Anayotaka Dr Slaa haya hapa!

Magobe T

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2008
Messages
2,968
Likes
373
Points
180

Magobe T

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2008
2,968 373 180
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini maneno ya Dr Slaa na pia nilibahatika kufanya naye mahojiano na yeye anasema hivi:

1. Anataka haki ionekane ikitendeka. Kama A amepiga kura kituo B na kupata kura 20. Anataka Tume ya Uchaguzi ya Taifa ikitangaza matokeo, iseme A alipiga kura kituo B na amepata kura 20 na siyo 15 au 30. Kwa hili anataka kifanyike kile ninachokiita 'mathematical truth'.

2. Aliposema akishindwa atakubali kushindwa, alitumia 'analogy' ya timu ya mpira wa mguu. Alisema wachezaji wanapoingia uwanjani kucheza wanatakiwa wao na refa wao wafuate sheria za mpira. Mchezaji akifanya faulo au kufunga goli kwa kutumia mkono, refa aoneshe faulo iliyochezwa na pia aoneshe goli lilifungwa kwa mkono na siyo kwa mguu kwa kupuliza kipenga na si vinginevyo.

Alisema hana sababu ya kukataa goli liliofungwa kihalali. Kwa upande wa uchaguzi, anasema yuko tayarai kukubaliana na matokeo halali hata kama ameshindwa. Yaani, mchakato mzima wa uchaguzi uwe wazi wazi na wahusika watimize wajibu wao bila upendeleo. Lakini pale ambapo haki inakiukwa na matokeo yanabadilishwa ili kumpendelea mgombea fulani, hapo hakubaliani na matokeo yake kwani siyo halali.

3. Baadhi yetu tumekuwa tukitoa maoni na kusema viongozi wawe tayari kukubali matokeo lakini tunashindwa kuonesha ni matokeo ya namna gani tunatakiwa tuyakubali. Ni matokeo halali tu ndiyo tunapaswa tuyakubali na siyo ya kupikwa. Matokeo ya kupikwa ni lazima tuyapinge kwa nguvu zetu zote. Nawaomba Watanzania wenzangu tunapochangia hoja kama hizi tujaribu kuonesha ni kitu gani tunachoongelea na tuepuke ushabiki ambao hauna tija kwa taifa letu. Kwa kuendekeza uchakachuaji wa matokeo, tutakuwa tunakataa 'kuziba ufa' na ni wazi kwa baadaye tutaanza 'kujenga ukuta'.

4. Kwa hiyo, Dr Slaa ana haki ya kisheria ya kukataa matokeo pale anapoona haki haikutendeka. Inabidi asikilizwe na kasoro anazodai zimetokea ziangaliwe na zielezwe kwa nini zimetokea kuliko kukana na kuonesha kuwa anachosema ni uongo. The mentality of 'might is right' doesn't hold water in a democratic country like Tanzania.
 
Gerad2008

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2009
Messages
525
Likes
129
Points
60

Gerad2008

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2009
525 129 60
Tunachojua ni kwamba Kikwete anataka kuthibisha ule usemi aliosema kwa jazba pale Msoga Bagamoyo tarehe 31/10/2010 akipiga kura kwamba "LAZIMA TUSHINDE". Kauli kama hii haina pande mbili bali upande mmoja tu wa kushinda na ina maana kwa gharama yoyote. Mtu anapoamua kushinda kwa lazima wakati wa mashindano ujue kama ni mpira wa miguu atakuwa amempa rushwa mwamuzi au ana influence kubwa kwa mwamuzi au waamuzi. Haikuwepo haja ya uchaguzi kama JK alikuwa ana uhakika wa kushinda.

Ndugu wana JF mtakumbuka JK akiwa anafunga kampeni pale Jangwani tarehe 30/10/2010 alitamka kwamba Dk Slaa ana UCHU WA MADARAKA. Kama rais alijua kwamba yuko katika ushindani asingethubutu kutamka kauli kama hii. Alitakiwa ajue kwamba kila moja ana equal chance ya kuchaguliwa kuwa rais na si lazima awe yeye. Alionyesha chuki na hasira kwa Slaa kana kwamba yeye JK hajui maana ya uchaguzi.

Matokeo yanayoeendelea kutangazwa ni kana kwamba JK anataka kumwambia Slaa AKOME NA ASIRUDIE TENA'
 
tempo_user1

Senior Member
Joined
Sep 7, 2010
Messages
134
Likes
0
Points
0

tempo_user1

Senior Member
Joined Sep 7, 2010
134 0 0
Mi nadhani wakulaumiwa hapa ni CCM, wamefanya kosa kubwa na hawajatutendea haki watanzania kwa kumpitisha JK kugombea tena kiti cha urais hali wakijua kwamba hana sifa za uongozi kwa ngazi aliyogombea.
 
Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
8,184
Likes
111
Points
160

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2010
8,184 111 160
Kwa kweli nilitegemea JK angeweza kushinda lakini siyo kama matokeo yanavyoonyesha sasa, inanipa mashaka kidogo kwa sababu kuu zifuatazo:-

  1. Ucheleweshwaji wa matokeo katika majimbo ambayo yalikuwa na upinzani mkubwa. Hii nakusudia kuanzia ubunge mpaka urais.
  2. Muafaka wa CCM na CUF Zanzibar. Ikiangalia kwa makini utagundua kuwa muafaka huo ulipatikana baada ya kinachoaminika ni upokwaji wa ushindi wa CUF karibu mara mbili hivi. Ikaonekana kabisa ili kuinusuru Zanzibar na machafuko ni muafaka. Hivyo kwa bara kwa sababu upinzani ndiyo umeanza kuonyesha cheche ipo siku ikionekana hali ni ngumu basi muafaka utafuata kwa sababu CCM haijajiandaa kuachia dolla.
 
Haika

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
2,318
Likes
68
Points
145

Haika

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
2,318 68 145
mie ningeomba tu mtu mwenye uwezo wa kunifafanulia tu utaratibu mzima wa uchaguzi (ideally) ulitakiwa uweje.
1kupiga kura,
2kuhakikiwa umepiga bila kukosa au kurudia,
3kuhesabu katika kituo cha kupigia kura
4kuhakiki na kukubaliana
5kutangaza/kubandika matokeo halali
6kusafirisha matokeo
7kujumlisha/kujumuisha matokeo ya vituo mbalimbali,
8kutangaza katika ngazi ya kati
9kujumuisha na kutuma taifani
10kutangaza/kujumlisha?

mi nadhani tukiamua kuwa wazi, tunaweza kujua bila hiana wapi pana tatizo na tunaweza kulirekebisha kama inawezekana, au kubadili kabisa mfumo.

haswa kipengele cha uhalali wa matokeo ya kutoka vituoni, matokeo yanyokwenda taifani, watu wanaohusishwa, vyombo vinavyohusishwa?
utaalamu unaohitajika, nk
 
Kwa kifupi sana, nasweza kuchangia hivi:
1. Uwazi katika kila hatua ya mchakato wa uchaguzi.
2. Kura zilizohesabiwa na kuhakikiwa na mawakala ziwe zilezile zinazotangazwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi. i.e 2 + 2 = 4 na siyo 3 au 6. Kama kuna kasoro zioneshwe na zitolewe maelezo kuliko kufichwa.
3. Wapiga kura (wadau wa uchaguzi) wanapoona mfumo na mchakato wa uchaguzi ni huru na wazi wanakuwa na imani na tume na matokeo yanayotangazwa.
 
Ehud

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2008
Messages
2,696
Likes
24
Points
0

Ehud

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2008
2,696 24 0
Kama NEC na CCM wameona watangaze matokeo wanayoyajua wao hakukuwa na haja ya kupoteza muda kufanya uchaguzi. Wangemtangaza tu mtele wao.
 
Quick

Senior Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
154
Likes
3
Points
35

Quick

Senior Member
Joined Nov 4, 2010
154 3 35
Haiwezekani timu ya BLUE ishinde wakati Refarii pamoja wasaidizi wake wameajiriwa na timu ya KIJANI,piga ua ni KIJANI tu
 
Saharavoice

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
2,672
Likes
223
Points
160

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
2,672 223 160
Watu wazima tumeamka asubuhi kwenda kupiga kura, tukitegemea kutangaziwa kile kilicho halali, halafu wanakuja wapumbavu kadhaa kwa maslahi yao wanabadilisha matokeo, very shame!!, Hakika JK hatatawala kwa aman hii miaka 5, itakuwa michungu kwake kama shubiri. Tutamzomea kila mahali atakapoenda, labda aendeleze utalii wake huko nje, but not inside.
 
Joined
May 25, 2009
Messages
21
Likes
0
Points
3

desertfish

Member
Joined May 25, 2009
21 0 3
Nadhani CCM pia itakuwa imetumia mwanya wa CHADEMA kutokuwa na mawakala wa kutosha au makini hasa huko vijijini wenye uwezo wa kung'amua janja ya uchakachuaji na kusimama kidete kutetea haki
 
QUALITY

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2010
Messages
854
Likes
2
Points
0

QUALITY

JF-Expert Member
Joined Sep 27, 2010
854 2 0
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini maneno ya Dr Slaa na pia nilibahatika kufanya naye mahojiano na yeye anasema hivi:

1. Anataka haki ionekane ikitendeka. Kama A amepiga kura kituo B na kupata kura 20. Anataka Tume ya Uchaguzi ya Taifa ikitangaza matokeo, iseme A alipiga kura kituo B na amepata kura 20 na siyo 15 au 30. Kwa hili anataka kifanyike kile ninachokiita 'mathematical truth'.

2. Aliposema akishindwa atakubali kushindwa, alitumia 'analogy' ya timu ya mpira wa mguu. Alisema wachezaji wanapoingia uwanjani kucheza wanatakiwa wao na refa wao wafuate sheria za mpira. Mchezaji akifanya faulo au kufunga goli kwa kutumia mkono, refa aoneshe faulo iliyochezwa na pia aoneshe goli lilifungwa kwa mkono na siyo kwa mguu kwa kupuliza kipenga na si vinginevyo.

Alisema hana sababu ya kukataa goli liliofungwa kihalali. Kwa upande wa uchaguzi, anasema yuko tayarai kukubaliana na matokeo halali hata kama ameshindwa. Yaani, mchakato mzima wa uchaguzi uwe wazi wazi na wahusika watimize wajibu wao bila upendeleo. Lakini pale ambapo haki inakiukwa na matokeo yanabadilishwa ili kumpendelea mgombea fulani, hapo hakubaliani na matokeo yake kwani siyo halali.

3. Baadhi yetu tumekuwa tukitoa maoni na kusema viongozi wawe tayari kukubali matokeo lakini tunashindwa kuonesha ni matokeo ya namna gani tunatakiwa tuyakubali. Ni matokeo halali tu ndiyo tunapaswa tuyakubali na siyo ya kupikwa. Matokeo ya kupikwa ni lazima tuyapinge kwa nguvu zetu zote. Nawaomba Watanzania wenzangu tunapochangia hoja kama hizi tujaribu kuonesha ni kitu gani tunachoongelea na tuepuke ushabiki ambao hauna tija kwa taifa letu. Kwa kuendekeza uchakachuaji wa matokeo, tutakuwa tunakataa 'kuziba ufa' na ni wazi kwa baadaye tutaanza 'kujenga ukuta'.

4. Kwa hiyo, Dr Slaa ana haki ya kisheria ya kukataa matokeo pale anapoona haki haikutendeka. Inabidi asikilizwe na kasoro anazodai zimetokea ziangaliwe na zielezwe kwa nini zimetokea kuliko kukana na kuonesha kuwa anachosema ni uongo. The mentality of 'might is right' doesn't hold water in a democratic country like Tanzania.
Cheers
 
Uyole12

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2010
Messages
588
Likes
18
Points
35
Age
32

Uyole12

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2010
588 18 35
Mimi nilikuwa mmoja wa wakala wa chadema vijijini kusema kweli wapigakura vijijini ni wachache mno mfano kituo changu kilikuwa na watu 279 waliopiga 166, kituo cha jirani walikuwa 426 waliopiga ni 136 unatarajia nini kwa kura zilizobaki kama si kuumia kama hauna wakala mzuri? Mie ni mmoja wapo 2liompitisha silinde mbozi maghalibi. Vyama vya upinzani mawakala waelewa vijijini ndo ushindi la sivyo hakuna ushindi milele.
 
Ndumbayeye

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2009
Messages
5,724
Likes
1,690
Points
280

Ndumbayeye

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2009
5,724 1,690 280
mpira dakika 90 wakuu, hata kama ni goli la mkono likikubaliwa mechi hairudiwi.CCM bingwa mbona simba na yanga wananunua mechi kila siku na ligi hairudiwi. KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI, nchi yetu sote hii...iacheni CCM maendeleo yanaletwa na watendaji wa serikali sio kina makamba na kinana, hata slaa atawakuta hao2 na watamchanganya pia, HAIKUWA RAHISI!
 
Forum statistics

Threads 1,203,561
Members 456,824
Posts 28,118,735