Angalia mwongozo wa kanuni uliyowachinja Wapinzani

Hapo Na.9 Hapo walikuwa wanahamasishana wasijiandikishe, nadhani Halima Mdee na mtu pekee aliyepaona! Sasa kituko unashawishi watu wako wasijiandikishe, halafu unatoka hapo unaenda kugombea, sasa sijui nani atakuchagua.
Hapo ndipo nikishangaa; yaani mtu anahamasisha watu wasijiandikishe Alafu yeye anawahi kujiandikisha
 
CCM waliwapa wagombea wao semina elekezi jinsi ya kujaza wapinzani wakabaki mitandaoni kulalama sasa wamejaza vidole juu wamekosea wanalia .

Panueni akili sio vidole

State agent
Mie nilishuhudia ccm walipeana semina namna ya kujaza form na walikutana na kujaza kwa pamoja mbele ya viongozi wao,lkn chadema wao walikua wakijaza mmoja mmoja.anavyoona inafaa
 
Ujinga wa ccm na viongozi wao bana unatia aibu!! Hivi inawezakanaje wagombea wote wa vyama pinzani kukosea fomu?? Kwamba ccm wao wako Safi wote Nchi nzima??. Kweli Nape alikuwa kichwa Sana na aliyetumia akili nyingi kuudhoofisha upinzan kwa akili nyingi kuliko nguvu za haya matahira
Nape Alikua anatumia njia gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ugumu utukuja katika kuwaongoza waliokukataa kisha ukapitishwa na dola.
Wangeacha uchaguzi uwe huru na wa haki.
Katika maisha halisi huku mpinzani akikidhi vigezo yanafanyika mawasiliano kuanzia mtendaji wa kijiji hadi hatua ya mwisho kuuliza nini kifanyike na viongozi wanachanganikiwa mno.
Watendaji wametishwa vibarua kuota endapo atapita mpinzani.
ila mimi binafsi sioni hofu ya serikali yetu inatoka wapi dhidi ya upinzani wakati kila mtanzania anaona juhudi za serikali kuboresha maisha ya watanzania,
Ndege nchi nzima madaraja ya juu maji na umeme vijijini hospitali za kutosha ingawa tukifika tunapewa tu ushauri au vipimo vya malaria dawa tunaelekezwa famasi.
Watumishi wanaongezewa madaraja kwa wakati mfano wengine tangu ajira ya 2013,2014 hawajawahi kupata nyongeza wala daraja.
Kiujumla serikali imefanya mengi sana mazuri na madhaifu kwa kuwa viongozi wetu ni binadamu hayakosekani.
Silaumu ila kuna umuhimu somo la Uraia kufutwa mashuleni. Sababu naona halina maana tena kwa kuwa tumepata viongozi bora wanaojali matumbo yao. Nieleweke namaanisha matumbo ya wananchi wao ni ya kwao pia.
Umuhimu wa vyama vya upinzani n.k
Ngoja niendelee kupalilia mahindi yangu ya vuli kwanza yaliobaki baada ya mengine kusombwa na mafuriko.
Pia nisisahau kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutuletea mvua za kutosha kule kwetu Tanga na maeneo ya jirani.
 
Mfano huku niliko mimi wamekatwabkaribia 95% na ukiangalia kanuni wamekatwa kihalali kabisa
Bado huelewi.Uongozi siyo vita.Wagombea hupewa vitabu vya mwongozo kupitia viongozi wa vyama hii ni kwa mjibu wa tume sasa hiyo tume inawahusu ccm tu?.
Tumia akili kidogo tu siyo nguvu kuujua ukweli.
 
Wakuu Hivi makopo kama Huyu bwana wanazalishwa kiwanda gani?
Maana halifai hata kuweka chooni kwa kuchambia.
 
Kwa hizo kanuni zilivyo na vichwa vya wapinzani wengi vilivyo wengi vilivyo vibovu watakuwa wamekosea Sana kujaza

Uzuri wa level ya watu wetu linapokuja suala la uelewa wana viwango vinavyofanana, na sio kwenye kuandika tu bali ni kwa mambo karibia yote kuanzia shughuli za kiuchumi mpaka ujengaji hoja. Ukitaka kujua ninachosema, chukua wote waliochukua fomu za kugombea, kisha fananisha maisha yao kwa ujumla, uone kama hao wa ccm wanautofauti mkubwa kiasi hicho kulinganisha na hao wa upinzani. Au ubora wa hao wanaccm uko kwenye kujaza fomu tu? Wakati mwingine watu weusi tunakuwa na ujinga mpaka unapitliza. Kibaya zaidi unakuta ushenzi huu wa wazi unaongozwa na wasomi. Kisha wazungu wakituita manyani tunaishia kulialia kuwa tumetukanwa.
 
Naomba niweke sawa hii Kitu!

Iko hivi.

Msajili wa Vyama Vya siasa katika Kumbukumbu zake,hana Chama Kinachoitwa "Chadema" bali ana "Chama Cha Demokrasia na Maendeleo" wala hana "CCM" bali ana "Chama Cha Mapinduzi"

Ndio Maana CCM tulikuwa na Semina Elekezi ili kukumbushana Mambo kama haya na Moja nilishiriki Kama Mgeni Mualikwa!

Ni Kweli Chadema Mmekosea Ujazaji wa Fomu zenu!nimeona fomu moja hadi nikaishia tu kucheka!!Sijui ni kwa sababu hamjui Chama Chenu kinaitwaje?!

Hii ni Legal Technicalities!Kisheria hakuna Chama Kinaitwa "CHADEMA" Wala hakuna Nafasi inayogombewa inaitwa "Mwenyekiti" kulikuwa na nafasi ya "Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa"wewe Unajaza "Mwenyekiti" Daah!!Poleni Watani zangu!

Chama Cha Mapinduzi na Maafisa wake walitimiza Majukumu yao kuwakumbusha wanachama kuhusu miongozo ya Chama wakati huo nyie mlikuwa mnapiga tu Porojo Mitandaoni,hamkuwa na Semina Elekezi??

Mmekosea Kweli na tusubiri Miaka mitano ijayo tukutane tena!!

Asante.

C&P
Mie pia nimeona fomu za chadema , makosa km hayo yamejitokeza sana
 
Mie nilishuhudia ccm walipeana semina namna ya kujaza form na walikutana na kujaza kwa pamoja mbele ya viongozi wao,lkn chadema wao walikua wakijaza mmoja mmoja.anavyoona inafaa
Ccm wamejaza chini ya viongozi na wanasheria ktk fomu zile tatu mmoja wamejaziwa ila kwa ukalamushi wao ccm na hili zoezi lilifanyika kwa umakini mkubwa mno
 
Vyama vingi wala havifutwi,kinakufa chama cha kijani.

Ukiona wanatumia nguvu kupita kiasi ujue mbinu zote za ki akili zimekwisha.
ccm wafwa!!!!!

Huu ndio ulikuwa muda mwafaka kujitadhimini kama je wananchi wanawaelewa or not
 
cant happen kwa your mere wish....
Hivi unajua nguvu ya umma wewe. jamii ikiamua utahama usiku na familia yako unadhani gadafi alipenda jificha kwenye daraja

Nyie jidanganyieni jamii ikibadilika yule mzee pale magogoni atatamani apige mbuzi baharia ya Hindi atokee Zanzibar achana na nguvu ya umma tena muache michezo yenu yakishezi inauma sana

Mtaani maisha magumu mfumuko wa bei kila kukicha nyie baada ya kuangalia mnatatua vipi changamoto mpo sijui fly over, sijui ndege sijui CAG ujinga ujinga tu
 
CCM waliwapa wagombea wao semina elekezi jinsi ya kujaza wapinzani wakabaki mitandaoni kulalama sasa wamejaza vidole juu wamekosea wanalia .

Panueni akili sio vidole

State agent

Wakati wapinzani wanapanua akili, wewe panua miguu ili waache kulalama, watanyamaza
 
Mchezo mzima unajulikana wewe dada....watendaji wamelazimishwa kufuta majina ya wapinzani
CCM waliwapa wagombea wao semina elekezi jinsi ya kujaza wapinzani wakabaki mitandaoni kulalama sasa wamejaza vidole juu wamekosea wanalia .

Panueni akili sio vidole

State agent
 
Duuuh!, kujaza form tu kanuni zote hizo hapo bado za kampeni, washinda mitandaoni lazima wakamatwe maana hawana mda wa kukumbuka kanuni zote hizo.
 
Binafsi sioni sababu ya kumnyima mtu haki ya kugombea kisa hakujaza form vizuri.
Ukisha kua na nia mbaya unaweka vitu kimtego mtego. Ungetegemea kama nia ni ushindani kungekuwa na muda wa kutosha wa kurekebisha palipokosewa. Hawa walivyokuwa washenzi wanakimbia ofisi, wanabadilisha kilichoandikwa, wanakataa tu na kusema fomu ina kosa ili mradi rabsha rabsha.
Korogwe uchaguzi mdogo (mwaka huu) vyama zaidi ya vitano kwa masaa zaidi ya matano hawakujua wapi kwa kurudisha fomu isipokuwa wa CCM. Na Kaijage na Kihamia waliamini hivyo (mmoja akiwa jaji na mwingine PhD holder).
Filikunjombe (2015) alituaminisha kuwa amepita bila kupingwa, kumbe walikwenda na kung'oa fomu za mgombea wa CDM. Na kijana aliyepokea fomu alipotoa msimamo basi wakaamua kumshughulikia. Uzuri aliamua kwenda kusoma masters yake na bahati nzuri au mbaya mheshimiwa akaitwa na Mola wake.
 
Kuna wanaccm mahal8 wamekosea kujaza form balaa. Sasa waneambiwa warudi kujaza form upya ili wapinzani wakitaka kuziona basi wawe na ushahidi...
 
Back
Top Bottom