembe ya dunia hii.

Sasa leo hebu tulonge kidogo ki-nadharia tete. Nimekaa kwa muda mrefu sana sasa nikijiuliza juu ya swali hili bila kupata jibu la uhakika.

Tuseme ingetokea mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA ndo angeibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha urais mwaka jana.

Halafu baada ya kuanza kazi akafanya mengi kama aliyoyafanya rais wetu wa sasa MTUKUFU Dkt. John Pombe Joseph Magufuli...

Yaani akapiga marufuku safari za hovyo hovyo za nje ya nchi, akaagiza baadhi ya sikukuu za kitaifa tubadili namna tunavyozisherehekea kitaifa, akawa ni mtu wa kukaa nchini muda mwingi na kutuma wawakilishi pale inapobidi, akatumbua majipu hadharani na faraghani, akanunua ndege mpya kwa lengo la kufufua shirika letu la ndege, na kadhalika na kadhalika.

Swali ibuka ni je, watu wanaompinga rais Magufuli sasa hivi, pia wangempinga Lowassa kama angekuwa ndo yeye anayafanya hayo anayoyafanya Magufuli?

Au wangemmiminia sifa kemkem na kusema kwamba acha awanyooshe maana walikuwa wamezoea?
Ungeongezea na haya
Angezuia mikutano mpaka 2020
Angezima bunge
Angezuia Ajira
Angekwapua pesa za kagera
Na angeropoka kwa kutukana watu ingekuwaje?
 
😳😳😳
Nyani Ngabu Kuna tofauti kubwa sana kati ya watu hao wawili.Mmoja ni Mwanasiasa na Mtafutaji vs Mwanasiasa kwa Bahati tu na Mtendaji. Sasa tusije Kariri kanuni isiyosahihi kwenye Mikwamo yetu ya Kimaendeleo.

Umesikia wapi watu wanamlaumu kwa mengi aliyokwisha ya fanya zaidi ya lawama kwenye issue ya uhuru wa shughuliza za kisiasa.
Point!
 
Watu walisema chadema hawawezi kumchukua Lowassa,ila hapa tena wanasema Lowassa asingefanya kama alivyofanya Magufuli.
 
waki nani wampinge nani?

kama wameshindwa kupinga "bwana yule kung'ang'ania uenyekiti sembuse Edo?

kama walishindwa kupinga ujio wa waliyemuita 'fisadi' watapingaje akiwa kama rais?

siasa ni mchezo wa kitoto sana.

kama rais angekuwa Edo,CCM wangeponda kila anacho kifanya,hili la mikopo lingekuwa la Edo UVCCM wangepayuka kila siku.
Rais angekuwa Edo kwa makelele ya CCM tungejua kuwa uchumi umeshuka.

siasa tuachie wenyewe.
 
Nilicho na uhakika ni kuwa Lowasa angekuwa bora mara mia ya huyu...ingawa asingetenda sawa yote anayoyafanya huyu
 
Kwani huyo mnae musudu pamoja na kufanya hivyo mbona ndio kwanza hali imezidi kuwa ngumu mtani tofauti na watangulizi wake
 
Wangekuja na zile "Tumeweza kuondoa mfumo"
Ndio maana Lowasa anafanikiwa.
 
Mtawala yeyote ni wakumulikwa tu-awe kijani au blue/nyekundu-lazima amulikwe na akikosea apashwe. Of course kwa wale "ulipo tupo" hiyo inaweza kuwa ngumu. Watu lazima wakumbuke ahadi/manifesto (dhamira?) inaweza ikapitana na utendaji.
 
Sasa hivi namba tunaisoma, huku watu wanafukuzwa kazi Kote serikalini na private, biashara haziendi, nchi haiwekezeki, hospitali hakuna dawa(chanjo Zinatafutwa kama tochi), kwenye Elimu vijana wananyimwa mikopo.
Ki ukweli watawala wajiangalie maana CCM tuliishaichoka matumaini yalikuwa kwa mtu na sio Chama, sasa na yeye Ndio Hali kama hii.
Nilishawai kuwaambia Watanzania kuwa chama ni watu na si mtu. Ccm hata wamsimamishe Yesu Kristo kwenye uchaguzi sita mpigia kura.
 
Back
Top Bottom