Marekani: Polisi wamempiga risasi kijana mwenye umri wa miaka 13 aliyekuwa na matatizo ya akili

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
1ff5622d-14d8-4243-9331-e023028dbea3-medium16x9_policeshootjuvenileinslcglendale090420kutv1.png
Polisi katika mji wa Salt Lake City katika jimbo la magharibi mwa Marekani la Utah wamempiga risasi kijana mwenye umri wa miaka 13 aliyekuwa na matatizo ya akili baada ya mama yake kupiga simu polisi kuomba msaada.​
Hatua hiyo ya polisi imechochea ghadhabu kutokana na kuwa mwendelezo wa matukio ya matumizi ya nguvu yaliyopitiliza kwa raia nchini Marekani yanayofanywa na polisi. Kwa sasa, kijana huyo, Linden Cameron anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali moja baada ya kupata majeraha katika bega, viwiko vya mikono, tumboni na kibofu cha mkojo.​
Mama yake, Golda Barton, alisema kuwa alipiga namba za dharura, 911, kuomba polisi kumzuia mwanaye aliyeanza kufanya vurugu kutokana na kutengana na mama yake aliyekwenda kazini kwa mara ya kwanza baada ya mwaka mzima wa kuwa naye karibu.​
"Niliwaambia 'Hana silaha yeyote, amekasirika tu na anapiga kelele.' Ni mtoto mdogo anayejaribu tu kutafuta usikivu, hafahamu jinsi ya kufanya hivyo kistaarabu," alisema mama yake katika mahojiano na kituo cha televisheni cha KUTV.​
Bi Golda amewalaumu polisi kwa kutumia nguvu kubwa kumtuliza mwanaye ambapo ameeleza kuwa maafisa wawili wa polisi waliingia ndani na kumkuta Linden kisha ndani ya muda wa dakika tano maafisa hao wawili wakaanza kupiga kelele kumtaka Linden kulala chini kabla ya kumfyatulia risasi kadhaa.​
"Ni mtoto mdogo mwenye matatizo ya akili," mama yake alilalamika. "Kwanini mlishindwa kumkamata kwa njia za kawaida tu?"​
Taarifa ya polisi imethibitisha kuwa kijana huyo alikuwa na matatizo ya akili na kuwa alijaribu kuwatishia baadhi ya watu kwa silaha, licha ya kusema kuwa hawakukuta silaha yoyote katika eneo la tukio. Polisi wameapa kufanya uchunguzi wa kina na kwa haraka.​
Matukio ya mauaji ya raia wasio na silaha yametokea kwa kiwango kinachotia wasiwasi nchini Marekani, hasa raia wenye asili ya Kiafrika, hali inayochochea maadamano yanayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini Marekani. Tukio hili linawaweka polisi katika wakati mgumu kufuatia maiaji ya kijana mwingine mwenye matatizo ya akili, Daniel Prude aliyekuwa na umri wa miaka 29 katika mji wa Rochester, New York nchini humo.​
Baadhi ya watetezi wa haki za binadamu wameanza kutilia shaka uwezo wa polisi kukabiliana na changamoto za utoaji wa huduma za dharura huku baadhi ya mamlaka za miji ikibadili mbinu za polisi za utoaji wa huduma za dharura. Asasi ya kiraia ya Neurodiverse Utah imesema kuwa polisi imesababisha madhara zaidi mahali ambapo ilitakiwa kutoa msaada.​
"Maafisa wa polisi hawakutakiwa kukuta hali ya utulivu kwa kijana wa miaka 13 mwenye matatizo ya akili kuliko maafisa wa polisi waliopitia mafunzo," taarifa hiyo ilieleza.​
Mama yake sasa anakusanya michango kwa ajili ya matibabu ya kijana wake, akimweleza kama mtu anayependa michezo ya video, kuendesha magari makubwa na michezo ya kuteleza barabarani, huku akitaka haki itendeke kwa makosa waliyofanya polisi.​
Chanzo: The Guardian
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom