Angejua asingejitokeza kuomba msaada!

Angejua asingejitokeza kuomba msaada!

Sweet16

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Posts
6,357
Reaction score
11,756
Nimepata maswali mengi sana toka nimeona habari ya umauti wa yule binti aliyepigwa risasi October 29 na wale mashetani ya kibibi cha Malawi alijitokeza kuomba msaada mwezi jana tu hapa!

Akajitokeza msamaria eti wa kificho asijulikane wala asitajwe ni nani, kwa wenye D hata moja ilitosha kuwapa jibu la moja kwa moja kuwa ni nani.

Kwahiyo wamemchukua wakaenda kummalizia asiendelee kusimlia hiyo risasi alipigwa akiwa katika mazingira gani ili dunia ione na matahira wanaoimba chadema iliua watu wafunguke akili kwamba mauaji yalikuwa yamepangwa tu ilimradi watu wafe.

Ameishi mwaka mzima akiwa na afya yake ivo ivo kitendo cha kujitokeza tu wale umbwa wauaji wakasema no way huwezi kuendelea kutufichua namna hii. Mwaka mzima, wiki mbili tu kufika muhimbili umezima😭😭😭 mama yako angejua kinachokwenda kutokea ni bora angebaki na wewe katika hali uliyokuwa nayo mpaka hapo Mungu atakapokuchukua.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina
 
Watanzania muwe na roho ngumu dunia ilipo sio sehemu ya kulia ni muda wa kusimama wima macho makavu mbele ya kila ubaya wanaowatendea wajue mpo tayari tuumizane kila mmoja kwa mbinu na vyanzo vyake
 
Back
Top Bottom