Kwa kufanya hivyo, tunaweka mtandao wetu tuupendao hatarini kwani kikiwa ni chombo kilichoandikishwa na licha ya watu kutumia majina mbadala endapo jambo fulani linatokea mtandao huu una wajibu wa kushirikiana na vyombo vya kiusalama kutekeleza amri halali ya mahakama kuweza kuwapata wahusika. Sasa tusichukulie kimzaha tunapotoa kauli zenye mfanano wa vitisho, kauli hizo hazilindwi na "uhuru wa maoni" kwani ni kama ilivyosema "kupiga kelele moto, kwenye ukumbi uliojaa".
Mkuu ulisema lini wakati umejiunga juzi?na una post 7!wote wageni naona!lolNilishawahi kusema humu ndani kwamba great thinkers ni wachache sana humu ndani. na sikuficha hisia zangu kuwa MZEE MWANAKIJIJI ni mmoja wao. Mwanakijiji, hili swala uliloliongelea ni zito,kubwa na lina ukweli uliopitiliza. ukweli ambao unaweza usiingie akilini kwa baadhi ya wana JF. humu kuna watu ambao hawauoni ukweli,wakiuona hawataki kuukubali na wakiukubali wanaupindisha kwa makusudi.
Swala la kuiweka hatarini JF pamoja na MOD nililiona muda mrefu sana, binafsi nililiongelea kwa mtazamo wangu MOD akanisimamisha
uanachama na mwisho nikaamua kuachana na hii forum mpaka hivi punde nimejiunga upya.
Mwenye akili timamu atakuwa amekuelewa kwani article yako imejitosheleza sana na imekuja katika kipindi ambacho tunaelekea kuapishwa kwa raisi.Sina haja ya kusema ila nliwahi kusikia hivi karibuni kuwa MOD wa hii forum bwana MELLO ni miongoni mwa watu watakaoishi kwa shida sana katika kipindi cha miaka mitano ijayo. na hii ni kutokana na kuruhusu matusi, kejeli na uchochezi katika JF wakati akiwa MOD.
Nakuunga mkono kaka, bado tunaihitaji sana hii FORUM na hakika bila watu kujirekebisha kutumia jazba na matusi dhidi ya mamlaka zilizoshika mpini, ni wazi makali tuliyoshika katika huu mvutano yatatukata na kutuacha na majeraha.
Tujiwajibishe wenyewe, tuilinde forum yetu
Mwanakijiji una hopes za ajabu sana wakati mwingine hadu huwa nadhania hauishi kwenye dunia tuishiyo wengi.....(simaanishi kiubaya hata kidogo...ni kwamba nashangazwa na matumaini uliyonanyo)