Anayeua wanawake Dar es Salaam ashitukiwa

Kwa hiyo yeye anahitaji wake za watu tu? Kutakuwa na sababu ya huyo jamaa kuwalenga wake za watu zaidi..

Huenda alisalitiwa na mke wake na hivyo kuishia kuchukia wanawake wote waliokuwa katika ndoa na ambao si waaminifu; mungu amsamehe na ampe rehema ya kusamehe waliomkosea ili aondokane na kamba za kuzimu.
 
huyu yawezekana mtu maarufu sana na wanamjua aidha alikua kiongozi au la kulikua na kitu kilichompa umaarufu kwa hiyo sababu hawa wanawake wanamfahamu ndio maana ili kuficha siri anaamua kuwaua!
Labda yuko kwenye mikakati ya kurudisha wake za watu kwenye maadili mema-eti mke wa mtu anakutana na mtu asiyemjua njiani anaenda naye kumpa uroda-disgusting!
 
WAKATI hofu ya matukio ya kuuawa kwa wanawake jijini Dar es Salaam ikitanda, jeshi la polisi limepokea taarifa kuhusiana na mtu anayedaiwa kuhusika na matukio hayo yanayofanyika katika nyumba za kulala wageni.

Hayo yamethibitishwa na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Kamanda Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa polisi imepata taarifa kuhusiana na mwanaume mweupe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30, anayependelea kuvaa suruali aina ya Jeans, fulana nyeupe, raba na kofia kwamba ndiye mhusika wa matukio hayo ya mauaji.

"Inasemekana mtu huyu anapendelea kufuata wanawake weupe na hasa walioolewa na kisha huwapeleka katika nyumba tofauti za kulala hapa jijini na akishamaliza nia yake, huwaua," alisema.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, matukio hayo ya mauaji yametokea katika maeneo ya Tandika, Mtoni kwa Aziz Ally, Buguruni kwa Mnyamani na Keko Machungwa.

Wanawake wameuawa baada ya kufanyiwa mchezo mchafu wa kuingiliwa kinyume cha maumbile na kisha kunyongwa mpaka kufa.

Kutokana na matukio hayo, Kamanda Kova ametoa onyo kwa wanawake kutokubali kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume wasiowafahamu.

Kamanda Kova amewakumbusha pia wahudumu wa mapokezi katika nyumba za kulala wageni kuhakikisha wanaandika majina na anuani kamili za mwanaume na mwanamke kabla ya kuingia katika chumba.

Amesema, Polisi kwa kushirikiana na jamii imeanza msako mkali kuwasaka watuhumiwa wote wanaojihusisha na matukio hayo na kuomba mtu yoyote mweye taarifa za watuhumiwa hao kutoa taarifa katika vituo vya polisi vilivyopo karibu au kutuma ujumbe mfupi katika namba 0783034224.

Hivi karibuni yaliripotiwa matukio ya mauaji ya wanawake watatu katika nyumba tatu tofauti za kulala wageni katika Manispaa ya Kinondoni na Temeke.

Polisi ilibaini kuwa wanawake hao wote waliouawa, walikuwa wamekwenda katika maeneo hayo kwa ajili ya kustarehe na wenza wao.

Sometimes you get the feeling that our policemen wanasema tu ilimradi ionekane wamesema na waandishi wetu wanaandika tu mradi habari itoke gazetini. Kuna maswali kadhaa muhimu sana ambayo muandishi wa kawaida kabisa angeweza kumuuliza mheshimiwa Kova kabla ya kuandika habari hii:

1/ Hio description ya huyo alleged serial killer aliyotoa hapo is that all he can give to the public? "mwanaume mweupe anayekadiriwa kuwa na miaka 30, anayependa kuvaa fulana, jeans, raba na kofia"? Really? Kwenye Idara yetu ya polisi hakuna kitengo cha wachora picha ambao wanaweza kuchoro picha ya mtuhumiwa kutokana na maelezo ya watu wanaodai kumuona?? Is that the only description raia wema wanategemewa kuitumia ili kuisaidia Polisi kumkamata mtuhumiwa??


2/ Mimi ni mfuatiliaji wa habari za magazeti. Kwa kumbukumbu yangu kuhusu wanawake waliokutwa wamekufa kwenye Guest House katika kipindi cha miezi mitatu/minne iliyopita sikumbuki kusoma mahali kwamba kuna aliyekuwa mke wa mtu. Ninachokumbuka ni kuwa watatu kati yao walikuwa na vitambulisho vinavyowajulisha kama wanafunzi na wengine walionekana kuwa ni twilight ladies. Hizi taarifa zailikuwa zinatolewa na Polisi na kunukuliwa na Vyombo vya habari. Hizi taarifa za kuwa wengi walikuwa ni wake za watu wakati zilikuwa hazifahamiki??
 
ni hatari...kwa kila mtu. na tulivyo na laxity zetu inawezakana kuua watu wengi bila kugundulika. na akiamua kubadili aina ya walengwa wake sijui atamaliza wangapi kabla ya kukamatwa.
 
ingekua jinsia tofauti ndiye anaua wanaume naona angekamatwa mapema sana!
ni hatari...kwa kila mtu. na tulivyo na laxity zetu inawezakana kuua watu wengi bila kugundulika. na akiamua kubadili aina ya walengwa wake sijui atamaliza wangapi kabla ya kukamatwa.
 
mbona kuna movie ya kitanzania nimesha wahi kuiona wameigiza ivi ivi isue inavyotendeka? idea waliitoa wapi?
 
Kamanda Kova amewakumbusha pia wahudumu wa mapokezi katika nyumba za kulala wageni kuhakikisha wanaandika majina na anuani kamili za mwanaume na mwanamke kabla ya kuingia katika chumba.
Mhudumu wa mapokezi huwa haandiki jina la mtu we Kova, kuna counter book unarushiwa hapo ujaze ujuavyo wewe, na mapokezi hawezi ku verify any bullshit utakayoandika mule. Besides, Bongo hatuna vitambulisho, mapokezi atajuaje identification yako??? Na hata vingekuwepo, kama unakwenda na mke wa mtu, tena kumuua, ungeshindwa kuwa na kitambulisho fake?

Kutokana na matukio hayo, Kamanda Kova ametoa onyo kwa wanawake kutokubali kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume wasiowafahamu.
Sexist and unrealistic statement. Wanajuaje hizi zilikuwa ni one night stands?

Hata mke wako alikuwa hakufahamu kabla ya kuingia nae chumbani mara ya kwanza. Unajuaje hawa wanawake hawaku date na jamaa? Mtu ambae hahitaji date ni changudoa, lakini mke wa mtu or any girl worth her womanhood lazima uhangaike, umtoe, uhonge. etc. i.e. dating i.e kufahamiana. Sasa wanajuaje huyu jamaa walikuwa hawamjui?

Na kwa upande wa pili, hata mwanamme mademu kibao kama wangekuwa wauaji wangeshatuua, unapokwenda na demu chumbani mara ya kwanza unakuwa ushakutana na wazazi wake na "kumfahamu" kiundani? Please!

Tusilaumu wanawake waliokufa wala wahudumu wa mapokezi guest. Statement za Kova peke yake zinakufanya uone jeshi la polisi halijaenda shule, na ndo sababu ya high crime rate.
 
Maeneo yenyewe yaliyotajwa jamani, keko machungwa, tandika, buguruni, mtongani, etc. Maisha yenyewe huko mgumu, so anawarubuni tu wewe ukirudi mihangaikoni unakuta wali kuku wakati uliacha hela ya matembele, sasa mbona huulizi kuku umepata wapi? Maisha bora kwa kila Mtanzania??
 
jamani wa tz wezangu tuna elekea wap lakini mpaka tuna anza kuuana kama wanyama kwa nn jaamani:A S cry::A S cry::A S cry:
 
Back
Top Bottom