ANC wagawanyika baada ya kibuka wanaomuunga mkono na wanaompinga Ramaphosa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
1200x-1.jpg

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress kimewateua wajumbe wawili kugombea nafasi ya uongozi wa chama hicho. Mshindi wa kinyangànyiro hicho atagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.

Wajumbe hao ni mwenyekiti wa sasa Cyril Ramaphosa ambaye pia ni rais wa Afrika Kusini. Mwingine ni aliyekuwa waziri wa afya ambaye rais Ramaphosa alimsimamisha kazi kutokana na tuhuma za ufisadi. Waziri huyo wa zamani Zweli Mkhize ni mshirika wa rais wa hapo awali Jacob Zuma na alisimamishwa kazi mwaka uliopita kutokana na madai kwamba wizara yake ilitoa kandarasi kinyume cha taratibu kwa kampuni inayodhibitiwa na washirika wake. Tenda hiyo ilitolewa kwa kampuni ya washirika wake kwa ajili ya kupambana na janga la corona.

Wawekezaji wanahofia kurejea kwa kambi ya Zuma madarakani kunaweza kutishia mageuzi ambayo rais Cyril Ramaphosa ameyafanya katika kupambana na ufisadi unaohusishwa na mtangulizi wake Jacob Zuma ambaye kwa sasa anachunguzwa kwa tuhuma za kushirikiana na wafanyabiashara watatu wa Kihindi kupora mali na fedha za serikali wakati wa uongozi wake kati ya 2009 na 2018 lakini amekanusha tuhuma hizo dhidi yake.

Mkutano mkuu wa 55 wa chama cha ANC unafanyika mjini Johannesburg wakati ambapo mwenyekiti wake rais Ramaphosa amehusishwa na kashfa ya ufisadi. Rais huyo anatuhumiwa kufunika taarifa juu ya wizi wa mamilioni ya fedha uliotukia kwenye shamba lake binafsi. Wapinzani wa Ramaphosa wanamtaka aondoke madarakani kutokana na kashfa hiyo ingawa rais huyo wa Afrika Kusini amekana kutenda makosa na wala hajafunguliwa mashtaka yoyote ya uhalifu.

Umaarufu mkubwa wa chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC umezidi kupungua na chama hicho sasa kinakabiliwa na kitisho cha kupoteza wingi wa uwakilishi wake bungeni.

DW/ RTRE
 
Back
Top Bottom