Andhaa Kanoon

Andhaa Kanoon

BRN

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2013
Posts
5,346
Reaction score
6,841
Hili ni jina la filamu ya kihindi iliyotoka miaka ya mwanzoni ya 1980 ikimhusisha mtaalamu Amitha Bachan.Kwenye filamu hii Amitha anahukumiwa kwa kosa la mauaji..kiukweli hakufanya kosa hila ila na uonevu tu ndio unafanya aonekane anahatia.Baada ya kutumikia kifungo na kutoka jela siku moja anakutana na mtu ambae alidaiwa kupoteza maisha yake,alichofanya Amitha ni kumwua mtu huyo mbele ya hakimu na kuieleza mahakama kwamba hana hatia kwani tayari alishatumikia kifungo. Naifananisha filamu hii na hali ilivyo kwenye mahusiano mengi kwa wakati huu ambapo wenzi hutuhumiana kwa kukosa uaminifu katika mahusiano kwa kubambikiziana kesi.Ikifikia hapo mwenza anaona aahh!! Kama anatuhumiwa kutoka nje ya mahusiano wakati sio kweli ni bora atoke tu na mtu mwingine nje ya mahusiano ili kuleta uwiano na tuhuma anazopata. Huo ni mtazamo wangu tu.
 
no.gif
 
Kusema kweli nina mzio (alergy) na picha za kihindi
 
..............anaona aahh!! Kama anatuhumiwa kutoka nje ya mahusiano wakati sio kweli ni bora atoke tu na mtu mwingine nje ya mahusiano ili kuleta uwiano na tuhuma anazopata...................

  • Hili nalo kwa sasa ni tatizo kwa wapendanao.
 
Kwa kweli mi nimebakiza kupenda nyimbo baadhi tu tena za zamanii
 
Mie tafsiri niijuayo ni 'sheria haina macho'

Hapo ndio umenena mkuu. Na literary ni kuwa sheria imefumbwa macho kuona maovu yanayofanywa na badala yake inahukumu wanyonge wasiokuwa na hatia il-hali wahalifu wanatumia rushwa na kauli za uongo kuilaghai sheria. (sheria inafanyia kazi maneno ua watu)
 
Hili ni jina la filamu ya kihindi iliyotoka miaka ya mwanzoni ya 1980 ikimhusisha mtaalamu Amitha Bachan.Kwenye filamu hii Amitha anahukumiwa kwa kosa la mauaji..kiukweli hakufanya kosa hila ila na uonevu tu ndio unafanya aonekane anahatia.Baada ya kutumikia kifungo na kutoka jela siku moja anakutana na mtu ambae alidaiwa kupoteza maisha yake,alichofanya Amitha ni kumwua mtu huyo mbele ya hakimu na kuieleza mahakama kwamba hana hatia kwani tayari alishatumikia kifungo. Naifananisha filamu hii na hali ilivyo kwenye mahusiano mengi kwa wakati huu ambapo wenzi hutuhumiana kwa kukosa uaminifu katika mahusiano kwa kubambikiziana kesi.Ikifikia hapo mwenza anaona aahh!! Kama anatuhumiwa kutoka nje ya mahusiano wakati sio kweli ni bora atoke tu na mtu mwingine nje ya mahusiano ili kuleta uwiano na tuhuma anazopata. Huo ni mtazamo wangu tu.
Hii Safi Sana hakuna haha ya kubeba mzigo usiyokuwanafaida nao
 
Back
Top Bottom