Ndugu zangu,
Nimeona jana kwenye Tv Andrew Chenge akiwa Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge.
Katika mazingira ya sasa, kile cha jana kilipaswa kiwe kikao cha mwisho Andrew Chenge kukiongoza.
Maana, kwa mizoga hii tuliyoonyeshwa kwenye kabati la Chenge, inahitaji ujasiri wa kifisadi kuendelea kukalia kiti cha uenyekiti kuwaongoza Wabunge wa Jamhuri. ' August Session' ni moja ya vikao vya Bunge vyenye hadhi kubwa.
Haviwezi kuongozwa na mtu mwenye tuhuma nzito za ufiaadi na ni dhihaka kubwa kwa Jamhuri inayoongozwa na Rais aliyechaguliwa na aliyesema makubwa jana yenye kumhusisha Chenge pia.
Mimi nadhani, ni wakati sasa, kama Chenge hatajiuzuru mwenyewe nafasi ya uenyekiti Bungeni, Kamati ya Uongozi ya Bunge imshinikize kufanya hivyo. Kazi hiyo si lazima aifanye Kiongozi Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni, Waziri Mkuu.
Maggid Mjengwa.
Picha: Gazeti Mtanzania.