Andrew Chenge sasa aage na kuondoka...

Andrew Chenge sasa aage na kuondoka...

Hahahhh Mkulu ana mtindo wa kubadilishabadilisha kauli! Kesho anaweza akasema vinginevyo acha tuone tutaishia wapi! Amesema ni kazi ngumu lakini kama Mungu amemweka basi ataifanya kwa kumtegemea Mungu. Katiba Mpya ndio suluhu ya yote haya period!
Ukiona mwanasiasa mpigaji anamtaja taja Mungu ujue anajivuta kutafuta atatokaje hapo. Hataki kujibu kwa sababu anamjua Magufuli kichaa hachelewi kumdadilikia.

Magufuli atapozwa tu. Hawezi kumvua nguo Mkapa.

Chenge anajiamini uwezo wake meenyewe moaka kasahau kwamba kuna kitu kinaitwa ukweli au ubaya.

Kwa sababu anaamini anaweza kupindisha kila kitu kiende anavyotaka yeye.
 
Kama kuna Mhe. Mbunge yeyote aliyetajwa kwenye Sakata la madini jana na ni miongoni mwa Wenyeviti wa Bunge letu ni vyema kama yupo AKAJIUZULU na asikae pale mbele akiongoza vikao. Huku Mitaani wananchi hawafurahishwi kabisa na jinsi tulivyoibiwa wakati wengine bado wanadumu kwenye Bunge letu.
 
Hivi kweli kwa tuhuma zote hizo alizo nazo na hii ya madini,anawezaje kusimama mbele ya bunge na kuwatetea wananchi wa jimbo lake kuwa wanadai hiki na kile wakati pesa ambazo serikali ingepata amezichukua yeye na wenzie wachache,hii si kuitukana serikali kweli? Sehemu ambazo serikali inategemea kupata hela ili waweze kuwasiliza vilio vyenu nyie wabunge ndo mnazichota bila sura ya haya na bado posho ya siku bungeni.Ila mungu anawaona mjue,na siku zenu zimekwisha.
 
ndie nahondha wa timu.. mnaweza kuwa mnacheza ili mpate ushindi kumbe wengine wameuza timu
 
HUYU MZEE NI MSUKUMA ASEE KAAGA VEMA KWAO KAMA BASHITE
 
Safari hii kobe kaliwatiming....mwenyewe anajielekeza kibla.
 
Ndugu zangu,

Nimeona jana kwenye Tv Andrew Chenge akiwa Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge.

Katika mazingira ya sasa, kile cha jana kilipaswa kiwe kikao cha mwisho Andrew Chenge kukiongoza.

Maana, kwa mizoga hii tuliyoonyeshwa kwenye kabati la Chenge, inahitaji ujasiri wa kifisadi kuendelea kukalia kiti cha uenyekiti kuwaongoza Wabunge wa Jamhuri. ' August Session' ni moja ya vikao vya Bunge vyenye hadhi kubwa.

Haviwezi kuongozwa na mtu mwenye tuhuma nzito za ufiaadi na ni dhihaka kubwa kwa Jamhuri inayoongozwa na Rais aliyechaguliwa na aliyesema makubwa jana yenye kumhusisha Chenge pia.

Mimi nadhani, ni wakati sasa, kama Chenge hatajiuzuru mwenyewe nafasi ya uenyekiti Bungeni, Kamati ya Uongozi ya Bunge imshinikize kufanya hivyo. Kazi hiyo si lazima aifanye Kiongozi Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni, Waziri Mkuu.

Maggid Mjengwa.

Picha: Gazeti Mtanzania.
Wakuondoka sio Andrew Chenge, wakuondoka ni the Whole CCM na systems zake watupisheeee nchi wanaimaliza halafu wanajifanya wao ndio waokozi, shame on you miCCM.
 
Hakuna mwanaccm mwenyewe kuweza kumgusa chenge Labda akubali mwenyewe kukaa pembeni
 
Ndugu zangu,

Nimeona jana kwenye Tv Andrew Chenge akiwa Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge.

Katika mazingira ya sasa, kile cha jana kilipaswa kiwe kikao cha mwisho Andrew Chenge kukiongoza.

Maana, kwa mizoga hii tuliyoonyeshwa kwenye kabati la Chenge, inahitaji ujasiri wa kifisadi kuendelea kukalia kiti cha uenyekiti kuwaongoza Wabunge wa Jamhuri. ' August Session' ni moja ya vikao vya Bunge vyenye hadhi kubwa.

Haviwezi kuongozwa na mtu mwenye tuhuma nzito za ufiaadi na ni dhihaka kubwa kwa Jamhuri inayoongozwa na Rais aliyechaguliwa na aliyesema makubwa jana yenye kumhusisha Chenge pia.

Mimi nadhani, ni wakati sasa, kama Chenge hatajiuzuru mwenyewe nafasi ya uenyekiti Bungeni, Kamati ya Uongozi ya Bunge imshinikize kufanya hivyo. Kazi hiyo si lazima aifanye Kiongozi Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni, Waziri Mkuu.

Maggid Mjengwa.

Picha: Gazeti Mtanzania.

Sidhani kama Mh Chenge ana mshipa wa aibu, aliwahi kujifananisha mwenyewe na nyoka mwenye makengeza kwamba ni hodari wa kuona fursa (hakufafanua kama ni za kifisadi au la) na kuzitumia! Watu kama hawa ni kuwalaximisha kuwa na aibu hata kwa kutumia mfumo usioonekana kwa wengi!!!
 
HUYO NDIE JOKA LA MAKENGEZA SPIKA MWENYEWE HAMGUSI KWA CHOCHOTE NA UZURI WAKE YEYE SIE MUONGEAJI KAMA WENGINE WANAVYOPAYUKA,,REJEA SAKATA LA ESCROW ALIVYOITWA KUHOJIWA KAMA KUNA AMBAYE ALITHUBUTU KUMUULIZA SWALI..HAMNA WA KUMGUSA HUYO
 
wote walio husishwa kwenye uhujumu wa rasilimali za nchi yetu wachukuliwe hatua za kisheria bila kuwaonea aibv!!

kujiuzulu pekee haitoshi bali hatua za kisheria ndio stahili yao!!! tunaomba kama mhe rais alivyo sema wachunguzwe na hatua zichukuliwe!

acacia walipata jeuri na kiburi kutokana na madalali hao wa rasilimali zetu, hawafai hata kuitwa watanzania.
 
Huyu naye hafai kwani amewahi kuingia mitini na rambirambi za mke wa marehemu Daudi Mwangosi (R.I.P)
 
Ndugu zangu,

Nimeona jana kwenye Tv Andrew Chenge akiwa Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge.

Katika mazingira ya sasa, kile cha jana kilipaswa kiwe kikao cha mwisho Andrew Chenge kukiongoza.

Maana, kwa mizoga hii tuliyoonyeshwa kwenye kabati la Chenge, inahitaji ujasiri wa kifisadi kuendelea kukalia kiti cha uenyekiti kuwaongoza Wabunge wa Jamhuri. ' August Session' ni moja ya vikao vya Bunge vyenye hadhi kubwa.

Haviwezi kuongozwa na mtu mwenye tuhuma nzito za ufiaadi na ni dhihaka kubwa kwa Jamhuri inayoongozwa na Rais aliyechaguliwa na aliyesema makubwa jana yenye kumhusisha Chenge pia.

Mimi nadhani, ni wakati sasa, kama Chenge hatajiuzuru mwenyewe nafasi ya uenyekiti Bungeni, Kamati ya Uongozi ya Bunge imshinikize kufanya hivyo. Kazi hiyo si lazima aifanye Kiongozi Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni, Waziri Mkuu.

Maggid Mjengwa.

Picha: Gazeti Mtanzania.
Ajiuzulu kwa tuhuma ambazo hata hajapewa nafasi ya kuzijibu?

Tukienda hivyo kamwe hatutafika
 
Nyie watu wa ajabu kweli kweli

Kwamba ndio mmejua leo kuwa Chenge hafai?

Mlivyomchagua kuwa mwenyekiti wa Bunge kwa kura nyingi za wabunge wa CCM hamkujua?

Hebu msituchoshe na msitufanye wajinga kwa makosa yenu mnayofanya kila siku.

Waingereza walirudisha chenji ya Rada Bil 40 na ushee na SFO ikasema kabisa Chenge amehongwa...Mlifanya nini?

Msituchoshe wezi nyie CCM

Freeland uko sahihi hapa. Huyu mleta mada ni kati wale wanaopenda sana kucheza mdundiko wa wanasiasa kama huu wa makanikia.

Kwanza baada ya kulitosa Azimio la Arusha baharini kwa kupitia Azimio la Zanzibar, CCM ilikumbatia sera za uliberali mamboleo (neo-liberalism) ambazo zinahimiza ubinafsishaji holela na utandawazi (tamka 'utandawizi') kama hili ya kukabidhi rasilimali za nchi kwa makampuni ya kibeberu (multinationals).

Pia sera za uliberali mamboleo zinataka serikali ijitoe katika utoaji wa huduma za kijamii kama elimu na afya kwa kuzifanya hizi huduma kuwa bidha kwa ajili ya wenye pesa tu. Na ndio maana elimu na huduma bora za afya hapa nchini ni kwa ajili ya wenye pesa 'ndefu' tu.

Chini ya hizi sera za uliberali mamboleo, serikali inakuwa ni wakala (comprador) tu wa mataifa ya kibeberu na makampuni yake.

Sasa Chenge hawezi kufanywa lolote kwa sababu yeye kama mtumishi wa serikali na baadaye kama kada wa chama tawala alichofanya ni kutekeleza sera za chama chake ambazo hazijabadilika hadi leo hii.

Kwa upande mwingine, kwenye hili suala la Acacia na makanikia, Magufuli ana malengo yake tofauti ya kisiasa nje ya 'rasilimali zetu kuibiwa'. Kumbuka hiki ni kipindi cha bunge la bajeti na serikali yake imefeli vibaya katika kutekeleza bajeti ya 2016/17.
 
Kama ccm wako serious wamvue uanachama Mtemi Chenge ili automatically awe amepoteza vyote uenyekiti wa bunge na ubunge wenyewe.
 
Back
Top Bottom