Anayejua jinsi ya kujiunga na pay pal | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anayejua jinsi ya kujiunga na pay pal

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kamongo, Dec 29, 2011.

 1. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  natumaini wote ni wazima wa afya, mimi nataka kuagiza gari japan kuna kampuni inaitwa YOSHIDA AUTO ila nimesikia njia nzuri ili nisitapeliwe initumie pay pal sasa naombeni msaada hiyo huduma inatolewa na benki gani hapa Tanzania au nikitaka kujiunga nifanyeje
   
 2. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Usitumie paypal kununua gari, nakushauri ingia tradecarview.com na lipia gari unayoipenda kwa kutumia pay trade, hii ni huduma nzuri na ya uhakika. Inagharimu dola 150 lakini its well woth it... Sina uhakika kama 150 ni flat rate au inavary kulingana na thamani ya gari.
  If u insist on using pay pal, fungua www.paypal.com halafu create account, jaza form na soma maelekezo yote utafanikiwa. Hakuna bank yenye huduma ya paypal duniani. Unatakiwa uwe na credit/debit card inayoweza kuprocess electronic transactions kama visa/ mastercard, amex nk...kwahiyo utahamisha hela electronically kutoka kwenye ac yako ya bank kwenda kwenye ac yako ya paypal, then hapo ndio utalipia kutoka paypal... Ni kama unahifadhi hela zako kwenye benki nyingine inayofanya kazi online tu...
  Wengine wataendelea kama bado hujaelewa au kuridhika na maelezo.
   
 3. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nadhani mkuu kamongo!! umesoma thread flani masaa machache yaliyopita!! pay-pal ni nzuri kwa ununuzi wa vitu vidogo vidogo kama ujuavyo, ebay, amazon na zingine nyingi tu!! mara nyingi provider wa hizi service za online shopping kama vile e-bay huwa wana suggest na kuhimzia watumiaji kujisajili na pay-pal ili kuepuka watu kudhulumiwa na kuanza kutafuta ofisi za e-bay bila mafanikio.
  lakini kwa ununuzi wa magari na nyumba kaka hatufanyi hivi. kuna jinsi nyingine za ku secure kitita chako kwa mfano hapo juu Doltyne kakupa upenyo!!
  Ngoja waje wataalamu humu wamwage ya kwao... mafundi wengi humu usijali itakuwa tu... good luck
   
 4. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  hiyo huduma ya PAY TRADE ni salama?
   
 5. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  nina wasi wasi na paypal coz niliwahi kusikia kuwa paypal iliingia katika matatizo na bank moja ya huko huko JAPAN
   
 6. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Pay trade ni salama kabisa, inasimamiwa na tradecarview... Ukimlipa muuzaji unawalipa wao kwanza kutoka katika ac yako, ukienda bank na invoice yako, bank wanaelewa nini cha kufanya. Na Trade Car View kupitia Paytrade, wanahakikisha ukidhulumiwa au gari yako isipokufikia kwa sababu zozote zile watakulipa hela zote ulizolipia gari minus their fee (150 usd).
  Kumbuka, mawasiliano yako yote na muuzaji gari yafanyike ndani ya mtandao wa tradecarview na sio kungine, msitumiane email direct kwa kupitia huduma kama yahoo mail, hotmail, google mail etc... Create account Trade Car view, na log in kila wakati unataka kuwasiliana na wauzaji...ukishaingia kwenye mtandao wao utaelewa zaidi.
   
 7. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Thank You Mkuu,Umenielimisha na Mimi pia,JF imesheheni Maarifa!!
  Hauwezi kuingia humu halafu utoke kapa!!
  Hicho kipengele cha kulipwa fidia mambo yanapokuwa yamekwenda Mrama,nani analipa,TradeCar View au Bank yangu?!!!
   
 8. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Fafanua kdogo kaka, waalingia kwenye matatzo gan? Paypal ni mali ya Ebay, na hawa jamaa reputation yao nadhani unaifahamu. Kabla haujajiunga nao na kutumia huduma zao tafadhali SOMA KWA UMAKINI TERMS AND CONDITIONS! watu wengi hatuna utaratibu huo, matokeo yake baadae tunaanza kulalama. Kwa gari Japan pia nisingekushauri kutumia paypal!
   
 9. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Utalipwa na trade car view. Wanachofanya, wanaregister kampuni zote zinazoaminika ili kulipia kwa pay trade. Sasa iwapo kampuni uliyonunua gari imekudhulumu au halijafika, wataifatilia na kuona tatizo lilipo. Wakishamaliza uchunguzi wanakurudishia hela yako, ndio maana unalipa ile fee ya dola 150, yaani ni kama bima vile..
  Sasa ninachoona mimi, trade car view watakuwa wameshajiridhisha na kampuni zilizoopt kulipa kwa paytrade...na zile fee za wanaolipa dola 150 magari yao yakafika ndio zitakazokulipa wewe lisipofika, halaf wao watawadai wahusika kisheria zaidi.
  Bank yako haihusiki na malipo yako, kwani wao ni kama wakala tu wa kusafirisha pesa hapa. Its like m-pesa, hela zikiyeyuka utamdai wakala aliyekutumia au utawadai voda?
   
 10. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  In late March 2010, new Japanese banking regulations forced PayPal Japan to suspend the ability of personal account holders registered in Japan from sending or receiving money between individuals and as a result are now subject to PayPal's business fees on all transactions
   
Loading...