KipimaPembe
JF-Expert Member
- Aug 5, 2007
- 1,285
- 696
Kwa wachangiaji wengi makini hapa JF hiki kilikuwa kipindi cha kupumzika kwa sababu kuna wengine wameigeuza forum kuwa battleground pengine kwa kujua au kutojua! Kwa kweli michango mingi humu ndani wakati wa kampeni na wakati wa matokeo ilikuwa terrible na unaweza kusema uhuru wa habari uliopitiliza kama ulioonekana humu unatia kichefu chefu. Watu tuna tofauti, lakini viwango vya ustaarabu havitofautiani sana.
Vile vile kuna watu wameamua kutumia kipindi hiki cha uchaguzi kuchafua hali ya hewa na kuifanya social media kama Jamii Forums ionekane kama kitu kisichofaa! Pengine hawa walikuwa wengi sana kipindi hiki, na wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwa-put off watu wengi wanaoiona jamii forums kama channel muhimu ya kupata habari na fikra huru zisizo-haririwa.
Mimi nashauri members wapya sana wawe wanapewa nafasi ya kuona content tu bila kupewa ruhusa ya kuchangia. Member mpya akisajiliwa awe anapewa kama One month ya kukaa kama observer kabla ya kuruhusiwa ku-post kitu chochote kwenye forum. Nahisi kuna watu humu wakiona hoja zinazowashinda hukimbilia kujisajili kwa ID mpya na kuvuruga mijadala yenye hoja hizo. Hili linawezekana kutokana na urahisi wa kujisajili upya na kuanza kuchangia. At least masharti haya yanaweza kuwekwa katika baadhi ya majamvi tu, sehemu kama mapenzi na mahusiano watu waruhusiwe kujimwaga.
Ni kweli mijadala mingi isiyokuwa na lugha za kistaarabu inavuruga sana forums na kufanya wale wanaoitegemea kuchukia na kutafuta alternative source.
Siasa ni mchezo msafi, kwani siasa hutoa viongozi wanaotakiwa kuwaongoza watu. Si ajabu kuwa nchi yetu inaendelea kuzama katika lindi la umaskini, ikiwa tunaendelea kuichukulia siasa kama ni sehemu ya kutumia hila, fitna na uzandiki kiasi cha watanzania kuaminishwa kuwa siasa ni MCHEZO MCHAFU. Mchezo mchafu, hauwezi kutoa washindi wasafi. Taifa linatakiwa kuongozwa na watu wasafi. Lazima tuseme kuwa siasa zetu tunaziendesha vibaya ndo maana matokeo yake ni mabaya kwetu wote.
Tunataka mabadiliko, lazima tutumie njia safi ili kujitenga na wanaotumia njia mbovu. Tunajua fitna na hila zitaendelea kuwepo na kwa kipindi fulani zitaonekana kushinda. Lakini dawa yake ni kuzikataa hila na fitna sehemu yoyote tunapopata nafasi ya kufanya hivyo, hatimaye ukweli utasimama. Kujaribu kumuondoa nyoka ndani ya nyumba kwa kuichoma moto inaweza isiwe uamzi wa busara sana!