Angalizo: Usitafute mchumba kanisani

Angalizo: Usitafute mchumba kanisani

Makanisani ndio sehemu kwenye mafisi wengi wenye ngozi za kondoo.

Watu wengi waliokosa wachumba hukimbilia kanisani kudhani kuwa mke bora au mke mwema hupatikana kanisani, lakini mke mwema hutoka kwa Mungu. Penye watu wawili au watatu Mungu yupo katikati yao.

Makanisani watu ndio sehemu yao ya kutembeza ngoma, huko watu wanapigana mijeledi kinoma.
Waimba kwaya ni wazinzi kinoma.

Vijana ni wazinzi, wapigaji mizinga na matapeli kupindukia. Ukitaka mwenzi mwema, usiende kumtafuta kanisani, muombe Mungu akupe, naye atakupa kutoka kwenye hazina yake.

Huenda mkakutana kwenye daladala, au sehemu yoyote ile, usikate tamaa, Mungu ana jibu kwa wakati wake.

Ombeni bila kukoma.
Ushauri mwema Heko!
 
Inategemea kupata mke mwema unaweza kumpata sehemu yoyote.
Inaweza kuwa kanisani au la!

Tatizo watu wakimuona mtu anakwenda kanisani wanakuja na fallacy of generalizations kwamba huyo mtu nimtakatifu.

Unahitaji kujitahidi kumjua mke unaetaka kumuoa vyema ndio sababu ya kupewa akili na utashi havikutolewa kwa bahati mbaya.

Naona makanisa ya Kiroho huwa kunakosekana ukaribu wa wachumba kuna katabia kakupenda kuuziana mbuzi kwenye gunia na baadae yanaanza majuto na yakianza majuto ukienda kwa mchungaji anakwambia hilo ni jaribu lako.

Sema tu ndoa nyingi za siku hizi zina matatizo ambayo kiroho tunaita majaribu ila mtaani tunaita matatizo.

Akili na utashi ni lazima vitumike sawasawa ukitumia vionjo na akili ya mchungaji lazima ulizwe.

Shida inakuja mke unaetaka kumuoa hamsali pamoja inakua ni ngumu kukubaliwa hata awe yuko vizuri vipi.

Hili linasababisha limited choice na mtu kumuomba Mungu amuonyeshe mke ila anampangia Mungu tena huyo mke lazima awe ameokoka na wanasali wote.

Mungu hapangiwi huenda mke mnaeendana nae ni kahaba na unapaswa kumbadili lakini wewe umeng'ang'ana lazima mkeo atoke kanisani unaposali ndio mchungaji akubali.
 
Mkuu, umenikumbusha enzi ya miaka ya 90 katika sherehe za Idd Pemba na Unguja, tulishauriwa si vema kumtongoza msichana ukimkuta kwenye viwanja vya sherehe. Eti anakuwa na uzuri wa dukani.
 
Inategemea kupata mke mwema unaweza kumpata sehemu yoyote.
Inaweza kuwa kanisani au la!
Tatizo watu wakimuona mtu anakwenda kanisani wanakuja na fallacy of generalizations kwamba huyo mtu nimtakatifu.
Unahitaji kujitahidi kumjua mke unaetaka kumuoa vyema ndio sababu ya kupewa akili na utashi havikutolewa kwa bahati mbaya.
Naona makanisa ya Kiroho huwa kunakosekana ukaribu wa wachumba kuna katabia kakupenda kuuziana mbuzi kwenye gunia na baadae yanaanza majuto na yakianza majuto ukienda kwa mchungaji anakwambia hilo ni jaribu lako.
Sema tu ndoa nyingi za siku hizi zina matatizo ambayo kiroho tunaita majaribu ila mtaani tunaita matatizo.
Akili na utashi ni lazima vitumike sawasawa ukitumia vionjo na akili ya mchungaji lazima ulizwe.
Shida inakuja mke unaetaka kumuoa hamsali pamoja inakua ni ngumu kukubaliwa hata awe yuko vizuri vipi.
Hili linasababisha limited choice na mtu kumuomba Mungu amuonyeshe mke ila anampangia Mungu tena huyo mke lazima awe ameokoka na wanasali wote.
Mungu hapangiwi huenda mke mnaeendana nae ni kahaba na unapaswa kumbadili lakini wewe umeng'ang'ana lazima mkeo atoke kanisani unaposali ndio mchungaji akubali.
Hata ' bar ' mkuu????
 
Wanaotafuta wachumba kanisani ni madomo zege au wapenda kitonga au na wao ni disgraces, yaani waliochokwa na jamii kwahiyo wanakimbilia church.
 
Makanisa ya kilokolee ndo usime, one day nimeenda kwenye moja wapo ya hilo kanisa.
Aiseee acha kabisa kumbe wanawake na waume wanaosali pale 70% wana matatizo makubwa mengine ayafai kusimulia.
 
Yes hata Bar kuna watu walikutana na wake zao bar na wanaishi kwa amani.
Kikubwa kuendana na mke unaemuoa hata umtoe wapi kama hamuendani litakua ni tatizo tu
Pia tambua kuna ' mme ' na mwaume vile vile ' mke ' na mwanamke.
 
Mimi sikubaliani na hoja hii.

Kanisani ni sehemu mwafaka kwa mkristo kuongea na Mungu. Kuongea na Mungu ni pamoja na kuabudu, kusali, kutukuza, kusifu, kuomba n.k. Kama mke mwema anatoka kwa Mungu, inabidi mkristo aongee na Mungu ili Mungu ampe huyo mke mwema. Moja ya njia ya kuongea na Mungu ni kuomba. Hivyo mkristo anayehitaji mke humwomba Mungu. Kwa hiyo kanisani ni sehemu maalumu iliyokubalika kufanya maombi ingawaje mkristo anaweza kufanya maombi yake nje/mbali na kanisa.

Hakuna haja ya kuwa na shaka maadamu mke mweka hutoka kwa Mungu hakuna sababu ya kuhofu kupata kitu kibaya kutoka kwake. Kwa kuwa kanisani kuna wabaya na wema kwa jinsi ilivyo hakana haja ya kuhofu kuwa mwombaji atapata 'watembeza ngoma', 'wanaopigana mijeledi', vijana wazinzi, 'wapigaji mizinga', matapeli wa kupindukia n.k.

Lakini pia ni vizuri kujihoji. Je, kama mimi ninataka/ninapenda mke mwema, mimi ni mwema? Ni vizuri huyo mke mwema ninayemuomba nimtayarishie mazingira ya wema. Inawezekana sipato mke mwema kwa sababu mimi si mwema.
nadhani hujamuelewa sawia mleta mada
 
Safi sana. Maanake naona maadui wa kanisa wanajitahidi kupotosha.
 
Haya maneno yenu ni kwenye magenge tu.

Huwezi toka huko nankujikoroga koroga kwako na dunia kisa unataka kuoa ndio ukatafutie kanisani, lazima utapata wa kufanana na wewe.

Mungu husema na wanaomcha yeye na kama unajitunza atakuonya na kukujulisha kuhusu mtu unayetaka kumuoa au kuolewa nae.

Haya mambo hayatambulikani kwa macho ya nyama, walio wa rohoni wanatambua.

Kwa kufurashisha genge inawezekana uko sahihi.
Kweli kabisa, hii ni furahisha genge
 
Back
Top Bottom