Angalizo kwa wana JF - Lugha ya matumizi ya nguvu haina nafasi

Status
Not open for further replies.
Ni kweli kabisa, japo mi ni member mgeni wa kujiunga ila nimekuwa nikiitembelea hii forum muda mrefu, nimeona watu wengi wanapoona wanatumia majina mbadala wanatumia hoja za nguvu na kauli ambazo kwa mtazamo wangu ni hatarishi na zinawaweka ma mods pabaya.

Hivyo nina shukuru Mkuu kwa kutujuza na kutukumbusha wanaJF kwa ujumla kuwa tuwe makini kwenye kutoa hoja tukijua kuwa uhuru wa kuoa maoni si uhuru wa kuvunja sheria, na kwa technolojia ya sasa we can easily be traced no matter tunatumia majina mbadala.

Tusikubali JF iharibiwe na wasio itakia mema, kwani JF ime na ina endelea kutusaidia wengi, walio nchini na wasio nchini.

Umesikika na kueleweka!
Muulize huyo unayekubaliana naye CCJ iko wapi? yeye ndo alikuwa mshehereshaji mkuu wa CCJ. the spinning master.
 
Hoja nzuri na sisi wengine tumekuwa tunaliona wakati mwingine kulikemea lakini mtu anaamua kutukana sababu ya partisanship na kuwa na mawazo na mtazamo tofauti. Dhana ya kuwa JF is for great thinkers unatoka na jamii itaishusha hadhi na thamani forum yetu.

Wote Tunapaswa Kuilinda na Kuifanya Kila Mtu Awe na Shauku ya Kusoma JF kupata Mawazo ya Maana toka kwa Watu Wanaofikiri si Kuropoka Hata Mkuu wa Kaya awe Anaingia JF Mwenyewe Kusoma Mawazo ya Watu badala ya Kutafuta Mawazo Sehemu Tofauti
 
Hii thread kwa kweli nimeipenda. Mimi nimejiunga November tu na baada ya muda kidogo nilianza kupata hofu kuwa hapa sipo nilipota kuwa. Baada ya kuona wachangiaji wakitoa maneno ya kashfa kwa makabila mbalimbali hasa wamasai (kuna mtu aliwaponda sana kuwa ni wajinga). Nafarijika sasa kuwa hapa nilipo ndipo nilipotaka kuwa. Mwanakijiji hongera sana kuanzisha hii thread.
 
Mkuu I support you 100%.

Kuna wakati nimekuwa nikijiuliza hivi kweli JF ni HOME OF GREAT THINKERS au la. Kuna mambo kadhaa ambayo yameanza ku-dilute nguvu ya hii forum ntatoa machache.

1. Kutokubali mawazo m-badala.
Kuna tabia inayokuwa ya wachangaiaji wengi kuamini yoyote mwenye mawazo tofauti na yako basi yuko katika njia potofu. kwangu hili ni kosa maana lengo moja la forum hii ni watu kutoa mawazo yao kwa uwazi (pasi kuvunja sheria). Hivyo basi ili uweze kujipima usahihi wa mawazo yako mawazo tofauti na yako ni muhimu ili kuona kama kuna eneo ambalo umelisahau katika kujenga hoja ambalo linaweza kukupa mwelekeo mzuri zaidi.

2. Kushambulia watu zaidi kuliko hoja

Mara kadhaa tunasahau hoja na kumchambua mtoa hoja. Hii pia inapunguza umaarufu wa forum.

3. Kauli za jazba, vitisho na hata matusi
Busara za mtu huanza kupimwa kwa kauli zake maana matendo hujitokeza baadae baada ya kumjua mtu husika. Mtu mwenye natusi huonyesha upungufu wa busara.

My opinion:

JF inapaswa iwe chungu cha kupika hoja ambazo zinaweza kutumiwa na mtu yoyote ikiwemo wawakilishi na viongozi wetu katika kusukuma mbele Taifa letu.

Mgongano wa mawazo ni sharti la kwanza katika kujenga jamii imara. Lazima tujenge utamaduni wa kusikilizana. jamii lenye mawazo yanayofanana ni jamii mgando.

Naomba kuwakilisha
Nakubaliana na The Good kwa asilimia mia moja. Labda niongezee kwamba kusiwe na dhana kwamba JF ni forum ya CHADEMA tu, hivyo mtu akija na hoja tofauti (isiyopendwa na CHADEMA) inakuwa " ....NA HUYU KATOKEA WAPI?..."
 
Lugha za kutumia nguvu ni kweli zinahatarisha legitimacy ya JF, ila kwa upande wa pili wa shilingi kujadili yale ambayo yapo vichwani mwa wananchi mitaani bila ya sisi kuwa chanzo cha lugha hizo(kikubwa ni sisi kuacha uzushi) ni msaada mkubwa kwa nchi yetu kwa kufikisha hali halisi on the ground kwa law enforcements and dictatorial policy makers japo wana mashushushu wao ila nina hakika somtimes huwa hawana precisions inayotakiwa hasa pale information inapokuwa analysed kama genuine au nomal blah blah.

Tuliport matukio kama yalivyo kwani nina hakika JF ni sample ya watanzania wengi wenye mapenzi mema kwa nchi yao ambao wasingependa kuiona siku moja ikiteketea bali kuwa strong and properous kwa kuwawajibisha watu wanaoweka vikwazo kwa ustawi wetu kwa kuweka masilahi yao mbele hata kama ikibidi Tanzania iangamie, hao tusiwape nafasi tuwafichue kwa ukweli na uwazi kwa lengo la kujenga na si kubomoa.
 
Well articulated observation for all JF columnists on the importance of maintaining self-sensorship among ourselves.
 
nafikiri maana ya kutumia nguvu ni pale unaposhinwa au kuchoka na hamna mabadiliko,nguvu lazima nchi hiiiiii,ndio solution manake ccm kutoka na wameshindwa kuleta mabadiliko sio rahisi,tupo tayari kutumia nguvu kama libya!!!!!!!!!!!!!
 
Muulize huyo unayekubaliana naye CCJ iko wapi? yeye ndo alikuwa mshehereshaji mkuu wa CCJ. the spinning master.
Dah... Biggy umenikumbusha CCJ, mtoto aliyefariki mara tu baada ya kuzaliwa... kweli uzazi salama bado ni tatizo kubwa sana hapa tanzania, tulimpoteza mtoto huyu kutokana na mama kukosa huduma ya haraka ya uzazi alama kwenye hospitali za kata
 
i dont think the current leaders will initiate a change, i have spoken to Ministers and a number of CEOs in Tanzania, everyone is afraid of 'change' as you would expect from old people;

Their generation needs to go and then our generation will enact change; and i dont think we even need to plan for change; Whether we like it or not, CHANGE WILL COME!

NOTE The Following:-

many young people, who are coming up in the government are thinking differently, the technology is catching up, the way of thinking is MUCH way advanced, you cant think of inheriting the power, the World has become like a village, people are empowered, people are willing to voice their desires.. if you look around the Worldthings are changing and Tanzania is not left behind, so,
CHANGE is inevitable! :poa
 
Mzee Mwanakijiji,
Mawazo yako ni Mazuri sana kwa nchi zilizostaraabika.
Tumeshuhudia Rockycity Nyamagana na Ilemela wananchi ilibidi watumie nguvu na kulala City Hall kulinda na kutaka matokeo halali ya kura yatangazwe.

Ubungo hali kadhalika hali haikuwa njema, nakumbuka Mh,Mnyika alifanya kazi ya ziada kuhakikisha Simu yske iko hewani masaa yote ikikusanya na kutoa taarifa kwa wapenda mabadiliko.

Jimbo la Shinyanga Mjini pia matokeo yamebakwa, CCm ilishindwa hadi Jumatatu jioni Chadema walikuwa wasensema Shytown huku wakiimba Peoplesss Power kwa ushindi wa mbunge wao, Lakini Usiku huo wa Jumatatu From no where kichaa fulani akalazimisha matokeo yatangazwe kuwa Marehemu Shilembi amashindwa kwa kura moja.(Inatuuma sana Wanashinyanga ktk hili,)

Ofcourse mazingira ya fujo yapo ila umesahau kuna watu wanaotengeneza mazingira hayo tete ili watu wachukie.
Mwanakijiji, Ukimchekea Nyani utavuna Mabua huo ndio ukweli.
Kanda ya ziwa tutaendelea kulinda kura zetu bila kurusha jiwe kwa yeyote lakini hatutakubali kuibiwa kura zetu. Tumejipanga hata Arumeru Mashariki tutatoa Msaada. Hadi kieleweke.
Nawasilisha
 
''Tupo pamoja Mwanakijiji Naunga mkono Hoja.Jambo la msingi ni umoja na mshikamano katika hoja ili kupambana na kila aina ya uovu unaofanywa na jamii tawala.Pia chamsingi tukumbuke, Hakuna Utawala wenye nguvu duniani Dhidi ya wananchi endapo wakiamua. Hivyo selikali haina budi kutumikia wananchi kama katiba Inavyo Iongoza sheria kwamaana hiyo, matumizi ya nguvu hayana nafasi katika nchi yenye Selikali sikivu.'' Wa Tanzania tupambane kwa hoja Kabla ya nguvu'' Hongera JF kwa hapa mlipo tufikisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom