Huyo atakuwa na ugonjwa wa akili. Hata kule UK mwaka fulani sikumbuki (2005 au 6 hivi) Met Police waliwahi kukamata mtu mmoja aliyekuwa na tabia ya kuua machangudoa wa kule. Na alikuwa na chaguo lake: blonde tu. Alikuwa anawavizia wanakojipanga anachagua mmoja anampakia kwenye ki-fiat chake, anapeleka nyumbani kwake kabisa, anafanya akimaliza ananyonga anapakia kwenye buti ya gari kisha anaenda kumtupa. Hadi anakamatwa alishanyonga 9 na kuwatupa sehemu mbalimbali kwenye mitaro, public parks, chini ya daraja, mtoni nk. Kule waliweza kumkamata kwa ku-review zile CCTV footage kutoka kwa zile camera walizotega maeneo hayo ya machangudoa. Na alikiri mwenyewe mahakamani kuwa aliua wote hao kwa kuwa anachukia tabia yao, na pia ati alitaka kuonesha hasira yake kwa kitendo cha serikali kuacha biashara ya uchangudoa ishamiri, ati akadai ni kinyume cha maadili. Alitwangwa life imprisonment. Swali litakaloendelea kutusumbua ni hili: Ikiwa katika hiyo nchi iliyoendelea na yenye vifaa vya kisasa na mbinu kali walikufa kwanza watu 9 ndipo muuaji akakamatwa, hapa kwetu na 'usanii' huu na uduni wa vitendea kazi kuna uwezekano wowote wa kukamatwa huyu?