Anayeua wanawake Dar es Salaam ashitukiwa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WAKATI hofu ya matukio ya kuuawa kwa wanawake jijini Dar es Salaam ikitanda, jeshi la polisi limepokea taarifa kuhusiana na mtu anayedaiwa kuhusika na matukio hayo yanayofanyika katika nyumba za kulala wageni.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Kamanda Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa polisi imepata taarifa kuhusiana na mwanaume mweupe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, anayependelea kuvaa suruali aina ya Jeans, fulana nyeupe, raba na kofia kwamba ndiye mhusika wa matukio hayo ya mauaji.

“Inasemekana mtu huyu anapendelea kufuata wanawake weupe na hasa walioolewa na kisha huwapeleka katika nyumba tofauti za kulala hapa jijini na akishamaliza nia yake, huwaua,” alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, matukio hayo ya mauaji yametokea katika maeneo ya Tandika, Mtoni kwa Aziz Ally, Buguruni kwa Mnyamani na Keko Machungwa.

Wanawake wameuawa baada ya kufanyiwa mchezo mchafu wa kuingiliwa kinyume cha maumbile na kisha kunyongwa mpaka kufa.

Kutokana na matukio hayo, Kamanda Kova ametoa onyo kwa wanawake kutokubali kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume wasiowafahamu.

Kamanda Kova amewakumbusha pia wahudumu wa mapokezi katika nyumba za kulala wageni kuhakikisha wanaandika majina na anuani kamili za mwanaume na mwanamke kabla ya kuingia katika chumba.

Amesema, Polisi kwa kushirikiana na jamii imeanza msako mkali kuwasaka watuhumiwa wote wanaojihusisha na matukio hayo na kuomba mtu yoyote mweye taarifa za watuhumiwa hao kutoa taarifa katika vituo vya polisi vilivyopo karibu au kutuma ujumbe mfupi katika namba 0783034224.

Hivi karibuni yaliripotiwa matukio ya mauaji ya wanawake watatu katika nyumba tatu tofauti za kulala wageni katika Manispaa ya Kinondoni na Temeke.

Polisi ilibaini kuwa wanawake hao wote waliouawa, walikuwa wamekwenda katika maeneo hayo kwa ajili ya kustarehe na wenza wao.
 
ni tatizo tu la kisaikolojia, hamna cha demonic wala nn....kama ni demonic na wizi, ufisadi, umalaya je? nayo si demonic? huyu serial killer alichelewa tu kupata ushauri wa kisaikolojia, manake inaonekana anawachukia wake za watu.
 
kwan hao anaowaua ni wake za watu tu???
ni tatizo tu la kisaikolojia, hamna cha demonic wala nn....kama ni demonic na wizi, ufisadi, umalaya je? nayo si demonic? huyu serial killer alichelewa tu kupata ushauri wa kisaikolojia, manake inaonekana anawachukia wake za watu.
 
Hivi Tanzania kuna kikosi maalumu kinacho
hangaikia mambo ya mauaji??
Ukiachia mbali polisi wa kawaida tu
na je kuna Crime labs? au kitu kaa hicho..
 
This is man seems that his mind has been dented with his past history..... based to Police explanation, I can say that he is Sadist.
 
Kumbe wake za watu sio waaminifu? Wanakutana na mtu njiani tu wanampa ndoa yao? Jesus. Nikwavile jamaa anawaua ndio maana simsupport ingekuwa adhabu nyingine wallah ningempa baraka zangu.
 
Kumbe wake za watu sio waaminifu? Wanakutana na mtu njiani tu wanampa ndoa yao? Jesus. Nikwavile jamaa anawaua ndio maana simsupport ingekuwa adhabu nyingine wallah ningempa baraka zangu.
Siku hizi Nguli Jabali uaminifu umeshuka sana kati ya wanandoa!
 
Kumbe wake za watu sio waaminifu? Wanakutana na mtu njiani tu wanampa ndoa yao? Jesus. Nikwavile jamaa anawaua ndio maana simsupport ingekuwa adhabu nyingine wallah ningempa baraka zangu.

Labda yuko kwenye mikakati ya kurudisha wake za watu kwenye maadili mema-eti mke wa mtu anakutana na mtu asiyemjua njiani anaenda naye kumpa uroda-disgusting!
 
Siku hizi Nguli Jabali uaminifu umeshuka sana kati ya wanandoa!

Aisee ni too much, anakutana nae sokoni anabeba bora hao wanaotegana maofisini safarini mashuleni etc, akitoka tu, ka-buuuuuum du noumaaaa. Huyu jamaa anasaidia kurekebisha tabia zao. Au waume zao ze Zakari not reachable au wameoa vicheche haviriziki?
 
hapa umenena. Itabid warudi tu kwenye hayo maadil, manake jamaa hana utani kadhamiria kwa moyo wake wote!
Labda yuko kwenye mikakati ya kurudisha wake za watu kwenye maadili mema-eti mke wa mtu anakutana na mtu asiyemjua njiani anaenda naye kumpa uroda-disgusting!
 
Now Tanzania is getting the experience of SERIAL KILLERS. Tulikuwa tunasoma tu habari hizo Ulaya
serial killer wapo na walikuwepo, tatizo lilikua namna ya reporting na ile spreading ya information nchi nzima

The guy ni psycho na anawezekana sana analipiza kisasi fulani... unfortunately, to the wrong people
 
Back
Top Bottom