Android inauza simu mara 4 zaidi kuliko Apple kila mwaka, lakini Apple inaongoza kwa mapato

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mwaka 2025, Android ilisafirisha simu 1,000,000,000 huku iPhone ikisafirisha 240,000,000, hivyo kwa idadi ya vifaa Android iko ligi tofauti kabisa. Hata hivyo, bei ya wastani ya iPhone ni dola 1,060 sawa na Tsh. 2.756 Milioni, ikilinganishwa na dola 370 sawa na Tsh 962,000 kwa simu za Android, jambo linalobadilisha kabisa taswira ya mapato.

SnapInsta.to_632362798_18194632621352449_8243384642796716933_n.jpg
Apple na Samsung zinadhibiti asilimia 40 ya mauzo ya simu janja duniani, ikionyesha kuwa soko limejikita zaidi kwa kampuni chache zilizo juu.

Hata hivyo, Nchini Marekani, iPhone ina umiliki wa asilimia 69 ya soko, hali inayompa Apple nafasi ya kuendelea kuuza bidhaa zake kwa bei ya juu

Maoni ya mdau

Apple Inc anamiliki simu (Kifaa) na Program Software (iOS) vyote ni vyake. Android hamiliki kifaa (Simu), vifaa (Simu/tablets) ni mali za watu wengine Samsung/Tecno/Infinix n.k.

Android anauza Software peke yake. Apple Inc lazima wawe na kipato kikubwa sababu wamedhibiti bidhaa zao, huwezi ipata iOS nje ya iPhone, lakini unaweza ipata Android nje ya Samsung/Tecno/Google pixel n.k.

Apple Inc lazima wauze bidhaa zao bei juu, sababu hakuna mbadala wa bidhaa zao (Yaan OS na Simu yaani iPhone). Android unaipata kwa wazalishaji wa simu wengi wenye kushindana.

Ingekuwa iOS inapatikana kwingine nje ya iPhone, kungekuwa na mbadala wa kifaa. Huna iPhone hujatumia iOS. Android is everywhere.
 
Apple Inc anamiliki simu (Kifaa) na Program Software (OS). Android hamiliki kifaa, vifaa (Simu/tablets) ni mali za watu wengine Samsung/Tecno/Infinix n.k.

Android anauza Software peke yake. Apple Inc lazima wawe na kipato kikubwa. Android ni third party sio mzalishaji wa simu.
Hii hesabu ni ngumu pia umetumia nini kusolve Periodic Table au 4 Figure?
 
Hesabu ndogo sana hii, hao Samsung, VIVO, Oppo hawawezi kuwa na mapato sawa na Apple, sababu unachokipata kwa Samsung (Android OS) unaweza kipata pia kwa OPPO/VIVO. Huwezi tumia iOS nje ya iPhone. Huna iPhone huwezi tumia iOS. Ukiwa na Samsung, OPPO, VIVO unaweza tumia Android. Samsung hapati mapato kwa kupitia Android, anapata mapato kwa kupitia Simu. Apple anapata mapato kote kwenye simu na kwenye iOS, maana vyote ni vyake. 😁
 
Kwenye laptop

Sasa umeshatoka kwenye lengo mkuu! Laptop sio simu, convenience unayoipata kwenye iOS ikiwa kwenye Laptop tofauti na iOS ikiwa kwenye simu. 😁
Ni sawa na wale wanatumia Mac kuweka window 10. 😄

Tafuta simu nje ya iPhone, utumie iOS mkuu. Tehe tehe tehe
 
Apple Inc anamiliki simu (Kifaa) na Program Software (iOS) vyote ni vyake. Android hamiliki kifaa (Simu), vifaa (Simu/tablets) ni mali za watu wengine Samsung/Tecno/Infinix n.k.

Android anauza Software peke yake. Apple Inc lazima wawe na kipato kikubwa sababu wamedhibiti bidhaa zao, huwezi ipata iOS nje ya iPhone, lakini unaweza ipata Android nje ya Samsung/Tecno/Google pixel n.k.

Apple Inc lazima wauze bidhaa zao bei juu, sababu hakuna mbadala wa bidhaa zao (Yaan OS na Simu yaani iPhone). Android unaipata kwa wazalishaji wa simu wengi wenye kushindana.

Ingekuwa iOS inapatikana kwingine nje ya iPhone, kungekuwa na mbadala wa kifaa. Huna iPhone hujatumia iOS. Android is everywhere.
iPhone pia ana simu za bei rahisi Ila hazinunuliwi Sana kama simu za bei ghali, advantage yao kubwa ni location Yao, wapo kwenye soko ambalo uchumi wao ni mkubwa. Ingekua ni Africa watu wangenunua iPhone 16E zaidi ama 16 plain kuliko 17 pro max.
 
Ukisha weka Apple vs Android tayari andiko lako linakua na WALAKINI mkubwa sana kimantiki
 
Mleta maada angalau angesema iphone vs google pixel(android) na sio android kiujumla maana kwenye soko la smartphone na tablet android amenyumbulika kwenye vifaa vya kampun tofaut tena zinazoshindana android kwa android tofaut na iphone(ios)hainyumbuliki kupitia kampun tofaut za kishindan
 
Back
Top Bottom