Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

  • Thread starter Mzee Mwanakijiji
  • Start date

Status
Not open for further replies.
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,875
Likes
8,036
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,875 8,036 280
Tunataka kutetea demokrasia na utawala wa demokrasia, hivyo hatuwezi kuwa wa kwanza kupendekeza njia zisizo za kidemokrasia kushughulikia matatizo ya kidemokrasia. Tupo ambao tumechukizwa, kukerwa na kuumizwa na jinsi ambavyo matokeo ya uchaguzi mkuu katika ngazi zote yalivyotolewa na yanavyoendelea kutolewa na hasa mahali tulipofikia vijana wetu kulazimika "kulinda kura". Wapo ambao wanaona kabisa kuwa baadhi ya watu waliotangazwa au watakaotangazwa washindi wamekosa uhalali wa nafasi hizo.

Pamoja na ukweli wa hilo siku za karibuni kuanzia mvurugano wa Tume na Matokeo ya Uchaguzi nimefuatilia wapo watu wamejiunga ghafla ghafla au wengine wa muda kidogo ambao wamekuja na siasa kali za kutaka kutumia JF kama jukwaa la kuanzishia itikadi ya nguvu dhidi ya utawala wa kisiasa (violence against public officials).

Mimi binafsi nikiwa ni muumini wa nadharia ya nguvu ya hoja siungi mkono hoja za nguvu kwani katika kutumia hoja za nguvu kunathibitisha kuwa umeshindwa kutumia nguvu za hoja kuweza kuwashawishi watu wengine. Lakini ukweli ni kwamba, hadi hivi sasa tumeweza kwa kutumia hoja tu kujenga hoja na kuwashawishi mamilioni ya Watanzania kuchagua mabadiliko. Hatuna sababu ya kubadili mbinu hiyo sasa hata kama tunajisikia hasira kiasi gani.

Binafsi napinga na kulaani vikali kauli zinazotolewa aidha kama entrapment ya JF au kutoka moyoni kweli yenye kuashiria kuwa ni bora kutumia nguvu kuweza kupata matokeo ya kisiasa. Tulipoanza JF miaka michache iliyopita hatukujua kuwa uongozi wa kisiasa ungekuwa ulivyo, lakini tumeweza kupita katika misukosuko mingi ya kitaifa na tumeweza kufika leo tumeshuhudia mabadiliko makubwa na ushindi usiokadirika wa upinzani Tanzania na hivyo kusababisha malango yaliyofungwa kuachia. Huu ni ushindi wa hoja si vitisho.

Kama kundi ambalo baadhi yetu tunajiita au tunaitwa wasomi, ni lazima tuwe tayari kutetea hoja zetu nakutumia ushawishi wa hoja kuweza kupata matokeo ya kisiasa. Ninachosema ni kuwa tuwakatae kwa hoja wale wote wenye kujaribu kutushawishi au kutoa kauli za matumizi ya nguvu kama "laiti ningekuwa sniper", "tuwapige risasi"n.k ili waone kama kuna watu wataunga mkono - na inasikitisha wapo wanaounga mkono.

Kwa kufanya hivyo, tunaweka mtandao wetu tuupendao hatarini kwani kikiwa ni chombo kilichoandikishwa na licha ya watu kutumia majina mbadala endapo jambo fulani linatokea mtandao huu una wajibu wa kushirikiana na vyombo vya kiusalama kutekeleza amri halali ya mahakama kuweza kuwapata wahusika. Sasa tusichukulie kimzaha tunapotoa kauli zenye mfanano wa vitisho, kauli hizo hazilindwi na "uhuru wa maoni" kwani ni kama ilivyosema "kupiga kelele moto, kwenye ukumbi uliojaa".

Hivyo, kwa wale ambao tumekasirishwa sana na matokeo, tujitoe zaidi kujipanga katika vyama tunavyovitaka au kushiriki kuunga mkono au kuwasaidia wagombea waliochakachuliwa matokeo yao. Mtu akitoa kauli yenye mwelekeo wa vitisho kwa viongozi wa umma - haijalishi kama ni wa chama tawala au upinzani - nawaomba tuflag comment hiyo na kuwataarifu ma MOD mara moja. Tusidhania MODs wanasoma kila sentensi ya kila thread ya kila mtu kila siku. Tuwe walinzi wa forum yetu sisi wenyewe kwani ninaamini katika siku zijazo tutahitaji chombo hiki kuendelea kuwepo.

Tukumbuke kuwa ufisadi bado upo, mgongano ndani ya CCM upo na changamoto mbalimbali za kitaifa bado zipo. Hivyo, ni kwa maslahi yetu sisi wenyewe wanachama, wageni, na mashabiki kuulinda mtandao huu kutoka kwa watu ambao wengine naamini ni political operatives wa baadhi ya watu ambao kazi yao ni kupandikiza hoja za kichochezi ili JF itajwe (kama mnakumbuka Feb 2008) kuwa ni mtandao wa kighaidi au kichochezi. Maana ikifanyika hivyo wengi hutimka na kukaa pembeni huku wachache vichwa vyao vikiwekwa katika kamba za wanyongaji.

Tujiwajibishe wenyewe, tuilinde forum yetu..

Napendekeza.
 
F

Ferds

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2010
Messages
1,267
Likes
27
Points
135
F

Ferds

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2010
1,267 27 135
Asante kwa maneno ya busara mzee mwanakijiji, yanasaidia kushusha temper za wanajf
 
Abdulhalim

Abdulhalim

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2007
Messages
16,513
Likes
205
Points
160
Abdulhalim

Abdulhalim

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2007
16,513 205 160
Asenti.

Ushauri wako ni mzuri. Lakini ni vyema hao wanaodhulumiwa wa-document kesi yao kwa watz na watu wa nje ambao wanaolitakia mema taifa hili, ili kila kitu kiwe bayana. Kasi ya kumjua adui yetu haiezi kuendelea tukikosa platform muhimu kama JF, hilo halina ubishi. Sasa ni kazi yetu kulinda kile tulichonacho kabla ya ku-pursue makubwa zaidi.
 
W

We can

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Messages
681
Likes
5
Points
35
W

We can

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2010
681 5 35
Hata mimi sitegemei kama Dr. Slaa ataruhusu matumizi ya nguvu. Naamini atatumia ushawishi wake kuhakikisha kuwa umma unaelewa kinachoendelea kwa amani na kuiandaa hasira yao kwenye sanduku la kura October 2015. Hata hivyo, haya ni maoni yangu binafsi, yanaweza kupingwa kwa hoja.
 
FarLeftist

FarLeftist

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2010
Messages
362
Likes
9
Points
0
FarLeftist

FarLeftist

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2010
362 9 0
kweli Mkuu,
tunahitaji nguvu ya hoja na sio hoja ya nguvu
viva la JF
 
Saharavoice

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
2,708
Likes
267
Points
180
Saharavoice

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
2,708 267 180
Mzee Mwanakijiji, Naunga mkono hoja yako.
Binadamu hatuna tofauti na wanyama pale tunapogundua haki imeporwa tena siyo kwa bahati mbaya bali kwa dhamira iliyoandaliwa.
Lakini pia kukaibuka watu humu, sina hakika kama wametumwa ingawa post zao zilionyesha kabisa kwamba ziko kwa ajili ya kuchafua hali ya hewa humu ndani. Ilihitaji kuwa na moyo mgumu kustahimili na matokeo yake ni hayo tuliyoyashuhudia.

Tusonge mbele kuijenga JF yetu.
 
Victory 1

Victory 1

Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
21
Likes
0
Points
0
Victory 1

Victory 1

Member
Joined Nov 3, 2010
21 0 0
Asante sana Mwanakijiji kwa pendekezo lenye hekima na akili
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
197
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 197 160
unajua Mwanakijiji na silaha kubwa ya ccm nikujua kuwa waTz WANAPENDA SIASA nyepesi zisizo na movement kali, wanajua tutawangoja 2015, wataiba tena maana hawana hofu ya machafuko.
mimi nasema bila kuchakachuana hapa hakitaeleweka.
 
A

Akiri

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Messages
1,458
Likes
65
Points
145
A

Akiri

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2010
1,458 65 145
umenena mkuu, tutumie jamvi letu kwa manufaa ya Taifa letu, Jamvi hili limekuwa chanzo muhimu cha habari, naomba niwaombe wana Jf taarifa tunasoleta hapa zile na ushaidi ili tuzidi kujenga heshima yetu na tuonekane tunatumia vema taaluma zetu. Asante Mzee Mwanakiji
 
K

Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2006
Messages
1,221
Likes
110
Points
160
Age
49
K

Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2006
1,221 110 160
Bro!
You nailed it! Thanks so much for the Advice! We're moving Forward,ALUTA CONTINUA!
 
The Good

The Good

Senior Member
Joined
May 26, 2010
Messages
153
Likes
6
Points
35
The Good

The Good

Senior Member
Joined May 26, 2010
153 6 35
Mkuu I support you 100%.

Kuna wakati nimekuwa nikijiuliza hivi kweli JF ni HOME OF GREAT THINKERS au la. Kuna mambo kadhaa ambayo yameanza ku-dilute nguvu ya hii forum ntatoa machache.

1. Kutokubali mawazo m-badala.
Kuna tabia inayokuwa ya wachangaiaji wengi kuamini yoyote mwenye mawazo tofauti na yako basi yuko katika njia potofu. kwangu hili ni kosa maana lengo moja la forum hii ni watu kutoa mawazo yao kwa uwazi (pasi kuvunja sheria). Hivyo basi ili uweze kujipima usahihi wa mawazo yako mawazo tofauti na yako ni muhimu ili kuona kama kuna eneo ambalo umelisahau katika kujenga hoja ambalo linaweza kukupa mwelekeo mzuri zaidi.

2. Kushambulia watu zaidi kuliko hoja

Mara kadhaa tunasahau hoja na kumchambua mtoa hoja. Hii pia inapunguza umaarufu wa forum.

3. Kauli za jazba, vitisho na hata matusi
Busara za mtu huanza kupimwa kwa kauli zake maana matendo hujitokeza baadae baada ya kumjua mtu husika. Mtu mwenye natusi huonyesha upungufu wa busara.

My opinion:

JF inapaswa iwe chungu cha kupika hoja ambazo zinaweza kutumiwa na mtu yoyote ikiwemo wawakilishi na viongozi wetu katika kusukuma mbele Taifa letu.

Mgongano wa mawazo ni sharti la kwanza katika kujenga jamii imara. Lazima tujenge utamaduni wa kusikilizana. jamii lenye mawazo yanayofanana ni jamii mgando.

Naomba kuwakilisha
 
K

Kyachakiche

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2009
Messages
936
Likes
98
Points
45
K

Kyachakiche

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2009
936 98 45
Mkuu na mimi naunga mkono hoja ya utulivu na amani
 
M

Mugerezi

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2007
Messages
456
Likes
3
Points
35
M

Mugerezi

JF-Expert Member
Joined Mar 28, 2007
456 3 35
Mkuu ulichosema ni kweli kabisa. Tupambane kwa hoja siyo mashoka. Nami kwa upande wangu nimenotice kuna watu kweli wamejiunga mhh hoja zao zinatia shaka na pia niza upande fulani. Nadhani wako kwa kazi fulani. Kama ulivyosema tuwajibishane kikwelikweli. MAPAMBANO YA HOJA YAENDELEE MPAKA NCHI IKOMBOLEWE KUTOKA MIKONONI MWA MAFISADI.
 
October

October

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Messages
2,147
Likes
5
Points
135
October

October

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2009
2,147 5 135
Asante kwa ushauri wako MKJJ. Ushauri wako ni wa busara na nakuunga mkono 100%.

Ni muhimu hasira tulizonazo zisitupofushe na kusahau kuwa hali bora ya Watanzania ndio lengo letu kuu katika harakati zetu iwe wa CHADEMA au Chama kingine chochote chenye vision hii kwa taifa letu.

Ukweli ni kwamba vurugu yoyote itakayotokea italeta madhara makubwa zaidi kwa watanzania na wanaharakati wote kuliko itakavyotatua tatizo. Kwa muda mwingi nimekua mfuatiliaji wa JF na nimeona jinsi watu walivyojenga hoja za msingi ambazo zimeleta mtikisiko na mabadiliko katika serikali yetu.

Kwa msingi huu wa nguvu ya hoja CHAEDEMA na wanaharakati wanaweza kuwa na ushawishi zaidi katika hatima ya Tanzania kuliko kutumia nguvu jambo ambalo kwanza tutashindwa kwa sababu huwezi kuishinda serikali kwa nguvu, Pili harakati zatu zitapoteza ushawishi na support kwa jamii na marafiki zetu wa nje na ndani
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,741
Likes
2,026
Points
280
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,741 2,026 280
Kama kuna wakati wananchi wa kawaida tumepata ushindi, basi ni katika uchaguzi huu. Pamoja na malalamiko yote na matatizo yanayojitokeza, ni wazi kabisa ule uliokuwa ukuta wa chuma umeweza kukatika. Mara nyingi mtu mwenye jazba huwa anaweka matumizi ya akili yake pembeni.

Ili kuibadili nchi yetu hii tuweze kufika nchi ya maziwa na asali, fujo na vurugu haziwezi kutifikisha huko. Si busara kabisa kutumia njia ambazo zinachochea watu kuweza kufanya fujo.

Fujo zinaharibu mara nyingi zaidi kuliko kujenga.

Nakubaliana kabisa na hoja za kutoanza kujenga mazingira ya chuki na fujo. Huu ni wakati wa kutumia opportunities nyingi ambazo kura imezileta kwenye mwendo mzima wa kuwezesha mabadiliko.

Great thinkers lazima wawe mstari wa mbele wa kuonyesha njia sahihi ya kufikiwa kwa malengo bila kubomoa yale ambayo yameshafikiwa hivi sasa.
 
N

notradamme

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
2,012
Likes
3
Points
135
N

notradamme

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2010
2,012 3 135
Nilishawahi kusema humu ndani kwamba great thinkers ni wachache sana humu ndani. na sikuficha hisia zangu kuwa MZEE MWANAKIJIJI ni mmoja wao. Mwanakijiji, hili swala uliloliongelea ni zito,kubwa na lina ukweli uliopitiliza. ukweli ambao unaweza usiingie akilini kwa baadhi ya wana JF. humu kuna watu ambao hawauoni ukweli,wakiuona hawataki kuukubali na wakiukubali wanaupindisha kwa makusudi.

Swala la kuiweka hatarini JF pamoja na MOD nililiona muda mrefu sana, binafsi nililiongelea kwa mtazamo wangu MOD akanisimamisha uanachama na mwisho nikaamua kuachana na hii forum mpaka hivi punde nimejiunga upya.

Mwenye akili timamu atakuwa amekuelewa kwani article yako imejitosheleza sana na imekuja katika kipindi ambacho tunaelekea kuapishwa kwa raisi.Sina haja ya kusema ila nliwahi kusikia hivi karibuni kuwa MOD wa hii forum bwana MELLO ni miongoni mwa watu watakaoishi kwa shida sana katika kipindi cha miaka mitano ijayo. na hii ni kutokana na kuruhusu matusi, kejeli na uchochezi katika JF wakati akiwa MOD.

Nakuunga mkono kaka, bado tunaihitaji sana hii FORUM na hakika bila watu kujirekebisha kutumia jazba na matusi dhidi ya mamlaka zilizoshika mpini, ni wazi makali tuliyoshika katika huu mvutano yatatukata na kutuacha na majeraha.
 
Anyisile Obheli

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2009
Messages
3,378
Likes
138
Points
160
Anyisile Obheli

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Joined Dec 13, 2009
3,378 138 160
naunga mkono hoja!!
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,239,157
Members 476,439
Posts 29,344,215