Angalizo: Usitafute mchumba kanisani

Angalizo: Usitafute mchumba kanisani

Mimi sikubaliani na hoja hii.

Kanisani ni sehemu mwafaka kwa mkristo kuongea na Mungu. Kuongea na Mungu ni pamoja na kuabudu, kusali, kutukuza, kusifu, kuomba n.k. Kama mke mwema anatoka kwa Mungu, inabidi mkristo aongee na Mungu ili Mungu ampe huyo mke mwema. Moja ya njia ya kuongea na Mungu ni kuomba. Hivyo mkristo anayehitaji mke humwomba Mungu. Kwa hiyo kanisani ni sehemu maalumu iliyokubalika kufanya maombi ingawaje mkristo anaweza kufanya maombi yake nje/mbali na kanisa.

Hakuna haja ya kuwa na shaka maadamu mke mweka hutoka kwa Mungu hakuna sababu ya kuhofu kupata kitu kibaya kutoka kwake. Kwa kuwa kanisani kuna wabaya na wema kwa jinsi ilivyo hakana haja ya kuhofu kuwa mwombaji atapata 'watembeza ngoma', 'wanaopigana mijeledi', vijana wazinzi, 'wapigaji mizinga', matapeli wa kupindukia n.k.

Lakini pia ni vizuri kujihoji. Je, kama mimi ninataka/ninapenda mke mwema, mimi ni mwema? Ni vizuri huyo mke mwema ninayemuomba nimtayarishie mazingira ya wema. Inawezekana sipato mke mwema kwa sababu mimi si mwema.
 
Huko kutafuta mke kanisani kuliishaniliiiza sitakaaa nisahau kumesababisha nimetwalia mke bila ndoa toka mtaani na sasa naishi vyema tu!
 
mpaka mtu unamkuta kanisani iwe kwa kutafuta mchumba au vyovyote anafaa tu kua mke, sina sababu ya kuogopa
tusipowatafuta kanisani ni heri twende club maana labda huko kuna cream nzuri kulinganisha na makanisani
 
Very true Mkuu, wengi wa watu wanaoenda kushinda makanisa hasa haya ya ulokole ni wanafki sana. Zamani nilikua nikimuona demu mkali anasali makanisa ya kilokole namkimbia najua amekwisha ungua anatafuta muujiza.
miujiza
 
Haya maneno yenu ni kwenye magenge tu.

Huwezi toka huko nankujikoroga koroga kwako na dunia kisa unataka kuoa ndio ukatafutie kanisani, lazima utapata wa kufanana na wewe.

Mungu husema na wanaomcha yeye na kama unajitunza atakuonya na kukujulisha kuhusu mtu unayetaka kumuoa au kuolewa nae.

Haya mambo hayatambulikani kwa macho ya nyama, walio wa rohoni wanatambua.

Kwa kufurashisha genge inawezekana uko sahihi.
 
Huko kutafuta mke kanisani kuliishaniliiiza sitakaaa nisahau kumesababisha nimetwalia mke bila ndoa toka mtaani na sasa naishi vyema tu!
Yule dada alie kubwaga akazama kwa mtt wa mchungaji nae mtt wa pasta kala mzigo kaubwaga pwaaaa!!! Akatangaza ndoa na msupuu mwingine wa mkoan ...
 
Kweli tupu
 

Attachments

  • FB_IMG_15256896695252210.jpg
    FB_IMG_15256896695252210.jpg
    21.6 KB · Views: 67
Back
Top Bottom