Andrew Chenge sasa aage na kuondoka...

Andrew Chenge sasa aage na kuondoka...

Adhabu ya kunyonga ingehusu walafi wa Rasilimali wengi wangekoma ila inahusu waibiwa wa Rasilimali ndio maana
 
maggid: Kwani nani Chenge amejipeleka hapo kwenye kiti? Mtindo wa kuzungukazunguka wakati mnajua kabisa kuwa wabunge wa CCM na wanaCCM ndio wamempeleka bungeni na kumchagua akalie hicho kitu ni wa kijinga kabisa. Hopelss kabisa wewe.
 
Kwani huyu si ndiye aliyetuandikia Katiba ya nchi tunayoisubiri kuipitisha siku chache zijazo? Au nni Chenge mwingine? CCM bwana, kwa kutuzuga hawajambo.
 
Hivi ni nani alikuwa dalali wa nyumba za serikali? Leo viongozi wa serikalini wanaishi hotelini na serikali kupitia kodi zetu inawalipa mabilioni ya shilingi. Watanzania tumerogwa na CCM. Hili ni jini makata.

CCM= Chama Cha Makinikia
 
Mimi namkubali saana Mzee Chenge...anazijuwa sheria na anayo support kubwa ya Govt.kumbuka alivyofanya accident...kumbuka rada
..kumbuka mbunge yule binti wa chadema pale bungeni nk....nk
This time ataweka pingamizi ya kuhojiwa kwa vile anacho kiapo.
Fanya subra utasikia
 
Ndugu zangu,

Nimeona jana kwenye Tv Andrew Chenge akiwa Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge.

Katika mazingira ya sasa, kile cha jana kilipaswa kiwe kikao cha mwisho Andrew Chenge kukiongoza.

Maana, kwa mizoga hii tuliyoonyeshwa kwenye kabati la Chenge, inahitaji ujasiri wa kifisadi kuendelea kukalia kiti cha uenyekiti kuwaongoza Wabunge wa Jamhuri. ' August Session' ni moja ya vikao vya Bunge vyenye hadhi kubwa.

Haviwezi kuongozwa na mtu mwenye tuhuma nzito za ufiaadi na ni dhihaka kubwa kwa Jamhuri inayoongozwa na Rais aliyechaguliwa na aliyesema makubwa jana yenye kumhusisha Chenge pia.

Mimi nadhani, ni wakati sasa, kama Chenge hatajiuzuru mwenyewe nafasi ya uenyekiti Bungeni, Kamati ya Uongozi ya Bunge imshinikize kufanya hivyo. Kazi hiyo si lazima aifanye Kiongozi Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni, Waziri Mkuu.

Maggid Mjengwa.

Picha: Gazeti Mtanzania.
Chenge hana kosa lolote, mwenye makosa ni Rais Mkapa, tuanze na huyo
 
Chenge asiage, bali afukuzwe kama walivyofukuzwa Halima Mdee na Bulaya.
 
Kwa kutumia busara Mh. Chenge ilitakiwa aandike barua ya kujiuzuru nafasi zake zote. Na kurudi nyumbani bariadi kuendelea na shughuli za Kilimo na ufugaji. Sasa imetosha.
 
Hususan kwa sababu kapiga deal na Mkapa na Kikwete na amechukua ushahidi wote.

Na Magufuli kashaapa hatawagusa marais wastaafu.

Sasa atamgusa vipi Chenge bila kuwagusa hao marais?
Hahahhh Mkulu ana mtindo wa kubadilishabadilisha kauli! Kesho anaweza akasema vinginevyo acha tuone tutaishia wapi! Amesema ni kazi ngumu lakini kama Mungu amemweka basi ataifanya kwa kumtegemea Mungu. Katiba Mpya ndio suluhu ya yote haya period!
 
Werevu wanashangaa sana kwa kweli. Mwizi anaambiwa aage????/!!!!!!!!! Hii sijawahi kuona "Ndugu niliowaibia kwa muda wote niliokuwa na nyadhifa serikalini leo nawaaga."

Nyie watu wa ajabu kweli kweli

Kwamba ndio mmejua leo kuwa Chenge hafai?

Mlivyomchagua kuwa mwenyekiti wa Bunge kwa kura nyingi za wabunge wa CCM hamkujua?

Hebu msituchoshe na msitufanye wajinga kwa makosa yenu mnayofanya kila siku.

Waingereza walirudisha chenji ya Rada Bil 40 na ushee na SFO ikasema kabisa Chenge amehongwa...Mlifanya nini?

Msituchoshe wezi nyie CCM
 
Mnasubiri aondoke...? hakuna wa kumgusa jemedari wa vita Chenge inabidi tumshauri aondoke mwenyewe heeee heeee kua na akili kama Chenge ni raha sana.
 
Back
Top Bottom