Elections 2010 Anayotaka Dr Slaa haya hapa!

I'm sick and tired of the name Kikwete, especially when he is tampering with grand gift God have given us, namely peace!
 
Jamani Jamani......Nadhani Watu wa usalama wa taifa wameingia kwenye JF. Baadhi ya page hazifunguki kwa sasa na nyingi zimekuwa private...Inauma...sambaza ujumbe
 
mpira dakika 90 wakuu, hata kama ni goli la mkono likikubaliwa mechi hairudiwi.CCM bingwa mbona simba na yanga wananunua mechi kila siku na ligi hairudiwi. KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI, nchi yetu sote hii...iacheni CCM maendeleo yanaletwa na watendaji wa serikali sio kina makamba na kinana, hata slaa atawakuta hao2 na watamchanganya pia, HAIKUWA RAHISI!

Hata kama mechi hairudiwi lakini walau isemwe kuwa goli lilifungwa kwa mkono na siyo kwa mguu wakati kila mtu na linesmen waliona goli lifingwa kwa mkono. Tukiambiwa hilo tuhoji je sheria za mpira zinasema nini kuhusu ufungaji wa goli. Binafsi uchakachuaji huu unatunyemelea kuanzia kwenye mitihani ya shule, vyeti, kwenye huduma zingine na sasa kwenye kura na baada ya hapo utahamia sehemu nyingine. Njia nzuri ya kupambana nao siyo kuufumbia macho bali kuupiga vita kwani utaweza kutufarakanisha.

Ni kama mtu uchumbie fiancee A na siku ya harusi ukute fiancee B halafu uambiwe 'kubali yaishe' hilo ndilo lilikuwa chaguo lako. Inaingia akilini? Kwa namna nyingine ni kwamba: suppose umeoa na ikatokea mke wako ni mjamzito na taarifa za clinic zioneshe kajifungua mtoto wa kiume hospitali na ndugu au jirani waone kweli ni mtoto wa kiume. Halafu baadaye nesi alete mtoto mwingine, ambaye ni wa kike kutoka sehemu watoto wadogo wanapohifadhiwa. Je, yupi ni mtoto wako halali: yule aliyezaliwa na kuonekana ni wa kiume au huyu wa pili wa kike? Hivyo nidvyo ilivyotokea kwenye uchakachuaji.
 
Kwa mimi naona jambo la msingi ni sisi wananchi na wabunge tupiganie katiba iliyopo ibadilishwe kwani hadi sasa inaegememea chama kimoja.tukiamua inawezekana na tume ya uchaguzi itakuwa ya huru na haki kwan iliyopo imeteuliwa na mafisadi kwa maslahi yao haina nia ya kumkomboa mlalahoi kama mimi.
 
Tunachojua ni kwamba Kikwete anataka kuthibisha ule usemi aliosema kwa jazba pale Msoga Bagamoyo tarehe 31/10/2010 akipiga kura kwamba "LAZIMA TUSHINDE". Kauli kama hii haina pande mbili bali upande mmoja tu wa kushinda na ina maana kwa gharama yoyote. Mtu anapoamua kushinda kwa lazima wakati wa mashindano ujue kama ni mpira wa miguu atakuwa amempa rushwa mwamuzi au ana influence kubwa kwa mwamuzi au waamuzi. Haikuwepo haja ya uchaguzi kama JK alikuwa ana uhakika wa kushinda.

Ndugu wana JF mtakumbuka JK akiwa anafunga kampeni pale Jangwani tarehe 30/10/2010 alitamka kwamba Dk Slaa ana UCHU WA MADARAKA. Kama rais alijua kwamba yuko katika ushindani asingethubutu kutamka kauli kama hii. Alitakiwa ajue kwamba kila moja ana equal chance ya kuchaguliwa kuwa rais na si lazima awe yeye. Alionyesha chuki na hasira kwa Slaa kana kwamba yeye JK hajui maana ya uchaguzi.

Matokeo yanayoeendelea kutangazwa ni kana kwamba JK anataka kumwambia Slaa AKOME NA ASIRUDIE TENA'

Hata kule Bukombe nasikia wakati akiwa kwenye kampeni, watu walionekana kutomuunga mkono na kumwonyesha dhahiri kuwa walikuwa upande wa Dr. Slaa ndipo akawaambaia maneno "mpigieni kura mnayemtaka lakini CCM itashinda kwa kishindo". Maneno haya yana maana kuwa lazima washinde na namna ya kushinda alikuwa anaifahamu.
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini maneno ya Dr Slaa na pia nilibahatika kufanya naye mahojiano na yeye anasema hivi:

1. Anataka haki ionekane ikitendeka. Kama A amepiga kura kituo B na kupata kura 20. Anataka Tume ya Uchaguzi ya Taifa ikitangaza matokeo, iseme A alipiga kura kituo B na amepata kura 20 na siyo 15 au 30. Kwa hili anataka kifanyike kile ninachokiita 'mathematical truth'.

2. Aliposema akishindwa atakubali kushindwa, alitumia 'analogy' ya timu ya mpira wa mguu. Alisema wachezaji wanapoingia uwanjani kucheza wanatakiwa wao na refa wao wafuate sheria za mpira. Mchezaji akifanya faulo au kufunga goli kwa kutumia mkono, refa aoneshe faulo iliyochezwa na pia aoneshe goli lilifungwa kwa mkono na siyo kwa mguu kwa kupuliza kipenga na si vinginevyo.

Alisema hana sababu ya kukataa goli liliofungwa kihalali. Kwa upande wa uchaguzi, anasema yuko tayarai kukubaliana na matokeo halali hata kama ameshindwa. Yaani, mchakato mzima wa uchaguzi uwe wazi wazi na wahusika watimize wajibu wao bila upendeleo. Lakini pale ambapo haki inakiukwa na matokeo yanabadilishwa ili kumpendelea mgombea fulani, hapo hakubaliani na matokeo yake kwani siyo halali.

3. Baadhi yetu tumekuwa tukitoa maoni na kusema viongozi wawe tayari kukubali matokeo lakini tunashindwa kuonesha ni matokeo ya namna gani tunatakiwa tuyakubali. Ni matokeo halali tu ndiyo tunapaswa tuyakubali na siyo ya kupikwa. Matokeo ya kupikwa ni lazima tuyapinge kwa nguvu zetu zote. Nawaomba Watanzania wenzangu tunapochangia hoja kama hizi tujaribu kuonesha ni kitu gani tunachoongelea na tuepuke ushabiki ambao hauna tija kwa taifa letu. Kwa kuendekeza uchakachuaji wa matokeo, tutakuwa tunakataa 'kuziba ufa' na ni wazi kwa baadaye tutaanza 'kujenga ukuta'.

4. Kwa hiyo, Dr Slaa ana haki ya kisheria ya kukataa matokeo pale anapoona haki haikutendeka. Inabidi asikilizwe na kasoro anazodai zimetokea ziangaliwe na zielezwe kwa nini zimetokea kuliko kukana na kuonesha kuwa anachosema ni uongo. The mentality of 'might is right' doesn't hold water in a democratic country like Tanzania.

Ndugu yangu unayoongea yamenitia uchungu sana. Ni mawazo mazuri sana. Unajua watanzania tuna ushabiki wa kijinga sana na tunapenda kuchukulia mambo juu juu tu bila kuyatafakari kwa kina kinacholalamikiwa na watu walioonewa. Kwa utamaduni huu, ccm itaendelea kuitawala nchi hii kwa ubavu bila kujali kama wananchi wanaipenda au la. Nchi hii ina watu wengi walioelimika lakini ni waoga wa kudai haki na mabadiliko ili kuondoa uwizi na ukilitimba unaofanywa na ccm. Mimi binafsi ninampongeza sana Dr. Slaa na kwa kweli Mungu ambariki sana. Ushauri wangu kwa Dr. Slaa ni kwamba pamoja na hatua anayochukua ya kudai haki, asikate tamaa kueneza elimu ya uraia kwa wananchi. Wabunge wa chadema walioongezeka si haba na kwa kweli ni mafanikio makubwa sana yaliyotokana na juhudi kubwa iliyofanywa na chama cha chadema. Mimi nina hakika tena sana kwamba kasi hii ya kuongeza wabunge ndiyo itakayotuwezesha kuibadili tume ya uchaguzi kuwa huru na hivyo kuondoa uwezekano wa ccm kuiba kura.

Ninawatakia afya njema viongozi wote wa chadema na mwenyezi Mungu aendelee kuwawezesha ili hatimaye nchi hii ifikie ukombozi kamili.
 
Back
Top Bottom